Donald Ngoma na Amissi Tambwe wapata dili England

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
AMISSI-TAMBWE-001-768x707.jpg

HUENDA siku za mastraika Donald Ngoma na Amissi Tambwe zikaanza kuhesabika kwani Derby County FC ya England imeonyesha nia ya kuwasajili.

Derby County ya Ligi Daraja la Kwanza England, imetuma watu ambao sasa wapo katika harakati za kupata video za Ngoma na Tambwe za mechi za nyuma kwani tayari wameshaona uwezo wao katika michezo ya karibuni.
Klabu hiyo iliyoanzishwa Februari 5, 1884 na William Morley sasa inatumia Uwanja wa Pride Park unaochukua watazamaji 33,597, inamilikiwa na Mel Morris, kocha wake ni Darren Wassall.

Tayari Burnley na Middlesbrough zimeshapanda kucheza Ligi Kuu England msimu ujao, lakini Derby County iliyoshika nafasi ya tano, itacheza mtoano na Brighton & Hove Albion, Hull City na Sheffield Wednesday ili kupata timu moja itakapanda ligi kuu pia.

Habari za uhakika ni kwamba, klabu hiyo imetuma watu wake wawili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata video za Ngoma na Tambwe pia kufanya mazungumzo ya awali ya kufanikisha uhamisho wao.

“Watu wawili walifika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo na akina Ngoma na Tambwe, watu hao walipata taarifa za wachezaji hao wakiwa huko kwao.

“Walijiridhisha uwezo wa wachezaji hao kwa kuwafuatilia zaidi katika mechi zao ikiwemo dhidi ya Al Ahly waliyorudiana Misri, ndipo wakafika nchini kwa ajili ya mazungumzo zaidi na kutaka baadhi ya video za mechi zao walizozicheza,” kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Tambwe kuzungumzia hilo, alishangaa kisha akasema; “Mmepata wapi habari hizo? Akili zetu sasa zipo katika Kombe la Shirikisho Afrika.

“Ila ni kweli kwamba watu hao walifika hapa Dar na kututafuta lakini walifanya mazungumzo na meneja wangu ila wameshaondoka nchini wamerudi kwao".

“Kikubwa walichofuata ni video za mechi ambazo tumezicheza ili kuona mabao tuliyofunga na uwezo wetu wa kutengeneza mabao, nasikia wamepewa kwa ajili ya kwenda kuziangalia,” alisema Tambwe.

Kwa upande wake, Ngoma alisema: “Ningependa kupata ruhusa ya kocha kwanza ili kuzungumzia hilo.”

Alipotafutwa Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm alisema: “Hata aje nani, kwa sasa hivi siwezi kumruhusu mchezaji yeyote kuondoka kwenye timu yangu kwani tuna mechi za kimataifa mbele yetu.”

Ngoma ana mkataba wa mwaka mmoja na Yanga wakati Tambwe amebakiza miezi sita.

Kama mambo yakienda sawa, kuna uwezekano mkubwa wa Ngoma na Tambwe kucheza Ligi Kuu England msimu ujao, endapo Derby Country itafuzu.

Moja kati ya nyota waliochezea Derby Country ni kipa maarufu wa zamani wa Uingereza, Peter Shilton, 66, ambaye alicheza mechi 175 kati ya mwaka 1987-1992.

Source: Champion
 
Hivi mnadhani kila mchezaji anaweza kuuzwa tu ulaya kama Samatta?

Mzungu anaangalia umri sio kwanza. Sasa hao unaowataja wote ni vikongwe nadhani wana msimu mmoja tu kucheza katika kiwango chao hicho
 
wamechukua video zao mkuu . punguza povu.

Ngoma bado nafasi kuwa pro wa ukweli, ila akikubali mpira wake uishie yanga tuu atakuwa mbulumundu wa kutupa
 
Waandishi wa habari wa Tanzania ni miongoni mwa wadau wanaochangia mpira wetu kushuka kiwango
 
Back
Top Bottom