Dome okochi budohi a kenyan taa executive and tanu member

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,853
30,195
20131201_100944.jpg


Wanaukumbi,


Kilichonifanya nimrudishe shujaa huyu wa uhuru wa Tanganyika ambae
wengi hawamjui ni kuwa nimekuta picha yake katika nyaraka zangu.

Hii picha nimekuwanayo kwa zaidi ya miaka 40.

Nimeona itapendeza sana kama hii picha nitaiweka hapa jamvini ili JF
wafurahi.

Kwa haraka haraka nimeokota hapa na pale kutoka kitabu changu mle
ambapo nimemtaja Dome Budohi na kuweka hapa jamvini.

Naamini haya yatatufikirisha lau kama kiduchu kuhusu yale ambayo
hayajulikani katika historia ya nchi yetu.

20131201_100944.jpg



20131205_065337.jpg
 

Attachments

  • DOME OKOCHI BUDOHI.docx
    14.4 KB · Views: 109
Mohamed Said.

Tunashukuru sana kwa kutujuza mengi kuhusu historia yetu huyu Dome Okochi Buduhi, ilikuaje akaingia kwenye siasa za Tanganyika.

Ni kweli alishawahi kuwa kiongozi wa TAA na muasisi wa TANU.



CC: THE BIG SHOW gombesugu FaizaFoxy wabara kahtaan faby

Shariff Ritz,

Dome Budohi alikuwa mmoja wa viongozi wa TAA lakini hakuwa kuwa
kiongozi katika TANU.

Nakuwekea hapa kitu kidogo angalia mwenyewe:

20131205_065337.jpg


Shariff,
Nadhani umeona hapo sahihi ya Julius Nyerere, Abdu Sykes Dome Wafula
Budohi,John Rupia, Ally Sykes, Waziri Dossa Aziz.


Waandishi wa historia ya TANU kutoka CCM walipotaka kuletewa nyaraka kama
hizi muhimu wakaziogopa.

Nyerere Foundation nikawaandikia kuwaambia kuwa nina nyaraka muhimu za Nyerere
hadi leo hawajanijibu.
 
Asante sana kwa kutujuza kuhusu mkenya huyu aliyekuwa mwanaTAA na ambaye alishiriki kutafuta uhuru wa Tanganyika.
 
Shariff Ritz,

Dome Budohi alikuwa mmoja wa viongozi wa TAA lakini hakuwa kuwa
kiongozi katika TANU.

Nakuwekea hapa kitu kidogo angalia mwenyewe:

20131205_065337.jpg


Shariff,
Nadhani umeona hapo sahihi ya Julius Nyerere, Abdu Sykes Dome Wafula
Budohi,John Rupia, Ally Sykes, Waziri Dossa Aziz.


Waandishi wa historia ya TANU kutoka CCM walipotaka kuletewa nyaraka kama
hizi muhimu wakaziogopa.

Nyerere Foundation nikawaandikia kuwaambia kuwa nina nyaraka muhimu za Nyerere
hadi leo hawajanijibu.

Mohamed Said

Hizi data unazipata wapi sidhani hata Makoa Makuu ya CCM wanazo hizi data au waandishi wa habari kina Mzee Mwanakijiji na wenzake hawajuhi waanzie wapi kuandika historia ya TAA na TANU.

Dome Okochi Budohi alipewa kadi nambari ngapi?

Na bado yupo hai?
 
Last edited by a moderator:
ingekuwa haioneshi jina na wadhifa wa Nyerereingekua hoja.

Mwanakijiji,
Kwani lazima useme kitu?

Nani kakwambia kuwa Nyerere ni tatizo kwangu katika kuiandika historia ya wazee wangu?
Nyerere siku zote nimemueleza kama alivyokuwa.

Nimesema na narudia tena kusema.
Nyerere hakuasisi TANU.

TANU ni mtoto wa Abdulwahid Sykes na moja ya nyaraka za marehemu Abdu ndiyo hii.
 
Mohamed Said

Hizi data unazipata wapi sidhani hata Makoa Makuu ya CCM wanazo hizi data au waandishi wa habari kina Mzee Mwanakijiji na wenzake hawajuhi waanzie wapi kuandika historia ya TAA na TANU.

Dome Okochi Budohi alipewa kadi na ngapi?

Na bado yupo hai?


Shariff Ritz,
Budohi kadi yake ya TANU na. 5.

Budohi amefariki dunia mjini Nairobi.

Huyo Mwanakijiji hana alijualo katika haya.
Hao CCM ndiyo wanatia hata huruma.

Wao CCM wanaogopa habari za Abdu Sykes na harakati za ukombozi wa Tanganyika
zisijulikane.

Wanataka TANU ianze na Nyerere 1954.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said

Ulibahatika kukutana au kuongea na Dome Okochi Buduhi?

Shariff,
Kwa mara ya kwanza nilikwenda kumuona nyumbani kwake Nairobi,
Ruiru 1972 alinialika nikaone All Africa Trade Fair.

Nilikaa kwake kwa juma moja.
Kisha nilikwenda tena kumtembelea 1974 safari hii akiishi Ngei Estate.

Nilipokea mengi sana kutoka kwake kuhusu harakati za TAA/TANU na jinsi
alivyokamatwa kwa tuhuma za kuwa Mau Mau.

Yapo mengi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom