Donald Trump piga marufuku viongozi wa nchi za kiafrika kutibiwa Marekani

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Kama ambavyo huwa mnapiga marufuku watawala madikteta na wasiofuata utawala wa kidemokrasia kuingi nchini Marekani,nakushauri upige Marufuku viongozi wa nchi za kiafrika kutibiwa Marekani na kama ni kuweka sheria basi hakikisha kunakuwa na sheria ya aina hiyo nchini mwako.

Badala yake nakushauri uweke sera ya kusaidia nchi za kiafrika katika swala zima la kuboresha huduma za afya kama vile kutoa mafunzo kwa watalaam wa Afya, kusaidi vifaa vya matibabu,n.k lakini sio kuendeleza hii kasumba ya kupokea viongozi wa kiafrika wanaokuja huko kutibiwa ili hali nchi mwao huduma za afya ni mbovu huku wananchi wao wakikosa hata madawa.

Mmewaendekeza vya kutosha na bahati mbaya hawaonekani kujiingeza.

Enough is enough.
 
Ndio hivyo wajenge hospitali bora makwao.......

Nakumbuka tezi dume jamaa alienda mwezi mzima......
 
Back
Top Bottom