Dola za Kimarekani zamwingiza pabaya kwa pupa ya utajiri

kisute

Member
Oct 6, 2010
54
3
:fear:Mwanzoni mwa wiki hii, jamaa yetu mmoja ambaye ni mfanya biashara hapa Nzega kwa jina Kapuni .Watoto wa mjini walimwingiza mjini kwa kumuuzia dola za kimarekani zenye thamani ya Tshs Milioni thelathini. alifungua bahasha iliyokuwa na noti zenye thamani ya dola mia kila moja. Alizihesabu na kuridhika. Vijana hao walizirudisha ndani ya bahasha na kufunga kwa stapple machine. Mfanyabiashara huyo alikimbia benki kuchua (kudraw) noti za kitanzania ili wabadilishane. Wakati anarudi aliwakuta wakimsubiri pale pale dukani. walimkabidhi bahasha yake yenye dola, nae akawapa noti za Kitanzania. Vijana hao walitoweka na kwenda zao. Jamaa aliamua kuifungua bahasha yake ndipo alipojikuta kaibiwa, noti zilizokuwemo bahashani zilikuwa ni za dola za hamsini hamsini sio dola mia mia tena. Jamaa alibaki kachanganyikiwa hajui nini afanye.
Angalizo tujitahidi kuwa makini na tusimwamini mtu yeyote kwa kujipatia utajiri wa haraka haraka.
nawakilisha.
 
Mkuu hii thread yako mimi sijaielewa. Ina maana huyo mfanyabiashara kwa kuwa na hizo M. 30, hakuwa tajiri au alikuwa anataka utajiri zaidi, au ndo mambo ya VIJISENTI? Naomba ufafanuzi, tafadhali!
 
Alikuwa ANATAKA UTAJIJRI ZAIDI. Alivyouzia dola ilikuwa cheap exchange
 
Back
Top Bottom