Don Nalimison: Tamko rasmi la kugombea URAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2025

Masterplan

Senior Member
Dec 10, 2019
175
500
"Kwasasa Sina Mke natarajia FIRST LADY atakuwa raia wa Marekani ambaye nitamuoa ili kujenga uhusiano mwema wa Kimataifa. Nitaoa mwanamke anayejua maana ya mme na anayejua maana ya MKE wa Rais. Na Watanzania wote watafurahishwa na Mtazamo wangu."

Unataka upandikize adui nchini au Dhumuni lako Ni lipi sidhani kama atakuwa na uchungu na nchi yetu huyo
 

Masterplan

Senior Member
Dec 10, 2019
175
500
Unamuuliza mwehu alietoka kutumikia kifungo?
Ile Avatar ni yake au maana na kichwani
Screenshot_20201121-170739.jpg
 

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
3,553
2,000
Don Nalimison kwasasa hufundishi tena? Maana taarifa nilizonazo mimi kupitia kazi yangu ya kujenga taifa, ninajua kuwa wewe ulikuwa mwalimu wa somo la General study pale MKOLANI SECONDARY SCHOOL chini ya uongozi wa Mkuu wa shule ASENSIO MATHIAS. Na hata kabla haujakamatwa ulikuwa mwalimu, na kituo chako cha kazi kilikuwa ni hicho tajwa hapo juu.

Achilia mbali hao wachache uliofanikiwa kuwashika akili zao kupitia uzi wako huu, ningependa unieleweshe mimi pia, Kama hautojali.
 

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
3,553
2,000
Vip kuhusu uraia maana kwa sasa wewe ni raia wa Marekani
Huyo sio raia wa Marekani, Mara ya mwisho kabla haha kamatwa,alikuwa ni Mwalimu wa somo la General study kwenye shule moja hivi ya secondary iitwayo MKOLANI,Iliyopo mkoani Mwanza.Maisha yake ninayajua kuliko hata yeye mwenyewe.
Sio ndugu yangu,Ila kazi yangu imeniruhusu kumjua kuliko anavyofikiri.
 

fundi25

JF-Expert Member
Apr 16, 2013
10,199
2,000
Huyo sio raia wa Marekani, Mara ya mwisho kabla haha kamatwa,alikuwa ni Mwalimu wa somo la General study kwenye shule moja hivi ya secondary iitwayo MKOLANI,Iliyopo mkoani Mwanza.Maisha yake ninayajua kuliko hata yeye mwenyewe.
Sio ndugu yangu,Ila kazi yangu imeniruhusu kumjua kuliko anavyofikiri.
Kuna kipindi alisema hapa hapa JF kuwa anaenda zake Marekani kwenda kufanya siasa huko huko Marekani 😂
 

Mapank

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,356
2,000
TAMKO RASMI LA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MWAKA 2025.

Ndugu Watanzania na wote wanaopenda Mageuzi ya Fikira. Mimi DON NALIMISON NALIMI raia wa Tanzania Leo ijumaa ya Novemba 20, 2020 nachukua fursa hii kuwatangazia Watanzania kwa Mara ya pili kuwa mwaka 2025 nitagombea URAIS wa JAMHURI ya MUUNGANO wa Tanzania. Niliwahi kueleza dhamira yangu hii mwaka 2012 nikiwa Katibu wa BARAZA la Vijana wa CHADEMA Mkoa wa Tanga (BAVICHA) na pia niliwahi kueleza dhamira yangu hii mwaka 2013 nikiwa Katibu Mwenezi Taifa Kitengo Cha Vijana wa NCCR-Mageuzi kabla sijahamia CCM mwaka 2014 na kabla sijapendekeza kuanzisha Chama Cha siasa Cha Arena for Correcting Africa-ACA. Dhamira yangu iko palepale na haitafutika milele.

KUHUSU KAMA NIMEPOTEZA SIFA ZA KUWA RAIS
Kwa wasio jua Sheria wanadhani nimepoteza sifa za KUGOMBEA hii si kweli. Jina DEOGRATIUS NALIMI KISANDU ndilo lililofungwa lakini nimeapa kwa Wakili na Sasa Mimi ni DON NALIMISON. Hivyo jina DON NALIMISON NALIMI halijawahi kufungwa na ndio jina litakalotumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa URAIS wa mwaka 2025. Don Nalimison jina hili halijawahi kufungwa na hivyo lipo rasmi kwa Uchaguzi ujao.

NINI MAADHIMIO YANGU
DON NALIMISON nitajenga Nchi ambayo haikuwahi kutokea tangu Nchi ipate Uhuru. Kwanza tahakikisha Uingereza inatupatia Nchi yetu Uhuru wa Pili yaani UKOMBOZI wa Pili wa Taifa LETU kwa kuwa tangu tupate Uhuru hakuna MABADILIKO yoyote yaliyowahi kufanyika yaani mpaka leo bado tunaishi Kama watumwa, magerezani Watanzania wanauawa, wanateswa Kama wanyama. Vituo vya Polisi Watanzania Lockup wanasondekwa Kama utitiri bila kujali afya za Watanzania.

Watanzania wanazuiwa kudai Haki zao za msingi hata kufanya maandamano ya Amani ambayo yapo kwa mjibu wa Katiba ya Nchi na Sheria za Nchi. Watanzania wanaishi maisha magumu Sana tofauti na matamko yanayosemwa Nchi iko kwenye uchumi wa Kati. Ajira hakuna, Watumishi wa Umma wananyanyaswa, Mishahara haiongezeki wakati Nchi kila siku inakusanya Kodi na je Kodi hizo Zina enda wapi? Lazima tuhoji kwa mjibu wa Katiba ya Nchi ibara ya 18.

Watanzania wanabambikwa kesi na Mahakama zinawafunga Watanzania hata Kama wameshinda kesi kwa ushahidi thabiti. Siasa za Vyama zimeminywa na kuegemea upande mmoja tu.

Nitabadilisha Mfumo wote wa Jeshi la Polisi na Magereza kuanzia chini mpaka juu, nitabadili Mfumo wa elimu na Sheria ili kuendana na hadhi za Kimataifa. Nitawafungua Vijana kwa Wazee kifikira ili wajijenge Kiuchumi. Nitainua uchumi wa Nchi kwa wananchi 100%.

Pia nitatengeneza diplomasia nzuri na Mataifa mbalimbali ili kuweka wigo wa kupata Wafadhili wazuri wakuisaidia Nchi. Utalii wa ndani nitaujenga kwa hadhi ya Kimataifa.

KUHUSU MKE WA RAIS 2025
Kwasasa Sina Mke natarajia FIRST LADY atakuwa raia wa Marekani ambaye nitamuoa ili kujenga uhusiano mwema wa Kimataifa. Nitaoa mwanamke anayejua maana ya mme na anayejua maana ya MKE wa Rais. Na Watanzania wote watafurahishwa na Mtazamo wangu.

Pia nitawalipia mahali Vijana wote wanaotaka kuoa.

Natoa TAMKO hili kwa mjibu wa Katiba ya Nchi ibara ya 18 Kama sehemu yangu ya maoni. Sitegemei kupelekwa Detention kwa kuonesha Nia yangu maana kila mtu ana Haki ya Kikatiba kuwa Rais. Chama nitakacho gombea nitakitangaza 2023. Nasitegemei Polisi au Usalama wa Taifa kunikamata kwa nia yangu ya 2025.

Ninaweza kuwa Rais na Nina nguvu za kuwa Rais.

Mimi
DON NALIMISON NALIMI.
20 NOVEMBA 2020.
Kila la kheri Mkuu, unikumbuke kwenye Baraza la mawaziri. Hii safari ni yetu.
 

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
3,553
2,000
Kuna kipindi alisema hapa hapa JF kuwa anaenda zake Marekani kwenda kufanya siasa huko huko Marekani 😂
Mkuu niamini mimi kuwa asilimia100%, huyo alikuwa Mwalimu wakati anakamatwa. Hakuwa hata na nyumba alikuwa amepangua, gari hana, mke hana nguo anabadili Mara mbili kwa wiki. Kiufupi huyo jamaa ni masikini wa kutupwa, hata sasa baada ya kutoka gerezani mienendo yake yoote ninayo, mpaka anapoishi kwasasa ninapajua.Marekani hawezi kufika huyo Don Nalimison

NB;Mimi nashauri awekeze katika swala la kujenga maisha yake aachane kabisa na swala la siasa kwakua maisha yake yako uchi Sana, na bado hana nguvu yoyote ile ya kujihami hasa kiuchumi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom