Donors syndrome

Dua

JF-Expert Member
Nov 14, 2006
3,229
662
Fund Your Budget, Donors Tell Tanzania.

Damas Kanyabwoya The Citizen (Dar es Salaam) said:

NEWS
8 November 2007
Posted to the web 8 November 2007

The launching of general budget support in 2001 was in retrospect a milestone in efforts by the government and other stakeholders at making donor funding to Tanzania serve the interests of the country and thus produce the desired results.
Its main positive factor was its alignment to the national budget, an aspect that was expected to reduce donor conditionality and transaction costs. The donor money would have finally been used to fund Tanzanian budget priorities.
Whether the general budget support funding mode removed harsh donor funding conditionality making the money almost unusable remained an area of concern in the media and in government circles.

This was specifically so following the remarks by the British High Commissioner Philip Parham at the debut of the GBS meeting last week that the donors had prepared and circulated to the Ministry of Finance in September a matrix of donor conditionality on budget support. He said the matrix "summarizes the conditions of each development partner for the provision of future budget support. Our decisions and actions will be with these conditions. We want to avoid surprise, and to base decisions on regular, close dialogue with the government, at both Ministerial and official levels."

He said development partners will take all these things into consideration as they decide their budget support funding commitments for 2007/08. When cornered by the media and some government technocrats, Mr Parham said the conditions were nothing new and definitely were not the harsh traditional conditionality that the GBS has tried to avoid. The conditions are just to ensure monitoring and efficient use their money, "to avoid surprises."

After all donors have a right to see their money well spent, and also not all conditions are bad conditions. But what was of much concern to donors was how the government can become self-sufficient in budget funding in the near future. It was as if donors were becoming increasingly tired of funding the government budget. "We expect the government to be able to fund its budget entirely in three years to come," said David Stanton, the head of DFID in Tanzania.

Donors were highly concerned that despite abundant natural resources that the country has, revenue collection mechanisms were very weak and as a result the government was getting peanuts, and relying instead on foreign aid for budget funding. In forestry for example, donors said, only 27 per cent of all potential revenue was being collected.

The recent 'Discussion Paper on Forestry'by the Tanzania Development Partners Group estimated that revenue from forestry alone, if the sector was adequately and sustainably exploited, would be able to fund the current budget annually. Currently the revenues from forestry account for less than one per cent of the budget funding. Mr Parham said categorically that Tanzania must be fully aware and face the main budget challenges ahead. He said the $5 billion annual budget was still very small for a country of almost 40 million people, comparing the malnutrition situation in Tanzania to be equivalent to post-conflict countries of Angola and Liberia.

He said Tanzania is now rowing in calm waters and should use this chance to ensure it benefits and become self sufficient in funding its public expenditure. "This (GBS) review comes at a time of huge opportunity for Tanzania, arising from a happy confluence of positive factors. Tanzania must grasp that opportunity by attracting the necessary aid flows and using them effectively, and by quickly improving the environment for investment," he said.

He mention the factors as a strong foundation of stability, harmony and constitutional development, good macroeconomics, increasingly vigorous democracy and accountability, enormous economic potential, particularly in agriculture, tourism and minerals, considerable international goodwill and global liquidity. It was hard to tell whether budget self-sufficiency in the near future was part of government's main concerns in the GBS review meeting. Most of government presentations dwelt in technicality of the government budgetary process.

But what was absolute clear was that there was no timetable set by the government to graduate from aid. There was scarce talk from the government of setting a timeframe for budget self-sufficiency.

Its high time for the government to refuse foreign aid in our budget. We can't seriously depend on them to fund our budget and be free to choose what we want. Enough is enough and we should put our house in order.
 
wewe ota tu!

Shalom, sawa hii inaonekana kama ndoto... lakini ukweli wa mambo ni kuwa tukikomaa inawezekana kujitegemea. Mfano mzuri ndugu yangu ni Kenya...tusife moyo, tuwakomalie viongozi wetu, hata kwa kuandika tu hapa na kujadili mambo...

SteveD.
 
Shalom, sawa hii inaonekana kama ndoto... lakini ukweli wa mambo ni kuwa tukikomaa inawezekana kujitegemea. Mfano mzuri ndugu yangu ni Kenya...tusife moyo, tuwakomalie viongozi wetu, hata kwa kuandika tu hapa na kujadili mambo...

SteveD.

..we ulishaona wapi watu wanaopenda kuomba wakaacha kuomba?muulize matonya na nduguze watakueleza!

..kuomba kukishazoeleka kunakuwa kama utamaduni,wala watu hawaoni haya tena!

..mbaya zaidi unakuta mijibaba na mijimama mizima inaomba wakati ingeweza osha magari au pika mamantilie ikapata fedha tena nyingi!kumbuka uchumi tunao ila tunaukalia!

..kimsingi,ukiwa ombaomba hutoacha kuwa masikini siku zote za maisha yako!

..sasa,hali hiyo ndio aliyonayo tanzania!
 
inasikitisha sana mpaka leo hatuwezi kukusanya kodi zetu,sasa ikija kwenye kusimamia tulizozikusanya au kupewa msaada ndio tutaweza kweli,na hii teknoloji yote bado hatujaweza take advantage ili itusaidie,kazi ya serikali ni kukusanya kodi sasa kama hawawezi hiyo ni failure mbaya sana na tunazidi kuwa maskini tuu,wenzetu cheza na vingine lakini sio kodi yao mana utaishia jela au kukimbia nchi na usirudi tena
 
wewe ota tu!

BTW maneno hayo hapo juu ni ya donors wanakwambia hawawezi kuendelea kukupa dezo na wewe mpokeaji unawaambia waendelee kuota, I wonder nani anaota.

Tatizo lako kubwa binafsi na watu wengine kama wewe ni kutegemea misaada kwa mambo ambayo mnaweza kuyafanya wenyewe. Mimi sishangai kwa nini umeamua kwenda personal wakati unafahami fika kwamba katika viongozi wanafiki na wasiokuwa na aibu ni hili kundi ama genge ambalo tunalo hivi sasa wengi wao ni MAFISADI. Wanapokwenda mikutanoni na kuombaomba wakati uwezo tunao huwa hawaoni aibu? Hata siku moja huwezi ukaona wenzetu kama Wachina, Botswana au hata nchi ndogo kabisa kama Mauritius wakawapigia magoti mafirauni. Leo hii tunagawa mali asili yetu tena bure tu kwa sababu ya peremende, halafu tunapiga makofi kwamba tumesaidiwa.

Jiulize wewe mwenyewe binafsi unaweza kwenda pale kwenye makutano ya Nelson Mandela Road/Sam Nujoma na Morogoro Road na kungoja taa ziwake na kwenda kwa madereva na bakuli na kuomba chochote kwa madereva huku umemshika mwanao mkononi? Kama huwezi kufanya hivyo, Je, ni kwa nini Tanzania as a sovereign state ambayo inaweza kabisa kutumia nguvu ya dola na kukusanya kodi iende na bakuli kwa mafirauni. Huu ni umalaya na hatuwezi kuungalia kwa macho bila kuukemea. Hata watemi wetu hawakuweza kuuza utu wao; kumbuka historia ya Mkwawa, Mirambo na wengineo.

Sisi wengine hatukuzoea kuombaomba kama watoto waliozaliwa na ombaomba.

Serikali ingeweza kabisa kuchukua hatua hivi sasa (kwa mfano) ya kuweza kujenga nyumba za kisasa kwa wananchi na kuweza kusambaza gesi ambayo tunayo kwa wingi kwa matumizi ya nyumbani ili kuokoa matumizi makubwa ya umeme ambao ni ghali. Haya mambo yanawezekana ni kuwa na mipango madhubuti ya kuangalia jinsi tunavyoweza kufaidika na rasilimali zetu. Hatuwezi kila siku kusubiri maamuzi mabaya yanayofanywa na baadhi ya viongozi. (Vile vile gesi tutawauzia nchi zote majirani ambao hawana gesi.)

Mfano mwingine hivi sasa kuna uhaba wa cement serikali imechukua hatua gani kwa mfano kupunguza matumizi ya matofali ya cement (Blocks) kwa kuwa-encourage wajenzi kutumia matofali ya kuchoma? Fikiria ni ajira ya kiasi gani itapatikana kama hili likitokea? Kitu kinachotakiwa ni kuwa na standard ambayo itakubalika na TBS na funds kuwa available.

We can do a lot better kuliko kukaa na kutegemea akina Bill Clinton, Bill Gates, Bono etc. kuja kutujazia madola ambayo yanatafunwa na watu wachache na hata huko yanakoelekezwa yanafika kimkanda mkanda tu.
 
Tanzania ni nchi ambayo inauwezo kabisa wa kujitegemea ila inachohitaji ni kupata viongozi wenye sifa zifuatazo

1. Viongozi wawe na hofu na Mungu (wacha Mungu wa kweli) si ucha mungu wa kuhudhuria ibada hii itapelekea vitu kama ufisadi, rushwa, uzembe, uongo, ulevi, uasherati, nk kuwa ni hadithi tu

2. Wawe na uwezo wa ushawishi kwa wanachi na kutumia muda mwingi kuelezea jamii hasa kijijini nia yao ya dhati ktk yale waliyokusudia kiasi kwamba hata ukimwambia mwananchi kuwa tunafunga mikanda basi wamkubali

3. Elimu yao irandane na kazi au wajibu anaotekeleza na pia uzoefu wa kazi hiyo ou wajibu huo. Kama ni doctor awepo hospitalini na wala si ukuu wa wilaya au mkurugenzi wa jiji. Kama ni engeener awe ktk field yake na siyo kuwa mkuu wa chuo cha siasa kivukoni.
4. viongozi wawe na uwezo wa kubaini vipau mbele na hasa suala la kilimo na waweke limit ya muda wa kuwa ktk kilimo mathalan 2015 tuwe tumeachana na kilimu cha jembe la mkono na kuingia ktk klimo cha kutumia matrekta na by 2030 viwanda vya kusindika mazao ktk kata viwepo.

5. Wawe na uwezo wa kubaini ni elimu ipi inafaa kwa wakati unaofaa. Kama ni tech. school zinafaa wakati huu sawa na kama ni vyuo vikuu sawa wawe na huo uwezo.

6. Wawe na uwezo wa kubaini namna gani jeshi letu la wananchi linaweza kusaidia kuleta maendeleo mbali na kulinda nchi yetu; kuna la ziada jeshi letu pengine linaweza kusaidia

7. wawe na uwezo wa kuleta nidhamu ktk jamii hasa nidhamu ya matumizi ya mali tulizonazo na pesa kidogo tunazopata ni vitu gani tuanze navyo family wise. Familia zetu zinahitaji shule kutoka kwa viongozi wetu tunaowaamini juu ya matumizi yetu na future ya nchi yetu.

8. Namna ya kutumia vyombo vyetu vya habari vichache tulivyonavyo ktk kelimisha watu ktk masuala ya uchumi na kuwapa courage wananchi kuhusu future ya nchi yetu.

hizi ni baadhi tu ya sifa za viongozi wetu ambao wanaweza kutupelekea Tanzania yetu kuwa huru kutokana na misaada hii.Wanachi wako tayari ila wamekosa viongozi hao.
 
wewe ota tu!

Watu wengine bwana,!!!

Anyway, back to the topic. Ukisoma kwa makini hiyo habari unaweza kubaini mambo yafuatayo kwa haraka haraka:
1. Nchi ina rasilimali za kutosha lakini haiwezi kukusanya kodi
2.Pamoja na ukweli kuwa misaada (budget support, whatever) imeendelea kumiminika kwa takribani miaka 40, misaada hii inaonekana kudhoofisha nguvu ya serikali katika kukusanya kodi
3.Pamoja na ukweli kuwa misaada imeendelea kumiminika kwa takribani miaka 40, ukweli ni kuwa impact ya hiyo misaada haionekani kwa wananchi wa kawaida. Ndio maana wanalinganisha hali ya manultrition kwa nchi inayojisifia kuwa na amani na nchi zilizozotoka kwenye migogoro ya kivita kama Angola.

Sasa mwenzetu shalom unaposema "wewe endelea kuota" sijui unamaanisha nini hasa???

Nadhani tatizo kubwa ni kuwa imefika mahali hawa wafadhali wameona kuwa misaada yao haisaidii kuwajenga watanzania katika kukusanya kodi. Kwa hivi, serikali inabidi ichukue hizi comments za donors kama compliment rather than criticism.

 
Hilo kapu linavuja- kwa miaka 50 sasa- misaada ikisitishwa tutaendelea na kupata akili!
So je misaada for how long? now 50? what is time frame? Are we not becoming more dependent?
Hii misaada inamsaidia nani?
 
I dont believe on aid/handouts as a pre-requisite to develoment!

Nakubaliana na wewe 100% Ukiona jirani yako anatoa msaada wa chakula kwenye familia yako, kuvisha nguo wanao, na hela ya matumizi mengine ujue kuna kasoro hapo. Usishangae utakapopima DNA ukagundua kuwa hao watoto si wako. Sasa logic ndogo kama hii, viongozi wetu wanashindwa kabisa kung'amua??? Yaani wamefika mahala wanaona kama ndio utaratibu wa maisha vile!!! Disgusting!!!
 
Hilo kapu linavuja- kwa miaka 50 sasa- misaada ikisitishwa tutaendelea na kupata akili!
So je misaada for how long? now 50? what is time frame? Are we not becoming more dependent?
Hii misaada inamsaidia nani?

Hao wanaotia signature kwenye hayo makaratasi yanayobainisha kiwango cha pesa. Mtoaji na mpokeaji wote wanafaidika. Anayesahaulika ni "mlengwa" au mwananchi wa kawaida. Kwanza sina hakika hata kama huyo "mlengwa" huwa ni "mlengwa sahihi"
 
Kufa kufaana. Kipindi Cha njaa 2005/6 tuliomba misaada lakini ikaliwa vilevile. Umasisikini wa nchi yetu wanaosema wanaomba na wanakula. DHAMBI KUU KWA HAO WANAOKULA KWA MIGONGO YA MASIKINI
 
Nakubaliana na wewe 100% Ukiona jirani yako anatoa msaada wa chakula kwenye familia yako, kuvisha nguo wanao, na hela ya matumizi mengine ujue kuna kasoro hapo. Usishangae utakapopima DNA ukagundua kuwa hao watoto si wako. Sasa logic ndogo kama hii, viongozi wetu wanashindwa kabisa kung'amua??? Yaani wamefika mahala wanaona kama ndio utaratibu wa maisha vile!!! Disgusting!!!

Misaada mingi tunayopata ni kuendeleza mitindo ya maisha ambayo kabla ya uhuru ilikuwa haipo. Rais wa nchi hafanyi kazi mpaka awe na ndege maalumu. Viongozi wetu wanajua hilo na wakikataa misaada ni wao watakoathrika na sio sisi.
 
Labda huu ni wakati mwanana wa kutembelea maelekezo ya "siasa za ujamaa na kujitegemea"...

Posted Date::11/17/2007
Tusikubali misaada na sifa za matusi

Na Profesa Leonard K. Shayo

KATIKA mahusiano ya kimataifa, falsafa ya kutoa na kupewa inajumuisha wajibu, rushwa, fadhila, uporaji na biashara. Hakuna misaada ya nchi kwa nchi pasipo maafa. Msaada kwa binadamu asiye mlemavu, au kwa nchi isiyokuwa na maafa, ni tusi la nguoni.


Ni tusi la kuwakwaza wabunifu ili wasitumie akili zao kujiletea maendeleo. Pengine misaada inachukiwa kwa sababu, fahari ya kuishi ni kufanya kazi na kujitegemea.


Ndiyo maana baba wa kaya maskini hawezi kukubali baba tajiri ampe mkewe misaada, na wala mama wa kaya maskini hawezi kukubali mama tajiri ampe mumewe misaada. Maumbile yanawataka wanaojiweza watoe misaada kwa wasiojiweza, yaani walemavu, wagonjwa, wazee na watoto. Vitabu vitakatifu havijaamuru nchi tajiri zisaidie nchi zinazofinyanga umaskini.


Tunahoji kwamba, nchi tajiri zina wajibu wa kutoa sehemu ya utajiri kwa nchi maskini, kama ilivyo wajibu wa watu tajiri kutoa sehemu ya utajiri kwa maendeleo ya nchi zao.


Utajiri unapatikana kwa kupora jasho la maskini, na kwa maana hiyo ni wajibu wa matajiri kurudisha sehemu ya jasho hilo ili maskini wasigutuke wakadai haki yao kwa nguvu. Anayebisha kwamba utajiri hautokani na kupora jasho la maskini, ahamie kwenye kisiwa, halafu aone kama atakuwa tajiri kwa jasho lake mwenyewe. Uchumi wa nchi tajiri utaporomoka kama zitawekewa vikwazo vya kuthibiti uporaji wa rasilimali za nchi maskini.


Maskini ni binadamu aliyekosa kiungo muhimu cha kufanya kazi. Binadamu wazima wasiotaka kufanya kazi wamelaaniwa wasile. Kwa mtazamo huo, umaskini wa nchi haupo, maana hakuna nchi iliyokosa kiungo cha kufanya kazi. Utajiri wa nchi unatokana na matumizi bora ya bongo za wananchi wake, na Mwenyezi Mungu amezijalia nchi zote bongo za kutosha kujipatia utajiri. Tofauti ni kwamba, nchi nyingine zinatawaliwa na ubinafsi, unaozifanya zifinyange umaskini kwa kukataa kutumia bongo za watu wake kwa ufasaha.


Ni makosa kuita matoleo yenye masharti �misaada�. Matoleo ya namna hiyo ni rushwa. Laiti kama wachumi wa nchi maskini wangechambua undani wa masharti ya matoleo ya nchi tajiri, wangegundua kwamba yameficha makucha ya uporaji wa rasilimali za nchi hizo. Ndiyo maana umaskini unazidi kuota mizizi katika nchi kama Tanzania, licha ya kupokea kinachoitwa misaada, kutoka pande zote za dunia ya mataifa tajiri, kwa zaidi ya miaka arobaini na tano.


Ni makosa kuita matoleo yanayosukumwa na urafiki wa viongozi, �misaada�. Matoleo ya aina hiyo ni fadhila inayoweza kuwa ahsante kwa mauzo ya siri ya rasilimali za nchi maskini. Kwa mfano, kiongozi wa nchi maskini anaweza kufanikisha mauzo ya migodi ya madini ya nchi yake, kwa viongozi wa nchi tajiri, halafu akapewa fadhila kwa kazi hiyo. Fadhila inaweza kugawanyika katika mafungu mawili, moja la kibinafsi, na la pili likiwa ni matoleo yaitwayo misaada kwa nchi.


Ni makosa kuita marejesho ya sehemu ya faida �misaada�. Biashara za kidhalimu baina ya nchi tajiri na nchi maskini zinaweza kuzipatia nchi tajiri faida kubwa mno, kiasi cha kuwajibika kurejesha sehemu ya faida hiyo kwa nchi maskini, lengo likiwa ni kujenga mazingira bora zaidi ya kukuza biashara hizo, pamoja na kuibua biashara mpya za kidhalimu. Huu ni wajibu wa nchi tajiri kwa raia wake, wanaofanya biashara na nchi maskini.


Ni makosa kuita ujenzi wa miundombinu, katika nchi maskini, �misaada� kwa sababu miundombinu hujengwa kwa ajili ya kufanikisha uporaji wa rasilimali. Kwa mfano, ujenzi wa barabara ya lami kwa ajili ya kusafirisha dhahabu kutoka migodini kwenda uwanja wa ndege, hauwezi kuwa msaada. Ujenzi wa zahanati kwa ajili ya kutibu wafanyakazi katika shamba la miwa linalomilikiwa na wageni, hauwezi kuwa msaada. Hata ujenzi wa reli enzi zile za ukoloni haukuwa msaada. Reli zilijengwa kwa ajili ya kusafirisha mali ghafi, kama pamba, kwenda ulaya. Kung�olewa kwa reli ya Mtwara na Mpanda ni kielelezo hai. Rasilimali zilizokuwa zinaporwa ziliisha.


Ukweli ni kwamba, matoleo ya nchi tajiri kwa nchi maskini ni moja kati ya wajibu, rushwa, fadhila, uporaji, ama biashara ya kidhalimu. Kwa mfano. matoleo ya kufadhili wasomi, kutoka nchi maskini, katika vyuo vya nchi tajiri, ni uporaji wa rasilimali bongo. Uvumbuzi wa wasomi hao una thamani maradufu kulinganisha na gharama za ufadhili. Kama utafiti unahusu viwanda vya nchi tajiri, basi matokeo yake yatatumika kuboresha viwanda hivyo.


Kama utafiti unahusu uchumi wa nchi maskini, basi matokeo yake yatatumika kubuni mbinu bora zaidi za nchi tajiri kupora rasilimali za nchi hizo maskini. Kitendawili ni kwamba, nchi maskini zinatuma wanafunzi wake kwenda nchi tajiri kupata shahada, bila kujali ni ya kitu gaini.


Kama vile kashfa hiyo haitoshi, wasomi wanaporudi wanahamasishwa wafanye tafiti kwenye eneo lolote, hata kama halina maslahi kwa taifa lao kwa miaka elfu moja ijayo. Ndiyo maana hatuoni aibu kuendelea kupokea fedha kutoka nchi tajiri kwa ajili ya kufadhili tafiti za wasomi wetu. Hii ni kashfa inayoimarisha mila ya kutegemea wageni.


Tunahoji kwamba, matoleo mengi, yanayoitwa misaada kwa makosa, ni ya kulemaza bongo za wazalendo ili zisinzie milele. Ni sindano za usingizi, tunazodugwa kila tunapoonyesha dalili za kuamka. Kwa kuwa mishipa ya fahamu ya nchi ni viongozi wake, wataalam wa kudunga sindano hizo wanawatafuta kwanza viongozi wa nchi maskini. Wataalam wa uporaji wanaweza kuwamwagia viongozi hao sifa za matusi, ama kuwapa rushwa, kama hatua ya kuwaandaa kudungwa sindano za usingizi.


Kwa mfano, katika karne hizi za sayansi na tekinolojia, ni matusi kwa nchi tajiri kumsifu kiongozi wa nchi maskini kwa jitihada za kujenga shule za msingi au visima vya maji, au kwa kukaribisha wawekezaji kutoka nchi tajiri. Wanatakiwa wasifiwe kwa kupora tekinolojia kutoka nchi tajiri, na kwa kujenga viwanda vinavyomilikiwa na wazalendo.


Matoleo ya nchi tajiri kwa ajili ya kujenga vibarabara vidogo, au visima vya maji, au vyoo, au madarasa, katika nchi maskini, ni kashfa ya ubaguzi wa bongo. Kunaashiria kwamba, wabongo hawana uwezo wa kufanikisha ujenzi huo, na wala hawajui matumizi bora ya fedha za kigeni. Je, ni vipi tulipiga vita ubaguzi wa rangi, halafu tunaruhusu ubaguzi wa bongo? Rangi ilibaguliwa, halafu ikakombolewa na bongo. Je, ubongo ukibaguliwa, utakombolewa na nani?


Mahusiano sahihi kati ya nchi na nchi ni ya biashara za kistaarabu. Hizi ni biashara za uwazi na za kutumia mbinu za kisayansi kuchambua faida na hasara. Kwa maana hiyo, ni biashara za kutokomeza umaskini. Tatizo ni kwamba, ubinafsi wa viongozi wa nchi maskini unafungua milango kwa waporaji. Siku zote, lengo la mfanyabiashara ni kupata faida kubwa iwezekanavyo, na kwa maana hiyo waporaji hawawezi kulaumiwa ikiwa watakuta milango wazi usiku.


Viongozi wa nchi maskini wanapaswa wajiulize maswali kadhaa, na wapate majibu, kabla ya kupokea matoleo yanayoitwa misaada. Maswali hayo yanajumuisha yafuatayo. Je, ni kwa nini zinapewa misaada angali nchi hizo siyo vilema?


Je, wanaozipatia misaada wanataka kupata nini? Je, mila ya ombaomba itayafikisha wapi mataifa maskini? Je, ni taifa lipi liliondokana na umaskini kwa kukumbatia sera za ombaomba? Je, nchi maskini zitakwepaje athari za kukimbilia misaada? Shida ni mama wa maarifa, na kamwe nchi haiwezi kupata maendeleo kama wataalam wake watawekwa kando katika ufumbuzi wa matatizo ya nchi.


Viongozi wa nchi maskini wanatakiwa waelewe kwamba, misaada pasipo maafa ni rushwa ya kuandaa mazingira ya kuuza nchi. Waelewe kwamba, rushwa inatumika kulinda rushwa. Je, ni mbinu gani zitumike kuvunja miduara ya rushwa?


Tunanena kwamba, matatizo ya kiuchumi yanayozikabili nchi maskini yanajikita kwenye miduara ya rushwa. Kwa kuwa rushwa na ubinafsi ni kaka na dada, vita dhidi ya rushwa haiwezi kufanikiwa kama wenye dhamana ya kutokomeza rushwa watakuwa na chembechembe za ubinafsi au rushwa.


Je, mamlaka zinazoteuwa wataalam wa kutokomeza rushwa zinaweza kuwa takatifu, halafu zikateuwa wataalam walarushwa? Tunahoji kwamba kuwepo, na kuendelea kuwepo kwa walarushwa miongoni mwa wataalam wa kutokomeza rushwa, ni ushahidi tosha kwamba, mamlaka zilizowateuwa ni za walarushwa.


Kwa upande wa Tanzania, ni vema kama wakuu wa nchi watahakikisha kwamba, wataalam wa TAKUKURU ni watakatifu katika upokeaji na utoaji rushwa. Vinginevyo watajipaka matope, maendeleo hayatakuwepo, na tutaendelea kunyanyaswa na wageni wanaotumia mbinu chafu kwa ajili ya kuhalalisha uporaji wa rasilimali zetu. Nchi maskini zinahitaji viwanda, zinahitaji sayansi na tekinolojia, na zinahitaji uhuru wa kutumia bongo za wazalendo kutatua matatizo ya nchi.


Profesa Leonard K. Shayo ni mtaalam wa Hisabati na Program za Kompyuta

Mobile: 0754 288 179 E-mail: shayolk-at-yahoo.com

Source link: Mwananchi.

SteveD.
 
Donors were highly concerned that despite abundant natural resources that the country has, revenue collection mechanisms were very weak and as a result the government was getting peanuts, and relying instead on foreign aid for budget funding. In forestry for example, donors said, only 27 per cent of all potential revenue was being collected.

Well hii ndio sifa kubwa aliyoipata Mkapa kwa hiyo leo mnashangaa kitu gani haswa?. tuliwambieni toka mwanzo sio swala la ukubwa wa fedha in millions bali ni kiasi gani cha asilimia ya fedha zinazokusanywa kulingana na vyanzo vilivyopo. Ndio hayo ya madini kuchangia asilimia 1.9 mfuko wa taifa imekuwa mshtuko mkubwa kwa baadhi ya watu waliokuwa wakisoma amount za mabillioni bila kufahamu kwamba kampuni ya bia ama sigara,kodi zetu za mishahara na pengine hata Bakhresa wote hawa kila mmoja wao huchangia mfuko wetu kwa aslimia kubwa kuliko madini. Hesabu za Nkapa ziliwapiga tobo wengi 2+2 = 22.
 
Hii naona itabakia kuwa ndoto. Ndoto za watu Weusi Amerika zimesikika kinamna yake, sijui kama sisi tutaweza. Hata hivyo mambo yote yanaongozwa kwa nia, hiari na malengo. Siku tutakapokuwa na hivi vitu tutaweza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom