Dondoo za usaili (Interview Tips) na Cv nzuri

Pconnect

Senior Member
May 4, 2014
134
225
Shukrani wakuu kwa kuendelea kutuamini iPointPro kwa huduma za kutengeneza Cv nzuri kwa bei nafuu kabisa. Online delivery service.

Wasiliana nasi kupitia pamojalite@gmail.com au tembelea ukurasa wetu wa Instagram iPointPro kwa sampuli zaidi.

Umeshawahi kujiuliza referees wako wanakuzungumziaje pindi wanapotafutwa na waajiri? Je wanakufahamu/ wanakukumbuka?

Pitia dondoo hii;

Referee ni mtu yoyote anayeweza kuthibitisha wewe ni mtu wa namna gani na uwezo wako wa utendaji kazi. Referee anaweza kuwa mfanyakazi mwenzio, mteja n.k hivyo chagua wanaokufahamu na wenye uwezo wa kuongelea mambo mazuri kukuhusu.

Nukuu ya mdau kutoka Twitter “Wabongo tuna roho mbaya, mtu anakuweka kwenye CV as referee alafu una mkana! Asubuhi nimepigiwa simu landline ya waajiri, wanashangaa referees wanamkana binti wa watu ambaye anatakiwa kwenye interview Jumatano ya kesho kutwa. Atleast mimi nilikubali kuwa namfahamu” - #Chapo

Unapaswa kuwaeleza adhma yako ya kutaka kuwatumia kama referees ili wawe na utayari pindi wanapotafutwa na waajiri kuulizwa maswali kukuhusu.

Zingatia kupewa majina sahihi, nafasi zao kazini na namba za simu/ barua pepe/ anwani pia ni vyema kupata referees wanaoendana na maombi ya kazi unayotuma kwenye makampuni/ taasisi ukizingatia zaidi kuwaweka referees ambao watakuwa rahisi kwa waajiri kuwafikia pale wanapohitaji maelezo kukuhusu.

Vilevile kama hujawahi kufanya kazi popote (Wahitimu) ni vyema ukawatumia wakufunzi/Waalimu /Wakuu wa idara wa shule/ Chuo ulichosoma ambao unaamini wanayo mazuri ya kuzungumza kukuhusu.

N.B Angalia sampuli (Sample Cv attached) na tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya COVID-19 kama tunavyoelekezwa na wataalam wa afya.
 

Attachments

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom