Don Nalimison: Tamko rasmi la kugombea URAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2025

Dj DON NALIMISON

JF-Expert Member
Jun 26, 2020
785
1,000
TAMKO RASMI LA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MWAKA 2025.

Ndugu Watanzania na wote wanaopenda Mageuzi ya Fikira. Mimi DON NALIMISON NALIMI raia wa Tanzania Leo ijumaa ya Novemba 20, 2020 nachukua fursa hii kuwatangazia Watanzania kwa Mara ya pili kuwa mwaka 2025 nitagombea URAIS wa JAMHURI ya MUUNGANO wa Tanzania. Niliwahi kueleza dhamira yangu hii mwaka 2012 nikiwa Katibu wa BARAZA la Vijana wa CHADEMA Mkoa wa Tanga (BAVICHA) na pia niliwahi kueleza dhamira yangu hii mwaka 2013 nikiwa Katibu Mwenezi Taifa Kitengo Cha Vijana wa NCCR-Mageuzi kabla sijahamia CCM mwaka 2014 na kabla sijapendekeza kuanzisha Chama Cha siasa Cha Arena for Correcting Africa-ACA. Dhamira yangu iko palepale na haitafutika milele.

KUHUSU KAMA NIMEPOTEZA SIFA ZA KUWA RAIS
Kwa wasio jua Sheria wanadhani nimepoteza sifa za KUGOMBEA hii si kweli. Jina DEOGRATIUS NALIMI KISANDU ndilo lililofungwa lakini nimeapa kwa Wakili na Sasa Mimi ni DON NALIMISON. Hivyo jina DON NALIMISON NALIMI halijawahi kufungwa na ndio jina litakalotumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa URAIS wa mwaka 2025. Don Nalimison jina hili halijawahi kufungwa na hivyo lipo rasmi kwa Uchaguzi ujao.

NINI MAADHIMIO YANGU
DON NALIMISON nitajenga Nchi ambayo haikuwahi kutokea tangu Nchi ipate Uhuru. Kwanza tahakikisha Uingereza inatupatia Nchi yetu Uhuru wa Pili yaani UKOMBOZI wa Pili wa Taifa LETU kwa kuwa tangu tupate Uhuru hakuna MABADILIKO yoyote yaliyowahi kufanyika yaani mpaka leo bado tunaishi Kama watumwa, magerezani Watanzania wanauawa, wanateswa Kama wanyama. Vituo vya Polisi Watanzania Lockup wanasondekwa Kama utitiri bila kujali afya za Watanzania.

Watanzania wanazuiwa kudai Haki zao za msingi hata kufanya maandamano ya Amani ambayo yapo kwa mjibu wa Katiba ya Nchi na Sheria za Nchi. Watanzania wanaishi maisha magumu Sana tofauti na matamko yanayosemwa Nchi iko kwenye uchumi wa Kati. Ajira hakuna, Watumishi wa Umma wananyanyaswa, Mishahara haiongezeki wakati Nchi kila siku inakusanya Kodi na je Kodi hizo Zina enda wapi? Lazima tuhoji kwa mjibu wa Katiba ya Nchi ibara ya 18.

Watanzania wanabambikwa kesi na Mahakama zinawafunga Watanzania hata Kama wameshinda kesi kwa ushahidi thabiti. Siasa za Vyama zimeminywa na kuegemea upande mmoja tu.

Nitabadilisha Mfumo wote wa Jeshi la Polisi na Magereza kuanzia chini mpaka juu, nitabadili Mfumo wa elimu na Sheria ili kuendana na hadhi za Kimataifa. Nitawafungua Vijana kwa Wazee kifikira ili wajijenge Kiuchumi. Nitainua uchumi wa Nchi kwa wananchi 100%.

Pia nitatengeneza diplomasia nzuri na Mataifa mbalimbali ili kuweka wigo wa kupata Wafadhili wazuri wakuisaidia Nchi. Utalii wa ndani nitaujenga kwa hadhi ya Kimataifa.

KUHUSU MKE WA RAIS 2025
Kwasasa Sina Mke natarajia FIRST LADY atakuwa raia wa Marekani ambaye nitamuoa ili kujenga uhusiano mwema wa Kimataifa. Nitaoa mwanamke anayejua maana ya mme na anayejua maana ya MKE wa Rais. Na Watanzania wote watafurahishwa na Mtazamo wangu.

Pia nitawalipia mahali Vijana wote wanaotaka kuoa.

Natoa TAMKO hili kwa mjibu wa Katiba ya Nchi ibara ya 18 Kama sehemu yangu ya maoni. Sitegemei kupelekwa Detention kwa kuonesha Nia yangu maana kila mtu ana Haki ya Kikatiba kuwa Rais. Chama nitakacho gombea nitakitangaza 2023. Nasitegemei Polisi au Usalama wa Taifa kunikamata kwa nia yangu ya 2025.

Ninaweza kuwa Rais na Nina nguvu za kuwa Rais.

Mimi
DON NALIMISON NALIMI.
20 NOVEMBA 2020.
 

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
5,674
2,000
Tutafsirie mkuu kwa kingereza nashauri utuandikie wewe mwenyewe

yote uliyoyaandika hapo hivyo uwe na nakala mbili incase hata first lady huko alipo aweze

kumsoma mume wake na kumuelewa ila kwa nakala hii imeegemea upande mmoja kwa lugha.
 

Akui

JF-Expert Member
Dec 3, 2016
435
500
Kabla ya chai ya saa nne utakuwa umeshinda huna mpinzani hongera sana kwa uamuzi ambao wananchi walisubiria kwa hamu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom