Donald Trump kukabidhiwa Ikulu ya Marekani leo.

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945

Mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba Donald Trump leo anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani.

Bw Trump wa Chama cha Republican anatarajiwa kuapishwa mbele ya watu 750,000 mbele ya majengo makuu ya bunge la Marekani, Capitol Building, Washington D.C.

Kisheria, rais anafaa kuapishwa kabla ya saa sita mchana saa za Amerika Mashariki ambazo Afrika Mashariki ni saa mbili usiku.

Hii hapa ni ratiba fupi ya matukio yanayotarajiwa siku hiyo.

Saa 17:30 (Saa za Afrika Mashariki) Wanamuziki walioalikwa wataanza kutumbuiza.

19:30 Hotuba za kufungua sherehe zitaanza kutolewa.

20:00 Muda mfupi kabla ya saa Mbili Afrika Mashariki Donald Trump atalishwa kiapo cha kuwa rais wa Marekani na Jaji wa Mahakama ya Juu John Roberts.

Baadaye, kutakuwa na msafara baada ya sherehe ya kuapishwa ambao utaanza katika vidato vya jumba la Capitol Building kuelekea ikulu ya White House kupitia barabara maarufu ya Pennsylvania Avenue.

Bw Trump na mkewe Melania baadaye watacheza dansi katika matamasha matatu, mawili katika ukumbi wa mikutano wa Walter E Washington na jingine katika ukumbi wa Jengo la Makumbusho ya Taifa.

Miaka minane iliyopita, Rais Obama alipokuwa anaapishwa kura rais, waliohudhuria walikuwa watu 1.8 milioni.

Siku moja baada ya kuapishwa kwa Bw Trump, wanawake takriban 200,000 wanatarajiwa kuandamana Washington DC na miji mingine kumpinga Bw Donald Trump.

Hillary Clinton na mumewe Bill wamethibitisha kwamba watahudhuria sherehe hiyo, sawa na George W Bush na mkewe Laura.

Wamesema wanataka “kushuhudia kukabidhiwa madaraka kwa rasi mwingine kwa njia ya amani.”

Rais mwingine wa zamani Jimmy Carter atahudhuria pia, lakini George HW Bush, 92, na mkewe Barbara hawataweza kwa sababu za kiafya.

Chanzo: BBC Swahili
 
Wazungu nao bwana!! Sasa hao wanawake wanataka kuandamana kumpinga ili iweje? Wakubali tu maana ndio anaapishwa hivyo. Wawe wapole tu maana hamna namna, kama sisi huku TZ tunavyoisoma namba, maana tulibugi wenyewe.
 
Lakini pia wataruhusiwa kuandamana, maana ni haki yao ya kikatiba. Siyo kama huku kwetu katiba ya nchi inakanyangwa kila siku. Kwani wakiandamana watawala wanapungukiwa nini?
 
Igwee! Leo ndio leo baada sintofahamu kibao hatimae bwana donadi anaapishwa kuwa presidaa wa marekani hivi inakuaje tunapo aminishwa kuwa USA ndio kitovu cha demokrasia halafu wanamkubalia mtu alie shinda kwa kutumia mgongo wa nyuma hivi kwa mtindo huu si ndio maraisi wa Afrika watafia madarakani?Hivi wamarekani walio shindwa wata muunga mkono huyu jamaa?Pia yule Mrusi aliye mpa sapoti donadi si atataka fadhila?Naona kama kuna anguko la Marekani vile?
 
mleta m

mleta mada utakuwa ni mtu wa kutokea kulee kwenye kijani sio bure
 
et donadi...unaona anguko la marekan..??mkuu unga wa sembe kilo 1900 pambana njaa inakuja tz sio America
 
Marekeni hata ukimweka Pdidy kuwa rais taifa halitaanguka;
tatizo ni huku kwetu, mara njaa, mara kipindipindu, mara mafuriko.
 
Back
Top Bottom