respect wa boda
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 4,556
- 3,838
Wakuu Salaam,
Naam hiyo ndiyo halihalisi kwenye mitaa mbalimbali ya Kariakoo hapa Dareslaam. Dola imekuwa adimu sana,upatikanaji wake ni wa shida. Hali hiyo imesababisha kupaa kwa Dola, haikamatiki.
Matokeo yake ni kupanda kwa bidhaa mbalimbali kwenye masoko kadhaa hapa Mjini. Hivi sasa kama unataka kwenda shopping na ni mtu mwenye angalau familia ya watu watatu, basi beba kuanzia shilingi 400.000 vinginevyo utaumbuka mbaba wa watu.
Kifupi hali ni tete, waliotuaminisha kuwa hapa itakuwa kazi tu, wala hatuwaoni wakichukua jitahada za makusudi kushusha dola hapa nchini. Yaani hali hii imesababisha hata wenye nyumba kutaka kulipwa kwa dola pango la nyumba zao wakidai shilingi inashuka thamani kila uchao.
Jamani hebu fanyeni "kazi tu" tupate unafuu kitaa.
BACK TANGANYIKA