Donald Trump: Afrika wameshindwa kujitawala na wanapaswa kutawaliwa tena kwa miaka mingine 100

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Kwa kifupi alichosem bwana Donald Trump ni kuwa Afrika tumeshindwa kujitawala na tunapaswa kutawaliwa tena kwa miaka mingine 100.

Bwana Trump,anaewania kuteuliwa kuwa mgombea wa uraisi wa Marekani kwa ticket ya chama cha Republican, amewaponda viongozi wa kiafrika kwa kuiba hela katika nchi zao na kuwekeza katika nchi za nje.

Pia amezishangaa nchi za kiafrika kwa kuagiza hata viberiti(matchstick) kutoka nchi za nje.

Je,unadhani bwana huyu yuko sahihi katika matamshi yake hayo?

Sema ndio au hapana.
 
Last edited:
Sasa kama watu wanang'ang'ana Halimashauri ya Kinondoni na ilala na wamezidiwa kwa number we huoni ni manyani hayo?
Trump kasema miaka100 mimi nasema miaka1000
Kama umeya umekuwa nongwa je ikiwa urais si yale yale ya burundi?
Zanzibar wameshindwa bado mijitu meusi haitaki na mfumo wa vyama vingi walikubali.
Tutawaliwe hata mpaka kihama maana hutu tu ngozi tweusi tuna laana.
 
Kawaulizeni waliotawaliwa kisha wakafanywa watumwa. Wakafungwa minyororo wakavushwa bahari na leo hii ni wahamiaji wanaohangaika kule hawatambuliki na huku hawapo. Kawaulizeni wanawake waliopoteza waume na watoto zao kwa ajili ya utumwa. Kawaulizeni wale waliofundishwa basic education ili wawezi kufanya kazi za utarishi na ulinzi wa wazungu. Kawaulizeni wale ambao........................................HALAFU NDIO MJE NA MAJIBU
 
Wamarekani walipigana na koloni lao la uingereza ingawa baadhi walikuwa waingereza wakashirikiana na wafaransa wakashinda. Tanzania tulipata uhuru kwenye meza ya UNO bila kumwaga damu je, tumetumiaje huu mwanya kujiendeleza badala yake, uchumi tuliojengewa na wakoloni umesambaratika kwa kwenda chini.

Tulijidai kuanzisha utawala wa vyama vingi lakini mioyoni mwetu bado utawala wa kiimra unashamiri ndo maana hata zile nchi zinazofanikiwa, huwa ni yale yale ya chukua chako mapema.
Trump anasema wanavyoficha pesa nje, sisi tunajua wazi watu wa vijisenti wana pesa kule lakini nani awaguse tunarudi pale juu.

Hatuagizi viberiti tu, angalia karatasi tunaagiza wakati wanaotuletea kila siku wanasomba magogo toka hapa kwetu. Hivi mfindi ingeshindwa kutengeneza madaftari ya east Africa bila kuweka mikoa inayovuna miti kama Kagera, Kili na Arusha? Kweli tununue njiti na toilet papers nje kweli??? Watoto washindwe kununua daftari wakati miti imejaa na inasafirishwa kinyemera uchina kweli??

Nasema ndiyo 100% and more.
 
Back
Top Bottom