Dona kwa afya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dona kwa afya

Discussion in 'JF Doctor' started by Raia Fulani, May 28, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Hivi mbona watu wanakula sembe? Dona ambayo ina kiini lishe kinaondolewa. Watu wanakula makapi. Ugali mweupe. Ni ustaarabu au ulimbukeni? Jamii inatakiwa kuhamasishwa kula dona ili akili na mwili viwe na nguvu. Ndio maana Cigwiyemisi wakati flani akiwahi kuwaambia watu wake wahifadhi pumba ili wakati wa njaa wazitumie. Alijua. Kuna sehem hapa dar wanauza unga wa dona?
   
 2. K

  Konzogwe JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 441
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hakika!!
  Mziwanda huu naona ni ulimbukeni.Madhara ya sembe ni vidonda vya tumbo,kisukari,maradhi ya moyo nk.Hii ni kwa sababu fiber iliyo ktk kiini na pumba imeondolewa na zimebaki calories ambazo zinapokuwa in excess,mwili unazitunza ktk mfumo wa mafuta (fat) ambayo ni chanzo kikubwa cha kunenepeana (obesity),kisukari(IDDM),kufunga choo (constipation) nk.
  Kwa hiyo kama tutakula dona la mahindi,ngano,mtama,uwele,ulezi nk,tutaepuka maradhi mengi ajabu na tutaongeza life span zetu.Nawapa kitabu hiki ni msaada sana ktk matengenezo ya afya E.G.White, "The Ministry of Healing"
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Katika hili la dona itafika muda nitalivalia njuga kivitendo.
   
 4. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Du! Ndugu yangu utadhani ulikuwa kwenye mawazo yangu. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi jinsi watu wengi wasivyotumia akili zao kufikiri wale nini. Wengi wetu kinachotusukuma tule nini ni kile macho yanachokipenda, au kina test nzuri au kuiga jamii ya mastaa fulani wanakula nini, au kuangalia watu waliofanikiwa kiuchumi wanakula nini.

  Sembe ni kati ya matokeo ya mfumo huu mbovu, watu wanalipa gharama kubwa kutokana na kutofikiria wanakula nini. Baada ya kuamia mjini nimejaribu kufanya uchunguzi wa maisha ya watu katika kula na nimegundua uzembe mkubwa wa nini tunachokula. Nimeogapa sana kula hotelini, kwa mama ntilie kununua vyakula vya supermarket n.k. Inaonekana ni namna fulani hivi ya ushamba au ulimbukeni lakini ni tahadhari tu. Nimejiandaa sasa hivi kula matunda kwa wingi, na raw foods kwa ujumla (nakwepa sana vyakula vya kupika)

  Ukiangalia jinsi watu wanavyobugia mafuta, utashangaa sana, mtu anaamka asubuhi anakunywa chai ya maziwa kwa maandazi, saana nne kwa mayai ya kukaanga, mchana anakula chipsi mayai, jiuni anakula ndizi nyama rosti Mafuta ni lukuki hapo.

  Badala yake angekula nyakumla mchemsho na matunda kama parachichi hivi, na karanga kidogo angekuwa amepata mafuta fresh ndani ya mwili wake. Mafuta mengi tunayotumia yametengenezwa kisanii mno.


  Kuna mambo mengi sana ya kuangalia katika milo yetu. Leo hii unaweza kukutana na mtoto wa miaka kumi lakini kwenye kiti cha watu wawili kwenye daladala anakaa mwenyewe na kuoccupy nafasi yote kwa sababu ya unene, balaa kabisa.

  NAKUUNGA MKONO MAN KUANZA KULIFANYIA KAZI ILI KUTENGENEZA PESA.
   
 5. K

  Kitoto Akisa Member

  #5
  Jul 17, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tafadahli naomba ushauri wenu, mimi nina mdogo wangu, mwaka 2006 alifanyiwa operation kitaalamu inaita colostromy (sijui ni sawa) kwa sababu alikuwa na tatizo la abdominal obstraction, sasa mwaka huu ameonesha nia ya kutaka kufunga ramadhani, nimemzuia lakini anasisitiza, Je kuna madhara yoyote atakayo yapata kama akifunga ramadhani?
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280

  Kama daktari wake bado yupo,mwambie aende akamwambie ili apate vipimo vya mwili wake,kutokea hapo ndio tuanze kujadiliana.Ni vizuri kumwamini Mungu,lakini suala la utaalamu lipo pale pale.
   
 7. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mziwanda umeshapata mchumba, sasa ndugu yangu kama umepata mcumba wa hapa JF anayekaa kwenye keyboard muda wote, kweli ataweza kula dona zaidi ya kukwambia mwende samaki samaki Mlimani city mkapate soseji

  Kaka nenda Usukumani kama unataka kuanza kula dona,

  by the way ukianza kula dona unishtue tuanze wote. Niko serious
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Jul 19, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  nimekubali kuwa jf inaleta uteja usipokuwa makini. Atakachofanya huyo waif ni kutumia sim nitakayomnunulia kuaccess jf hata kama yuko jikoni, kibaya asiharibu mapishi
   
 9. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hiyo itakuwa powa na utakula dona fresh na malaria itakufilia mbali
   
 10. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  duh! ingekuwa simpo hivyo kula dona tu na magonjwa kwishnei ingekuwa balaa!!
   
 11. F

  FALSAFA JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2015
  Joined: Sep 10, 2014
  Messages: 296
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Napenda Sana Kula Dona. Dona Ndo Habari Ya Mjini.
   
 12. P

  Pishoni Member

  #12
  Feb 5, 2015
  Joined: Jan 31, 2013
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Samahani sana! ukija kwangu na tukakuandalia ugali jua ya kuwa ni wa dona, kwa hiyo kama wewe si mdau sema mapema ili tukakuchukulie chips hapo kwa bonge jirani ili uenjoy kula mafuta artificial! Toa taarifa mapema kabla hatujapika! sawa eeh!
   
 13. Slim5

  Slim5 JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2015
  Joined: Jan 7, 2014
  Messages: 15,699
  Likes Received: 12,773
  Trophy Points: 280
  Kuna dona na nyama choma safi kabisaaa pale coet cafeteria! Monday to Friday at lunch time, never miss the place!
   
 14. l

  ladyfocus JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2015
  Joined: Jan 30, 2013
  Messages: 796
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 80
  dona tamu sana ilimradi ulipatie mboga. Nimeshasahau how sembe look like.
   
 15. wabungenjaa

  wabungenjaa JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2015
  Joined: Feb 21, 2014
  Messages: 1,785
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  hakuna madhara ingekuwa ndani ya miezi 6 ndio ingemsumbua
   
 16. k

  kimbisi mbisi JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2015
  Joined: Jan 4, 2015
  Messages: 508
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna mama mmoja namfurahia sana, yeye ana hotel hapo morogoro,anauza vyakula vya asili tu, ikiwemo na huo ugali Wa dona, ulezi, mhogo n.k,pamoja na mboga samaki mchemsho, magimbi, viazi, mihogo ilo chemshwa, uji wa ulezi n.k,
  Kila nikienda lazima nile hapo,nasikia na dar kuna hotel kama hiyo jamaa mmoja aliniambia lkn nimesahau ni wapi.Na siku hizi jamani kuna baadhi ya maduka wanauza dona tembea muone hapa hapa dar.
   
 17. m

  munrash Member

  #17
  Feb 5, 2015
  Joined: Jan 16, 2015
  Messages: 72
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dona mbona ipo kila sehemu dar tatzo walaji ndo hamnaa!
  Mimi mwnywe nianza kutumia juz juzi tu baada ya kuhamasishwa na jirani yangu.......!!! Dona ndo mpango mzima;)
   
Loading...