Donald Trump ajitangaza mshindi kabla ya matokeo ya mwisho

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
990
1,000

Katika hali ya kushangaza dunia, Dinald Trump rais anaetetea kiti chake kajitangaza mshindi kabla ya matokeo ya mwisho.

Mpaka sasa Trump ana kura za wajumbe 213 huku Joe Biden akiwa na 238.

Mshindi anatakiwa kuwa na kura za wajumbe (electoral college votes) kuanzia 270 au zaidi ili mwaka 20 January aweze kula kiapo.

Trump ana advantage ya kushinda kura za wajumbe wa Florida na Ohio; in most case haya huwa ni swing states na mara nyingi huwa yana amua hatima ya uchaguzi.

Kama Trump akishindwa na alijitangaza mshindi kabla, itapelekea huko.mbele mgogoro wa nini tafsiri demokrasia na kuheshimu tasisi za kidemokrasia.
 

Yudatade Edesi Shayo

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
2,874
2,000
Trump ajitangazia ushindi licha ya mamilioni ya kura kutukuwa zime hesabiwa hatari sana!!viongozi wa chama tawala wamepinga matamshi ya mgombea wao kuwa hayana ushahid

Usiku wa leo mamilioni ya kura za wizi zilikamatwa kumbe siyo africa tu hata huko
IMG-20201104-WA0001.jpg
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
4,464
2,000
Trump atatushangaza kama awamu iliyopita..

Katika states 9 zilizobaki.. trump atashinda states 3 zenye electors wengi... na kumuachia bidden states 6 zisizo na electors wengi...

Trump anashindanga states za wazungu wenye uchungu na nchi yao... matokeo ya michigan, florida na ohio ndio yatasema ukweli kama trump anarudi ama anaandamana kaibiwa kura
 

Chenchele

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
1,754
2,000
Kwani kura ni ngap kwa ngap mkuu
Biden 238
Trump 213

Zimebaki 87 electoral votes.

6+10 anaongoza Biden
Trump anaongoza mengine matano including Alaska. Akishinda yote anashinda Kwa 284 as 270 ndiyo target.

Hata hivyo Kura za email bado zinahesabiwa, Biden Yuko projected kuchukua states.

Anyway let's watch.
 

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,208
2,000
Mgombea Urais wa Marekani Donald Trump amesema amenusa viashiria vya mchezo mchafu (udanganyifu) kwenye matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kutangazwa na kusema licha ya kwamba matokeo ya mwisho ya jumla hayajatoka yeye tayari ni Mshindi.

"Kuna udanganyifu, hii ni aibu kwa Marekani, naenda Mahakamani ili mchakato wa upigaji kura usimame hatutaki zikutwe kura asubuhi na kura zinaongezwa kwenye orodha"- TRUMP
 

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
990
1,000
Trump atatushangaza kama awamu iliyopita..

Katika states 9 zilizobaki.. trump atashinda states 3 zenye electors wengi... na kumuachia bidden states 6 zisizo na electors wengi...

Trump anashindanga states za wazungu wenye uchungu na nchi yao... matokeo ya michigan, florida na ohio ndio yatasema ukweli kama trump anarudi ama anaandamana kaibiwa kura
2016 alitushangaza kwa kitu inaitwa Russian intrusion.

Mwaka huu tayari kuna kura zimeyeyuka zilizopigwa kwa njia ya Posta.


Inaonesha hata kwao hawaheshimu utawala wa sheria.

Shirika la Posta linaloongozwa na "mshkaji" wa Trump limegomea kutii amri ya mahakamu kuhusu baadhi ya kura za njia ya posta kuyeyuka
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom