Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ameandika katika ukurasa wake wa Facebook na kueleza kuwa Doreen amepata nafuu kubwa na sasa anatarajiwa kupelekwa katika matibabu maalum ya uti wa mgongo, Nebraska, Lincoln.
“Madaktari wataamua aende lini baada ya kuondolewa vyuma, tuendelee kumwombea apone katika changamoto alizonazo,” ameandika Nyalandu.
Doreen na wanafunzi wengine wawili, Saidia Ismael na Wilson Tarimo walinusurika katika ajali hiyo iliyotokea Mei 6 na kuua wanafunzi wenzao 32 , walimu wawili na dereva.
Chanzo: Mwananchi