Donald Trump Hawezi Shinda Urais Marekani Nov 2016

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Kuna wanaoamini Trump, Atakuwa Rais wa 45 wa Marekani Katika Uchaguzi wa Nov 2016, Iwapo Akishinda Tikiti kwa Chama chake huo utakuwa ndio ukomo wa safari yake ya Kujikweza, Ubaguzi na Kebehi

Hawezi Kushinda, Wanaomshabikia, Trump kwao Ni Kama Kioo, Anaakisi Tabia zao, Anasema maneno ambayo siku zote wangetamani Kusema Lakini Hawawezi. Trump Kumuita Ni Juha, Mbaguzi wa Rangi nk. Maneno ya Kwenye Kamusi hayana Uwezo wa Kusisitiza Ukweli huo. Siku za Usoni Naamini watu wenye Tabia Kama zake wanatakiwa waitwe kwa jina neno moja tu Trump!

On a much more serious Note, Trump hawezi Kushinda kwa sababu Zifuataza,
Marekani Kuna Vyama Vikuu Viwili, Na Vyote Viana Mambo Vimeegemea na Aina ya Wafuasi.

Republican:- Hawa Wanaegemea zaidi, kwenye (a) Uhuru wa Kumiliki Bunduki (a) Wanachukia Kodi (c) Kisirisiri ni Wabaguzi wa Rangi na Wanadharau sana Raia wengine wa Dunia. (d) Wengi ni wazungu, Wengi ni wa sehemu za Kusini, wengi hawajasoma, hata Kama wakiwa wamesoma ukiwasikiliza argument zao kwa Maswala mbalimbali Utatamani Kulia. (e) Wanadharau Sayansi (f) Wanapinga abortion (g) Wanashabikia sana Vita (h) Wanavaa Ukristo Begani. Theodore Roosevelt, Dwight David Eisenhower, Richard Nixon, George W Bush, George H Bush, Ronald Regan, Ni Baadhi ya Marais waliotokea Chama Hiki. Tangu Uhuru Chama Hiki Kimetoa Jumla ya Marais 18

Sasa Ukiwa Unataka Kugombea Kwa chama chao Ukiwa Mjinga sana Utajitahidi sana Kujihusisha na Maswala hayo hapo juu, ili Uwashinde wengine ambao nao wanataka chama Kiwape Tikiti. Ubaya Ni Kuwa Kuna Point of No Return au Mstari Ukiuvuka basi Utakasirisha Kundi ambalo Ni Muhimu sana Nitalitaja baadaye. Trump ameshavuka huo mstari 4X4

Democrats :- Hawa Wanaegemea zaidi kwenye (a) Kuheshimu Utawala wa sheria (b) Kuthibiti umiliki wa silaha (c) Kuruhusu mwanamke Kuamua juu ya Uzazi* (d) Wanajifanya Hawashabikii Vita(mara nyingi sio kweli) (e) Wanaamini Matajiri wanatakiwa walipe Kodi zaidi (f) Wangetamani Huduma za afya ziwe Bure (g) Wengi ni Rangi Mchanganyiko, Wengi wamesoma na Kama hawajasoma wanafikiri kwa Kichwa sio kwa maninii, Wengi wanakuwa ni wa sehemu za Kaskazini, Wengi ni wa Kipato cha Kati. (h) Bahati mbaya wanashabikia Ushoga. [URL='https://en.wikipedia.org/wiki/Franklin_D._Roosevelt']Franklin D. Roosevelt, Harry S. Truman, [/URL]John F. Kennedy, Lindon Johnson, Jimmy Carter, Bill Clinton na Barack Obama Ni Baadhi ya Marais waliotokea chama Hiki. Tangu Uhuru Chama Hiki Kimetoa Marais 16

Pia Ukiwa Unataka Tikiti ya chama hiki lazima uonyeshe upo nao kwenye core-values zao. Pia Ukivuka Mstari Mwekundu Utawaudhi Lile Kundi Muhimu na Hutashinda.

Marais Wengine Jumla yao 10 Walitokea Vyama Vingine vya Wakati wa Uhuru ambavyo Vyote Vilishakufa zamani sana. (Nashangaa Ni lini CCM nayo Itakufa) Hili Nimechomekea Tu.

Kundi Lingine Ambalo pia Limeovalap Kidogo na Makundi hayo mawili hapo juu, Ni Kundi muhimu sana, La Watu au Wapigakura Independent ambao Mara Nyingine wanaitwa Swing Voters. Huwezi Kamwe Kushinda Urais Marekani Bila Kupata Kura za Kutosha Kutoka Kundi hili, Ili Ujazie na zile za Kundi lako la Msingi. Kundi Hili Linajumuisha. (2) WAROMANI KATOLIKI(2) WATU WANYE ASILI YA KILATINO(3) WAMAREKANI WEUSI(4) WASOMI NA WAKUFUNZI WA VYUO.

Sasa Wote Hawa Donald Trump Kawakorofoa, Anabeza weusi, Amesema Mbofu sana Juu ya Walatino, Ameingia Katika Mabishano na kumjibu Kunya Pope! Wasomi wanaona Kuwa Trump ni Juha, sasa Niambie Ni Muujiza wa Namna Gani Utamwezesha Kushinda? Ingekuwa Tanzania Ohhh yes Zingenyang'anywa Computer na Vijana Kadhaa Kuwekwa ndani, na maji ya Upupu, Kisha Mtu unatangazwa mshindi. Kwa Kuwa Marekani Mauzauza hayo hayapo. Safari ya Urais ya Trump Ni safari ya Mtu Aliyeshika Sinia La Dhahabu Akimpelekea Ushindi Hilary Clinton au Ben Sanders. Most Likely Hilary.
 
Marekani hakuna kukatwa kama saccos ya CCM mkuu kuwa mpole anaongea anachoamini kama anavyofanya Magufuli
 
Marekani hakuna kukatwa kama saccos ya CCM mkuu kuwa mpole anaongea anachoamini kama anavyofanya Magufuli

Hapana Mzee Siasa za Marekani Ni Mahesabu Makali, Ukiongea Mbufu tu Unaweza Ukawafurahisha Kundi lako lakini Itakugharimu. Watu wako sensitive, Wewe Utamtukana Pope utegemee wakatoliki wakupigie Kura? Umelogwa!
 
Donald Trump kasema ukweli tupu kuhusu sisi watu weusi, japo unauma!

Kwamba Ni Kweli Waafrika Ni kama manyani na Wakijuacho Ni Kujamiiana tu, Kwamba sisi ni low life, "Maisha yasiyo na thamani?" Tafadhali! Kwamba Walatino Ni walanguzi wa Mihadarati, Wanawake wao wanamatumbo kama Water Melon, Na wanaume wao ni wabakaji? Kwamba ataua familia za watu Magaidi. Kwamba ataenda nchi zenye mafuta na ayachukue kwa Nguvu, (akasema specifically Iraq) Hivi Uchina u Urusi na wao wakienda Saudi Wakaamua wachukue mafuta kwa Nguvu atawaambia acheni? Trump si Mbaguzi tu, si mwenye majivuno tu, Bali ni Idiot (Juha) na Mwehu (Mgonjwa wa Akili)

Na by the way Ni Mtapeli, Sio Kuwa anautajiri anaosema, Kwa Domo Lake Kubwa Mabenki na Makasino wanamlipa Kutumia Jina Lake Utajiri wake halisi haufikii Bilion $3 Aliko Dangote anamzidi Mara kumi, Bill Gates anamzidi mara 20, Alina Warren Buffet, Michael Bloomberg etc. Hana utajiri wa Kiasi hicho.
 
Jamaa kaongea kweli ,ila kiongozi kama trump anafaa sana kwa kuwadhibiti viongozi kama m7,kagame,mugabe,nk
 
Nikajaribu kuguatilia watu wanao mchukia trump ni wache kuliko wanao mpenda.
Na hao wachache wanao mchukia wanalalamika akipita trump dunia nzima kutakuwa na vita .
Mimi nasema hapana lengo la trump sio kuleta vita ila ni kuiweka dunia katika mstali na hao wanao mtafsili trump vibaya na hao ndio watakao leta vita kutokana na ujinga wao.
Mbona mpaka saizi kuna watu wanawalalamikia wamarekani kwamba ndio wanao wachonganisha nchi za kiarabu ili wawe wanaiba mafuta lakini swali linakuja je kama adui yao ni mmarekani.
Kwanini nao wasielewane tu harafu nao waunde umoja wenye nguvu.
 
.. nimemsikiliza Trump kwa makini mara kadhaa ktk midahalo & townhalls. Mwanzoni nilikuwa namchukulia vingine lakini nimegundua ni mtu makini, na tusije shangaa atakapopata nomination & baadaye kushinda uchaguzi mkuu
 
Nadhani kichwa cha habari kingekuwa 'Sitaki Donald Trump Ashinde 'kwa sababu ulizozitoa wewe ambazo nyingi ni binafsi zinazotokana na wewe kuwa liberal.Watu wengi wanaompenda Trump sio kwamba wanampenda kwa siasa zake ,ama labda yeye ni bora zaidi ya Hao wengine hasa Hillary,Sanders Cruz Jeb etc,la hasha isipokuwa ni kwamba wanaona jamii kubwa ya hawa wagombea ni vibaraka wa makampuni makubwa ya Wallstreet hasa Hillary,na kwamba pindi watakapopata madaraka ,watalinda na kuendeleza na kutekeleza matakwa ya haya makampuni makubwa kwa kuwa upande wao na kutunga sheria kupendelea kundi hili huku wakiacha jammii kubwa ya wamarekani wakiwa hawawajali.
Kuhusu Swala la kushinda ni bora ukawa na subira mpaka matokeo yatakapotangazwa kwa sababu Hillary anayepewa nafasi kubwa kushinda Democrats Emailgate kwanza inaweza kumuondoa kwenye kinyang'anyiro(Endapo atapatikana kuwa na kesi ya kujibu (Indicted) kwa sakata la kutoa nyaraka za siri katika server ya Serikali na kuhamishia kwenye Server yake binafsi na hivyo kuhatarisha usalama wa nchi yao) Pili hata akipitishwa na chama chake atakuwa na kazi kwa wamarekani ambao wanamuona kama mwenye uchu wa madaraka,mwongo na anayeweza kuhatarisha maisha yao. Wachambuzi wa mambo wanasema Endapo Sanders atapitishwa basi hatakuwa na ubavu wa kupambana na trump hivyo democrats kushindwa wanategemea labda Mayor wa zamani wa New York anaweza akaokoa jahazi ambaye naye anaonekana ni kibaraka wa wallstreet. Kwa hiyo kutookana na upepo ulivyo ni bora tusubiri uchaguzi utakuwaje.
 
Back
Top Bottom