SAGAI GALGANO
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 43,707
- 60,753
Na zile Noah zetu ni aje?
Rais hapaswi kulaumiwa kwenye hili na anahitaji kutiwa moyo na watanzania wote bila kuingiza itakadi za vyama. Kwa hakika amepambana lakini kuna sehemu tunakwama, hasa kwenye utaalamu wa mambo haya ya madini na mikataba mibovu ambayo inasimamiwa kimataifa na ilishaingiwa huko nyuma.
Naamini Kinu cha uchenjuaji makinikia kitakua suluhisho la huu wizi wa mchana, rais aendelee kubana hayo mkontena haiwekani muuza korosho ajiendeshe kwa kuuza maganda ya korosho badala ya korosho yenyewe. Tumeibiwa sana.
Hebu tueleze japo kiduchu nini kinaendelea maana zile mbwembwe hatuzioni tena kinani?Ungekuwa na elimu ya coporate world usingeshindwa kujua kinachoendelea...
Nakubaliana na wewe kwenye kujenga mustakabali mmoja wa kitaifa,kila upande ujishushe,wawe kitu kimoja washauriane,hapo tutafika. Nionavyo mimi haya mambo ya kutunishiana misuli bila kukaa na kutafuta mustakabali wa pamoja hayana tija kwa kila upande kwa Taifa hili. Nadhan tunakosa baraka za Mungu kwa mtengano wetu usio wa lazima.Hakuna malipo nje ya mkataba,
Cha muhimu ni srikali kuweka wazi nikataba ijadiliwe kwa uwazi ili kuondoa au kupunguza mambo ya asilimia kumi. Botswana na Ghana waliweza kutikana na uwazi na uzakendo was mamlaka husika (parliament na rais)
Pia ni lazima wabunge na watz wore tuacge siasa za kubaguana kwa vyama Bali tufanye siasa za hoja kuhusu rasilimali zetu. I
Haiwezekani wabunge wanazomeana kisa tu mcgango umetolewa na mpinzani
Hatustahili/tunastahili kulipwa kutokana na mikataba na si mazungumzo ya kupata public support
Tunapigwa sana ni wimbo mpya wenye chorus ya zamani.Najiuliza tuna miaka miwili sasa tangu tuanze kuimba hii nyimbo je hatua zilizochukuliwa zina tija kiasi gani?Usichokielewa au unachokifumbia macho ni kuwa hizo data ulizotumia ni sehemu ya udanganyifu wa makampuni ya madini duniani! Hawajawahi kuweka wazi data halisi za uvunaji na faida ya dhahabu!!! Nikuulize kitu! Mtendaji wa barick alikuja DSM na ndege binafsi lakini miaka yote hapa nchini hawajawahi kulipa kodi itokanayo na faida zaidi ya tozo ndogo ndogo kama mirahaba! Miaka yote wanadai wanapata hasara, kwa nini hawafungashi virago? Mbona wanahisa wanapeana gawio kila mwaka? Mbona wanatembelea ndege binafsi ili kutetea mgodi unaozalisha hasara? Ukweli ni kwamba tunapigwa sana!!!
mkuu,mimi naamini tutalipwa siku moja,nauliza tu,hivi kwa uwezo wako wa kujua mambo nyeti kuna kipengele cha kuwapo kwa riba katika hayo malipo incase wakiwa wanachelewa kulipa??maana wao mikopo yao mingi kama si yote wanaweka riba sisi tulikumbuka kuweka kipengele cha riba?hebu nusanusa mkuu ulete mrejeshoKwa hiyo Kwa taarifa hii ya Pasco ndio unaamini hatutalipwa?
Kweli naamini maneno ya Trump
si tungewaona kila siku kwenye tv yao......Yale makontena bado tunayashikilia kwani?
Na wale watu wa Acacia kutoma Canada bado wanaendelea na mazungumzo au walisharudi kwao? Kimya kweli naona
....The late Nyerere alishauri yasichimbwe mpaka pale tutakapokuwa na capacity ya kutosha but tukamuona lofa...Rais hapaswi kulaumiwa kwenye hili na anahitaji kutiwa moyo na watanzania wote bila kuingiza itakadi za vyama. Kwa hakika amepambana lakini kuna sehemu tunakwama, hasa kwenye utaalamu wa mambo haya ya madini na mikataba mibovu ambayo inasimamiwa kimataifa na ilishaingiwa huko nyuma.
Naamini Kinu cha uchenjuaji makinikia kitakua suluhisho la huu wizi wa mchana, rais aendelee kubana hayo mkontena haiwekani muuza korosho ajiendeshe kwa kuuza maganda ya korosho badala ya korosho yenyewe. Tumeibiwa sana.