Donald Trump: Rais aliyeharibu makubaliano ya JCPOA

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Marekani hawajawahi kupata rais mpuuzi, mpumbavu na kichaa kama Donald Trump

Huyu Bwana akili zake hazikua nzima, ni Rais aliyeitia dunia hasara, na aliyewatia Marekani hasara

Jamaa alianzisha vita ya biashara na China matokeo yake yakaathiri hadi za dunia ya tatu, Shipping cost ziliongezeka duniani kwasababu ya mwanasesere mmoja tu kutoka Washington. Mnaoagiza bidhaa nje ni mashahidi, matokeo ya vita ya biashara yalipandisha sana gharama za kusafirisha mizigo, hiyo ni athari moja tu iliyonikumba hata mimi na biashara zangu za kununua mizigo kwa makontena kutoka China.

Nirudi kwenye makubaliano ya JCPOA ambayo ni Joint Comprehensive Plan of action

Yalikua ni makubaliano ya Nyuklia kati ya Iran na madola makubwa duniani

Ambayo ilikua ni makubaliano kati Ya Iran na kundi la 5+1 ambayo Ni US,UK,Russia,China,France+Germany pia EU ilihusika

Yalifikiwa vienna july 14 2015. Haya ni makubaliano ya kipekee ya karne yalowahi kufikiwa na kuwa na uzuri na sifa na rekodi ya aina yake Soma zaidi Joint Comprehensive Plan of Action - Wikipedia

Nitakuja kuchambua kwanini nasema yalikua ya aina yake nikijaaliwa muda

Huyu Trump alivyoingia akafuta makubaliano ya Iran na kuanza kuitia Iran vikwazo vya kidhulma nasema ni vya kidhulma maana havikua na tija maana iran ilikua ishaachana na mpango wa nyuklia na kuingia mezani na kupata makubaliano.

Akafuta akijitapa lakini nikuulize kulikua na faida gani ya trump kuvuruga haya makubaliano? Haya makubaliano yalikua muhimu mno kwa dunia na ustawi duniani lakini akaharibu. Trump na yule bwana wanafanana na wote wameishi na kutawala kwa term moja tu

Sijui walimuokota wapi huyu na kumpa nchi watu kama trump hawafai kabisa na ni hatari sana kwa usalama wa dunia

Jamaa aliharibu makubaliano ya Jcpoa kwa matakwa yake binafsi na kukurupuka

Soma zaidi mwanzo mwisho ujuwe kwanini Jcpoa ilikua ni the best agreement ever
 
Acha chuki. Trump was and is the best American president I have ever known. He left countries to grow freely unlike other presidents who interfere internal affairs of other nations particularly Tanzania, Africa. I real love him. I wish he run again for presidency in 2024. He cares about Africans. He is a peace keeping President and God fearing. #TRUMP2024
 
Marekani naona ipo kwenye Relative Decline

Mbinu yanayoitumia kulinda Hegemony yao imepitwa na wakati

Na kinachowatisha zaidi ni Uchina

Ni wazi wanaenda kuwa dethroned Kutoka kwenye u super power na kitu ambacho hawapo tayari kukikubali kirahisi

So hizo attempts za kina Trump ni katika kuizuia uchina

Binafsi sidhani kama wamepata rais yoyote wa maana hapa karibuni
 
Marekani naona ipo kwenye Relative Decline

Mbinu yanayoitumia kulinda Hegemony yao imepitwa na wakati

Na kinachowatisha zaidi ni Uchina

Ni wazi wanaenda kuwa dethroned Kutoka kwenye u super power na kitu ambacho hawapo tayari kukikubali kirahisi

So hizo attempts za kina Trump ni katika kuizuia uchina

Binafsi sidhani kama wamepata rais yoyote wa maana hapa karibuni
Ila China hawatamsahau Trump, jamaa aliwalima sanction za hatari
 
Acha chuki... trump was and is the best American president I have ever known... he left countries to grow freely unlike other presidents who interfere internal affairs of other nations particularly Tanzania, Africa. I real love him. I wish he run again for presidency in 2024... He cares about Africans... He is a peace keeping President and God fearing... #TRUMP2024
Daaa Trump anapenda Now US, na kwenye Republican hakuna wa kumshinda lazima atagombea Tena 2024
 
Kudondoka kwa hegemony ya Us ni kudondoka kwa Hegemony ya Whites wote duniani.

Kwasababu hiyo sio rahisi kihivyo Whites kupoteza Hegemony yao kwa Race nyingine (china) et kwasababu ni magwiji wa kopi na pest.
 
Hakuna mpuuzi yeyoye anayeweza kumiliki ghorofa Manhattan, New York. Wewe mtoa mada jipime Kama unaweza kumiliki hata kiwanja tu Azikiwe street, Dar
 
Back
Top Bottom