Dosari za Magufuli hizi hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dosari za Magufuli hizi hapa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kashaijabutege, Nov 16, 2010.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  1. Ni stageshow. Anapenda kuonekana anapotenda jema na anaongea kwa nguvu ili watu wamjue kuwa katenda. Ni mfuasi wa Mrema style.
  2. Ni msafi wa nje tu: Anajionyesha kwa watu kuwa ni msafi, lakini sivyo alivyo. Yeye si mwizi wa kujilimbikiza mali, bali ni "mwizi" wa kuwaangalizia wanaoiba wasishikwe. Kwa mfano, ilikuwa busara gani yeye kukubali nyumba 'za serikali' nyingi zilizojengwa na wakoloni ziuzwe kwa viongozi wa sasa wa CCM? Alisema Dr Slaa, inakuwaje hajawahi kuchoma nyavu zikiwa madukani (wauzaji), bali anachoma za wavuvi maskini?
  3.Anaamini sana takwimu: Takwimu zinasaidia kuamua, lakini si za kuaminisha asilimia 100%.

  NINAMPENDA MAGUFULI KWANI ANAWEZA KAZI NGUMU ZA KUKIMBIA KIMBIA, BUT HE IS NOT A STRATEGIC THINKER.
   
 2. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hizi fitna ni Uwaziri Mkuu au vita ya 2015 imeshaanza?
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tatizo lake ni nguvu ya soda.
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa umeliona eenhe

  Lakini pia tuone hoja zake maana zina mshiko
   
 5. K

  Kimambo Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 76
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  kashaija huna issue bora uende nyumbani ukabembeleze mkeo uliyegombana nae asubuhi
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Nov 16, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  acheni fitina Magufili anafanya kazi nzuri sana! kawakamata wezi wasamaki serikali imewachekea tuu! mlitaka afanye nini zaidi ya hilo na huyo mnayedhani ni mzuri kafanya nini! mtoto wa mkulima tumemwona na sasa amebaki kuwa Msukule tuu!!!
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Nilisikiaga kuwa anaendekeza hizi issues.....

  [​IMG]
   
 8. J

  Jafar JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tatizo CCM hawawezi kutoa Waziri Mkuu kwenye makabila "influential" - ukichukia haya shauri yako, japo haijaandikwa mahali bali huo ndio kumuenzi JKN (RIP).
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi zile nyumba alizo zifisadi alishazirudisha?
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  unajua mkuu tunaenda kwa system hii habari hakuamua yeye peke yake ilitoka juu! Mi sioni tatizo kama iliamuliwa na kina ben na yeye kama mtekelezaji akatekeleza!
   
 11. D

  Derimto JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huenda ukawa sahihi lakini tunaweza kumfananisha na Lowassa ambaye ni mchapa kazi mzuri na mtu wa maamuzi lakini hafai?

  Ni kweli Magufuli ana madhaifu yake mengi kama mwanadamu mwingine yoyote ila ikumbukwe kuwa tunatafuta kiongozi ambaye atakuwa angalau na unafuu fulani na kujali mali za nchi hii na hapa hatutafuti malaika kuja kuliongoza Taifa hili na nina imani kubwa atakuwa na watu wa kumshauri vizuri kulingana na aina ya uongazi wake na kuhusu nyumba za serikali kwanza nyingi hazikujengwa na serikali ila waliwanyang'anya wageni kama wazungu na wahindi waarabu nk. Na ilifika mahali ulikua ni mradi wa wakubwa fulani gharama za kufanyia matengenezo nyumba moja tu ni bora kuenga zingine mbili kifupi ulikuwa uchochoro wa kutisha malipo hewa ya wakubwa fulan na tena usisahau kuwa alikuwa anafuata wakubwa wake Sumaye na Ben wanataka nini apewe nafasi ajaribu. Akichemsha atapewa mwingine mwenye uwezo na watanzania wengi wanampenda siyo kwa kumwona bali kwa kazi ambazo tayari alikwisha kuzifanya
  Tuache majungu na kukosoa tu bila kuhesabu mazuri ambayo tayari kuyafanyia taifa hili.
   
 12. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Acheni majungu na fitna kwa watu wanaofanya kazi za wananchi na siyo za mafisadi. Ndiyo tunaelewa kuwa hakuna mtu aliyekamilika kwa 100% lakini kwa hayo unayoyazusha kwa Magufulu ni vigumu mno jamii kukuelewa. Hebu tafakari, ni waziri yupi aliyeweka rekodi kama ya Magufuli kwa ufanisi anaopata kila anapopewa wizara hata zile ambazo wengine mlifikiri kuwa hazina mchango wowote katika ukuzaji wa mapato ya serikali?
  Hayo unayotaka kutuaminisha ni dhahiri kuwa umetumwa na mafisadi uanze kumchafua mtu muhimu katika uongozi wa nchi yetu. Tunamhitaji sana magufuli hata kama ataomba kugombea uraisi 2015 ni mtu anayefaa na anaweza. Tunachotaka kuona kutoka kwa viongozi ni matokeo mazuri ya kazi zao. Magufuli ameweza kutoa matokeo mazuri kwenye kila wizara aliyopewa.
   
 13. c

  cerezo Senior Member

  #13
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mazuri yake?
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Huu ni utumbo una lako jambo:
  Naomba uelewe huwezi pata mtu msafi kwa 100% hata wewe siyo msafi 100%, kwani uamzi wakuuza nyumba za serikali ulikuwa wana nani na unajua malengo yalikuwa ni nini, nina vyofahamu mimi ilikuwa serikali iwe inajenga nyumba na kuwa uzia watu kwa kuanza na wafanyakazi wa serika kw bei nafuu na walikuwa wamepanga kuwatumia JWT ambao wanaujuzi mkubwa na kwasasa hivi wanaota vitambi tu hawana kazi yoyote. leo hii kama Magufuli angekuwa bado wizara ile ile tunge kuwa mbali sana, alisimamia magari yote ya serikari yaliyokuwa wamechukuliwa na mafisadi wote tuliona mpaka wakaanza kumsakama na kumtishia maisha hali iliyo pelekea kuwekewa ulizi maalum kipindi cha Mkapa, kama kuna mafanikio yaliyo patika kipindi cha Mkapa kwa nafasi kubwa Magufuli alichangia sana, Mafisadi walifanikiwa kumpa sumu akaenda kuponea ujerumani...Ni bifu la JK kumweka kwenye wizara ambayo siyo saizi yake kwa kweli ndiyo maana sitegemei kupewa uwaziri mkuu...Mnyonge mnyoneni lakini haki yake mpeni
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  zipi ile alimuuzia binamu yake au alizo wauzia wafanya kazi wa serikali?
   
 16. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #16
  Nov 16, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Nyerere aliwahi kusema ,watanzania wanapenda kuangalia makosa tu,hali halisi kuna mazuri mengi tu ambayo kama ungeyapiama basi usingeweza hata kuandika utumbo wako...:nono::nono::nono:
   
 17. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #17
  Nov 16, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna tetesi kuwa wale samaki waliobatizwa jina la samaki wa magufuli alitengeneza pesa nzuri kama kamisheni ya kuwahifadhi kwa mmiliki wa cold room mwenye asili ya kiasia kule mwenge. Maana hakukuwa na logic kuwatoa kwenye cold room ya meli ukawapeleka kwenye cold room binafsi halafu serikali ilipie ada ya uhifadhi huo ulikuwa ufisadi uliotukuka.
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Hivi sasa TANROADS ina kesi nyingi mahakamani zilizosababishwa na maamuzi yake yasiyoheshimu sheria.......................alijipatia umaarufu kwenye bomoabomoa ambayo ilifukarisha watanzania wengi bila ya fidia....................................................aliokolewa na fisadi lowassa wakati akiwa PM katika kashfa ya upoteaji wa zaidi ya bilioni kumi za barabara ambazo wengi waamini alizielekeza kibindoni kwake.................Waswahili husema ukiona debe tupu ujue halitaacha kutika......................na huyu Magufuli anatika kwa sababu ni mtupu....................ukiona karne hii ya 21 kiongozi anahangaika kurukia shahada ya mwenzie na yeye aonekana ana PHD ujue huyo hatufai............................
   
 19. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #19
  Nov 16, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Remember Waziri Mkuu ni kiongozi wa Mawaziri wengine ---> In this case hapana Magufuli sio chaguo bora!!!
   
 20. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #20
  Nov 16, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  MAGUFULI TUNAMHITAJI CHADEMA maana hatatughrimu sana kumsafisha amechafuka kiasi laikini anasafishika tutatumia maji kiasi akawa msafi.
  Hatuwezi kuchukuwa mtu kam LW itahitajika maji yote ya bahari ya hindi kwa ajili ya kumsafisha huyu jamaa ili afae.

  PIGA UWA GARAGAZA JK hawezi kumweka JPM kuwa PM kwasababu wanajua kwa mtazamo wa nje JPM ni CCM lakini damu yake siyo CCM.PIa kumbukeni huyu jamaa alikuwa kundi tofauti na akina JK ndo maana hata kwenye serikali ya JK yumo tu kwa sababu ya nguvu ya wananchi lakini hatakiwi!


  Mimi namshauri JPM kama ni mzalendo wa ukweli 2014 ahamie Chadema maana hata uchaguzi wa mwaka huu ameona alivyopata challenge jimboni kwake kwa matokeo ya awali nilidhani atapumulia machine siyo muda ....................
   
Loading...