Domo Kaya: Hukumu ni Kifo

Kwa hiyo kwa akili yako fupi unajua Mimi ni Kudo?
Sasa kama sio kudo ulikua na sababu gani kutuharibia hadithi yetu tunayoletewa bure? Ungepoteza nini ungemfuata private?

Au nyie ndio wale nzi wa chooni mnatuaga kwenye chakula kitamu.?

Pumbavu kabisa wewe
 
Unapenda sana bure wewe sio?usijali,nitakununulia!
 
migomba. Bila kujishauri zaidi, alikanyaga juu ya ukuta na kujirusha upande wa nje wa ile kambi na kuangukia shambani, kisha akaanza kukimbia kuelekea nje ya lile shamba huku masikio yake yakisikia miungurumo ya ndege zikitua uwanjani..

“Kumbe wapuuzi walinifunga hapa Banana!” Aliwaza huku akizidi kujiweka mbali na ile kambi ya wanausalama wa kupambana na ugaidi. Alikimbia huku akiapa kuwaadabisha wote waliokuwa wakitaka kumzamisha gerezani, akapanga kuliongezea joto jiji la Dar es laam.

**********

4:
Majira ya saa moja na nusu jioni yaliwakuta Bob Rando na Kisu wakiwa mita chache kutoka ilipokuwa nyumba ya Zuki Gadu. Kama kawaida yao, wao mara nyingi midomo yao ilikuwa haitulii, walizodoa na kuzodoana hili na lile, walikuwa ni marafiki walioshibina sana.

“Huyu jamaa anakimbiaje hapa mjini na kuacha nyumba kubwa kama hii!” Kisu alisema huku akiutazama ukuta mrefu wa nyumba ya Zuki Gadu.

“Hii ni nyumba ndogo kati ya nyumba nyingi alizokuwa akiishi huyu jamaa, lakini aliipenda zaidi hii nyumba.” Bob alimjibu huku akimpa ishara ya kusimama.

“Unatanguliza pua mbele au unahisi tunafunguo za hii nyumba?” Bob alimzodoa kwa swali swahiba wake.

“Uliambiwa mimi ni mnatabiri hadi nijue huna funguo za geti!” Kisu alijibu.

“Basi tuliza kwato, hapa tunaingia ndani kwa kuruka ukuta.” Bob alimwambia huku akichepuka na kuiacha njia na kuufuata ukuta.

“Ohoo! Kwa hiyo unajifanya mzungu wa kunigeuza mimi nyani?” Kisu aliuliza huku nae akifuata.

“Kama hutaki kuruka, baki hapo njiani wahuni wakupigie mluzi, utongozwe.” Bob alizodoa kwa mara nyingine.

“Mavi yako!” Kisu alimjibu kwa tusi jepesi.

“Kwa hiyo anatangulia nani kuruka?” Bob aliuliza huku akiwa amejiweka hatua tatu mbali na ukuta.

“Ladies first! Anza wewe.” Kisu alimjibu, Bob akageuza shingo na kumtizama kisha akasonya.

“Heh…!” Kisu alibaki akishangaa baada ya kumshuhudia mwenzake akinesa na kuudandia ukuta mithili ya paka anaewinda mijusi, alishika kiuno huku akiona uvivu kufanya alichokifanya mwenzake.

“Huyu bwege anahisi nina nyonga za chui. Mhmh!” Kisu alijisemea peke yake huku akigeuka na kurejea njiani kisha akakimbia kidogo hadi alipofika getini, aliona geti likiwa limefungwa kwa ndani na hakukuwa na komeo upande wa nje wala hakukuwa na sehemu iliyoonesha kulikuwa na uwezakano wa geti kufungwa siku nyingi.

“Mh!” Aliguna huku akigeuza shingo yake huku na huko ili kupima usalama wa mazingira yale. Nafsi yake ilimwambia hakukuwa na na jambo la kawaida, kulikuwa na kitu kilichokuwa kimetokea muda mfupi uliopita, alihisi hivyo baada ya kuliona geti lilifunguliwa na kuegeshwa.

“Hapa kuna kiumbe aliingia na kutoka, siyo rahisi hili geti kuachwa bila kufungwa na wakati mwenye nyumba hayupo.” Aliwaza huku akisukuma geti na kuingia ndani.

“Waoh!” Alijikuta akisimama na kuzubaa huku ile tahadhari yake ya awali ikipotea, mbele yake licha ya kuwa nyumba ilikuwa giza lakini alifanikiwa kuona idadi kubwa ya magari yakiwa yamepangana, upande mwingine aliona karakana ndogo iliyokuwa na magari mawili na pikipiki zaidi ya tano.

“Yaani ni kama nipo uwanja wa magari, huyu jamaa ni hatari sana.” Aliwaza huku akiwa hajachukua tahadhari yoyote, mawazo yake yote aliyaelekeza kushangaa idadi kubwa ya magari iliyokuwa nyumbani kwa Zuki Gadu, akajipa na muda wa kupiga hesabu za gharama iliyotumika kuyanunua magari yote pamoja na pikipiki alizoziona.

“Kwa hesabu za gizani naona ni kama milioni mia saba hivi, hapo nimeotea gharama ya gari la aina moja, lakini kama ningeliona ni gari za aina gani pengine itafika bili..” Alisita kumalizia alichokiwaza baada ya kuhisi kulikuwa na mtu hatua mbili nyuma yake, haraka aligeuka lakini alikutana na konde zito lililotua usoni na kumpeleka chini bila kupenda.

“Aiyii!” Kisu alibweka kwa mshituko, hakuwa ametarajia tukio kama lile.

“Tulia hapohapo kunguni we!” Mtu aliyempiga aliunguruma kwa sauti nzito huku akiwa amemwelekeza bastola.
Yule mtu aliyekuwa amevaa nguo nyeusi alipiga vidole vyake mara mbili, punde watu wawili walijitokeza kutoka nyuma ya kibanda cha mlinzi kilichokuwa karibu na geti na wao walikuwa na bastola mikononi mwao.

“Nimekuwaje Juma Kilaza namna hii?” Kisu alijilaumu huku akijifananisha na mpiga gitaa mashuhuri aliyekuwa akitumia gitaa la kamba miaka ya nyuma, kisha kipaji chake kikawavutia baadhi ya watu ambao wakampa nafasi ya kwenda nchini Ujerumani, huko akasahau kilichompeleka baada ya kuingizwa kwenye moja ya kumbi kubwa kwa ajili ya kutumbuiza, akashindwa hata kupiga gitaa lenyewe, waliompeleka wakamrejesha nchini na kuanzia hapo Kilaza ikageuka neno la kejeli kwa jamii nzima ya watu wa Tanzania.

“Simama taratibu na ukiwa umeweka mikono yako juu.” Jamaa mmoja alimwambia huku akifyatua kilinda usalama kwenye bastola yake kumaanisha, hakuwa na la ziada endapo maagizo yake yasingelitekelezeka.

“Twende aliko mjinga mwenzako.” Jamaa mwingine alimwambia huku akimsukuma kuelekea upande wa nyuma wa nyumba.

“Dah, nasukumwa kama Kilaza kweli.” Kisu aliwaza huku akiendelea kupiga hatua zake taratibu kama alivyoelekezwa.

Nyuma ya nyumba waliwakuta watu wengine wawili wakiwa wamempigisha magoti bwana Bob Rando. Kisu aliongozwa kupiga magoti karibu na mwenzake kisha wale watu watano wakasimama kwa kuwazunguka huku wakiwa makini na silaha zao mikononi.

“Tunaomba kufahamu mlichokuwa mmefuata hapa ndani.” Mmoja wa wale mabwana aliuliza, lakini hakupata majibu aliyoyatarajia.

“Mkiulizwa mnatakiwa kujibu haraka.” Jamaa mmoja alisema huku akiwashushia makofi juu a vichwa vyao.

“Wakati mwingine msipojibu, mmoja atatangulia akhera.” Aliwapiga mkwara.

“Mmefuata nini hapa? Kwa nini mmoja aruke ukuta na mwingine apite getini?” Yule aliyeuliza mwanzo, aliwauliza tena kwa mara nyingine.

Bob Rando aligeuza shingo yake na kumtazama Kisu, akaishia kutikisa kichwa chake kwa sababu hakudhani kutoonekana kwa Kisu ilikuwa ni kwa sababu alizunguka getini badala ya kukwea ukuta kama alivyokuwa amefanya yeye. Kisu alitamani kumshushia neno zito lakini alisita baada ya kuona mazingira hayakuruhusu, alitamani kufanya hivyo kwa sababu aliamini pengine walingelipita getini pamoja wasingeingia mtegoni kirahisi namna ile, lakini wakati anamlaumu mwenzake, alisahau hata yeye alikuwa ni mzembe pengine kuliko Bob maana yeye ndiye wa kwanza kugundua sintofahamu baada ya kulikuta geti likiwa wazi, lakini aliingia bila tahadhari na kuanza kushangaa idadi kubwa ya magari yalijaza uwanja wa nyumba ya Zuki Gadu p.a.k Miguu ya kuku kama walivyopenda kumuita wao, mtu ambae alikuwa idadi ya vidole vinne kwenye mguu wake, mrefu na mwembamba kiasi, mtu ambae atembeapo hakuwa akitoa vishindo na hapo ndipo wenzake wakampachika Miguu ya kuku.

“Tunaingia hatua nyingine, wafungeni.” Jamaa aliwaagiza wenzake.

Wale waliokuwa wamesimama nyuma wakagawana majukumu, mmoja alienda kumfunga Bob na mwingine alienda kwa Kisu. Kioja kikaibuka, Kisu alianza kutetemeka huku akilia mithili ya mtu aliyezidiwa na baridi na kugongesha meno yake, alietemeka huku akijikunja na kuanguka chini kama mgonjwa wa kifafa, wale jamaa walisogea pembeni ili kukwepa mateke yaliyokuwa yakirushwa na bwana Kisu aliyeingiwa na ugonjwa wa ajabu.

“Huyu atatuzingua, malizaneni nae.” Alisema yule aliyekuwa akihangaika kuikutanisha mikono ya Bob ili aifunge, alikuwa akikutana na upinzani kutoka kwa Bob ambae alikuwa akitumia nguvu kidogo ili mikono yake isikutanishwe.

“Fasta basi!” Kiongozi wao aliwaharakisha wenzake ili washumshugulikie Kisu ambae bado alikuwa anatetemeka na kurusha miguu yake hovyo huku akilia kama paka aliyetoswa na mwenza wake.

Wakati mmoja akifyatua kilinda usalama kwenye bastola yake, mara jambo lingine likawazubaisha; mlio wa risasi ukasikaka nje ya ukuta wa nyumba na haukuwa mlio tu, na sauti za kilio na hamaniko vilisikika kwa wakati mmoja.

“Ooh shiit!” Mmoja wao akaropoka huku akitaka kupiga hatua kuondoka lile eneo, hakufanikiwa, miguu yake ikadakwa na mikono imara ya Kisu, kisha akapigishwa mweleka safi na kuanguka nchini mithili ya fuko la viatu vya bondo na kwa namna ya ajabu kabisa, Kisu akamtandika ngumi safi kwenye via vyake vya uzazi na kumfanya yule bwana abweke kama mbwa aliyefumaniwa jikoni, shingo yake ikadakwa na kuzungushwa kwa kasi na kutoa mlio wa mvunjiko wa kijiti kikavu, kisha Kisu akasimama wima kwa mbwembwe kama mwanamitindo Jane Jackson.

Risasi iliposikika Bob nae hakutaka kuzembea, alifyatuka kama mshale na kwenda kitua kichwa chake tumboni kwa kiongozi wa wale mabwana, kisha akageuka kwa kasi na kumtandika teke zito mtu aliyekuwa nyuma yake na wote waliokutana na mapigo yake walienda chini kama viroba vya sukari bingwa, alipogeuka kwa mwenzake alikuta akiwa ameshasimama na anakabiliana na mtu mwingine, nae akamfuata mwingine aliyekuwa bado kasimama. Akapiga hatua moja kumfuata, akaona yule jamaa akiwa ananyanyua mkono wake wwnye bastola, haraka akainama na kuichomoa bastola yake kiunoni na kumcharaza risasi mbili kisha akageukana na kumchagua aliyekuwa akipambana na Kisu, akamtandika risasi mgongoni na wakati alipokuwa akiwakumbuka wale wawili aliowaangusha, risasi mbili zikavuma kutokea gizani na kuwachabanga wale mabwana waliokuwa wakijivuta kusimama. Bob na Kisu wakabaki wakiwa wamesimama wima kama wamechezeshwa mchezo wa ganda ganduka
 
Risasi iliposikika Bob nae hakutaka kuzembea, alifyatuka kama mshale na kwenda kitua kichwa chake tumboni kwa kiongozi wa wale mabwana, kisha akageuka kwa kasi na kumtandika teke zito mtu aliyekuwa nyuma yake na wote waliokutana na mapigo yake walienda chini kama viroba vya sukari bingwa, alipogeuka kwa mwenzake alikuta akiwa ameshasimama na anakabiliana na mtu mwingine, nae akamfuata mwingine aliyekuwa bado kasimama. Akapiga hatua moja kumfuata, akaona yule jamaa akiwa ananyanyua mkono wake wwnye bastola, haraka akainama na kuichomoa bastola yake kiunoni na kumcharaza risasi mbili kisha akageukana na kumchagua aliyekuwa akipambana na Kisu, akamtandika risasi mgongoni na wakati alipokuwa akiwakumbuka wale wawili aliowaangusha, risasi mbili zikavuma kutokea gizani na kuwachabanga wale mabwana waliokuwa wakijivuta kusimama. Bob na Kisu wakabaki wakiwa wamesimama wima kama wamechezeshwa mchezo wa ganda ganduka.

Mbele yao walikuwa wakitizama kiumbe mrefu akijongea taratibu kuwafuata, mwanzo walikuwa na hofu lakini kadri mtu yule alivyokuwa akizidi kuwasogelea, walijikuta wakitabasamu kwa pamoja bila kuambiana.

“Miguu ya kuku!” Bob alijikuta akiropoka bila kupenda huku akianza kupiga hatua kumfuata, hakufanikiwa, akajikuta akienda chini baada ya kulambwa mtama safi na rafiki yake Kisu, kisha akamshuhudia Kisu akipiga hatua za furaha na kwenda kujaa mwilini mwa Zuki Gadu p.a.k Miguu ya kuku.

“Eti braza, Bob alitaka awe wa kwanza kukugusa, inawezekana kweli kitu hicho kufanyika kabla ya mimi mdogo wa mwisho kukifanya?” Kisu aliuliza huku akicheka na Zuki nae alicheka kwa furaha.

“Wacha ujinga!” Bob alisema huku akimtandika Kisu kofi la kichwa na kumvuta pembeni kisha nae akaenda kumkumbatia rafiki yake wa siku zote, rafiki kama ndugu, bwana Zuki Gadu.

Uwanja uliokuwa na vita ukageuka uwanja wa furaha kwa dakika tatu, kisha wakarejea kumalizia kilichokuwa kimewakutanisha pale kwa dharura japo hawakuwa wamepanga kukutana pale na hawakuwa na taarifa ya ujio wa Zuki Gadu.

“Nilivyosikia risasi nje nikajua aina ya upigaji wako.” Bob alisema huku akiinama na kumkagua mmoja wa wale watu waliokuwa wamewateka.

“Nilifika hapa juzi, lakini huwezi amini waliniteka siku hiyohiyo hadi leo nilivyofanikiwa kuwatoroka, nafika hapa nakuta wameweka kundi huko nje, nimewachapa na kuingia huku na kuwakuta na nyie mkiwa kwenye songombingo.” Zuki aliwambia.

“Nadhani hapa siyo sehemu salama, tundoke!.” Bob aliwashauri wenzake huku akiinuka na baadhi ya vitu akivyovikuta kwenye mfuko wa mtu aliyekuwa akimpekua.

“Upo sahihi, lakini nina kesi na huyu bwege.” Kisu alisema huku akimtandika teke zito mtu mmoja aliyekuwa amelala chini bila uhai.

“Heh!” Zuki alishangaa.

“Yaani huyu fala kanitandika kofi la kichwa nikahisi nimebeba mzani wa kilo saba.” Alisema huku akimtandika teke lingine na kumtemea mate.

“Achana huyo kichaa, fungua boksi la Luku yako na uchukue utakachokiona.” Bob alimwambia Zuki ambae alifanya haraka kama alivyoelekezwa.

“Wewe bwege uliigiza kuugua kifafa hadi nikahisi unaumwa kweli.” Bob alimgeukia Kisu na kumtania.

“Bado nina kesi na wewe, kwa nini uliamua kutumia bastola wakati nilikuwa nataka kupiga busu huyu bwege.” Kisu alisema huku akimnyooshea kidole aliyekuwa kapigwa risasi na Bob.

“Nilimtandika ili siku nyingine asiwe anatupiga mikwara mbuzi wakati hata sisi tunaweza kumpiga mikwara dume.” Bob alijibu huku akimgeukia Zuki aliyekuwa akihangaika kuopoa kadi ndogo iliyokuwa kwenye boksi.

“Tukupe kijiti?” Kisu alimuuliza.

“Ishatoka” Zuki alijibu na kulifunga boksi kisha akawageukia wenzake.

“Hapa nitarejea sakata hili likiisha.” Zuki aliwaambia huku akianza kupiga hatua kuelekea upande aliokuwa ametokea.

“Tunaenda kuruka ukuta kwa mara nyingine, jitoe ufahamu unyonywe damu huko getini.” Bob alimpiga mkwara swahiba wake Kisu.

Wote walifanikiwa kuuparamia ukuta na kuangukia nje bila kupata madhara, walikuwa ni wajuvi kwenye nyakati kama hizo.

“Mlikuja na usafiri gani?” Zuki aliwauliza.

“Gari lipo barabarani kwa Ndevu.” Kisu alijibu.

“Liacheni huko tutamwagiza mtu akalichukue, tutumie hili la hawa wajinga.” Aliwambia huku akifungua mlango wa gari iliyokuwa imesimama upande wa nyuma wa nyumba yake, wenzake nao walipanda na safari ya kuelekea kwenye moja ya nyumba zao salama ilianza.

*******

Saa nne usiku iliwakuta wakiwa wamekaa kwa kuizunguka meza ndani ya nyumba yao ambayo wote waliitumia pale ilipobidi. Zuki alikuwa ameshaoga na kujipa huduma ya kwanza kisha alikula, Bob na Kisu walibadilisha mavazi na kula kisha wakaenda kukaa kwa lengo la kujadili kilichokuwa kikiendelea.

“Msishangae kwa nini niliamua kurejea hapa nchini, nimefanya hivyo kwa kuwa siamini kama Dodi anaweza kufanya hicho kitendo, pia nimerejea ili kuhakikisha biashara zake haziyumbi kwa kipindi chote atakachokuwa mahabusu.” Zuki alianzisha mjadala kwa kuwapa sababu ya kwanini aliamua kurejea nchini.

“Hata sisi tangu tuliposikia habari za kukamatwa kwake tuliamua kulivalia njuga, lakini kwenye kila njia tuliyotaka kupita ili kumsaidia, tulikutana na changamoto nyingi na hapo tukaamua kutumia mbinu nyingine, tuligundua kuna nguvu kubwa sana ilikuwa inatumika kumweka gerezani.” Bob alimpasha.

“Tangu awali nilihisi Luna nguvu ya mtu itakuwa nyuma yake, lakini kwanza tuanze kujiuliza ni kwa nini itumike nguvu kubwa namna hiyo?” Zuki aliweka hoja mezani.

“Kibaya zaidi wanaotumika zaidi ni watu wa serikali na kila sehemu ni wao wanaotaka kukwamisha jitihada za kumsaidia, namna kesi inavyoendeshwa unajua kabisa nguvu kubwa inatumika.” Kisu alichangia maoni yake.

“Kwa hiyo tunajiridhisha kwamba walioko nyuma ya haya yote ni serikali, lakini tujiulize, serikali nzima inaweza kupambana na mtu mmoja? Jibu ni hapana, lakini yawezekana yupo mtu mmoja au kikundi cha watu ambao wanatumia pesa zao ama madaraka kumwangamiza Dodi.” Zuki alisema.

“Hapo inabidi tutoke na maswali mawili, nani anafanya haya na kwa nini?” Kisu aliuliza maswali waliojiuliza wenzake.

“Ili tuanze kuyajibu yote haya inatulazimu kuanza na kisa chenyewe kilichosababisha yote haya.” Bob alisema.

“Kisa chenyewe ni mwanamke anaitwa Linatha Msuya ambae alikuwa ni mke wa Dodi Danga, lakini alikuwa pia na mahusiano na mwanaume mwingine aliyeitwa Ngurimi Mwangwa. Sasa tuanzie kwa huyo mwizi wa penzi la Dodi.” Kisu alisema huku akivuta kalamu na karatasi vilivyokuwa mezani na kuandika vitu fulani kisha akawatizama wenzake.

“Kuanzia hapa nitakuwa mkimya kwa sababu haya yalitokea nikiwa mbali, nategemea mengi kutoka kwenu.” Zuki aliwaambia.

Bob aliinuka na kuelekea chumbani kwake, sekunde chache alirejea akiwa amebeba kompyuta mpakato. Aliitua mezani na kuanza kucheza na batani zake kwa kasi kubwa. Bob alikuwa ni mtaalamu sana wa mambo ya kompyuta, hakuna kitu ambacho kingeliwezekana kutumika kwa kompyuta kingelimshinda. Kwenye kompyuta iliyokuwa mbele yake, alikuwa anatafuta wasifu na tawasifu ya Ngurimi Mwangwa.

“Huyu mtu anaonekana alikuwa ni Meneja wa benki ya Starehe, Starehe Bank.” Bob aliwaambia wenzake.

“Kuna kingine kuhusu yeye?” Zuki aliuliza.

“Mengini ni wasifu wake na tawasifu ila la muhimu nilililoliona ni hiyo kazi aliyokuwa akiifanya.” Bob alijibu.

“Alikufa akiwa bado anahudumu kwenye hiyo benki?” Kisu alihoji.

“Hapana! Alikuwa amesimamishwa wiki moja kabla ya kifo chake.”

“Sababu ya kusimamishwa kwake je!”

“Kuna gazeti liliripoti kwamba, alikuwa anatuhumiwa kwa utovu wa nidhamu lakini haukusemwa ni utovu gani. Cha kuvutia zaidi kwenye maelezo ya hili gazeti ni kwamba alikuwa anajiandaa kupinga adhabu yake mahakamani na kudai fidia ya kuchafuliwa.”

“Tunaomba itafute wamiliki wa hiyo benki kwanza.”

Bob aliparaza hapa na pale kisha akarejea na majibu..

“Hii ni benki iliyoanzishwa na wamiliki wa kampuni moja ya mafuta hapa nchini, wamiliki wa kampuni hiyo ni familia ya bwana Koba Kinyozi.”

“Koba Kinyozi?”

“Ndiyo. Koba Kinyozi ambae ni waziri wa Nishati na Madini pamoja na wanae wawili ambao mmoja yupo Afrika kusini na mwingine ndiye msimamizi mkuu wa kampuni hapa nchini.”

Wote walionekana kuzama mawazoni kutafakari taarifa walizokutana nazo.

“Tusifikirie sana kuhusu wamiliki wa hiyo benki, turejee kwa Linatha Msuya mke wa Dod.”

Bob akarejea tena kwenye kompyuta yake na dakika chache akainua kichwa chake na kuwatizama wenzake.

“Nae alikuwa ni mfanyakazi wa benki ya Starehe, alikuwa ndiye msoma miamala yote ya benki hiyo, tofauti na mwenzake, yeye hadi kifo kinamkuta bado alikuwa ni mfanyakazi halali wa hiyo benki.”

“Hilo ni tatizo na tatizo lenyewe linaanzia hapohapo benki” Kisu alisema.

“Lakini kwa nini Dodi? Kwa nini liishie kwa mtu ambae hakuwa mfanyakazi wa hiyo benki na hata wakati namkabidhi biashara hatukuwa wateja wa hiyo benki.” Zuki alionesha mashaka yake.

“Dodi kaangushiwa jumba bovu ili kuficha jambo kubwa nyuma ya vifo hivyo.” Bob alisema.

“Upo sahihi sana. Dodi ni mbuzi wa kafara tu.” Kisu akasema kisha ukapita ukimya mfupi.

“Mlisema mlifanikiwa kuingia gerezani na kuonana na Dodi, kuna lolote aliwaambia?” Zuki aliwauliza.

“Hatukuongea sana, aliishia kutuelekeza twende nyumbani kwako na kuchukua ile kadi.” Kisu alijibu.

Zuki aliinuka na kuelekea chumbani kwake, aliporejea alikuwa na ile kadi ya kuhifadhi kumbukumbu aliyoitoa kwenye boksi la kisoma umeme. Alimkabidhi Bob ambae bila kusubiri akafungua simu yake na kuiweka, kisha akauiwasha simu na kuingunisha na kompyuta yake.

Kwenye ile kadi kulikuwa na faili moja la Video, akalifungua na kucheza ile video na kuwaita wenzake waitazame, walimtazama Dodi Danga.
 
kudo yote sh ngapi
 
Back
Top Bottom