Dola bandia kutoka Korea Kaskazini zilivyosambaa duniani na kutumika kwa zaidi ya 20 bila kujulikana.

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,593
32,681

Dola bandia zilizotumika kwa miongo miwili na kupumbaza dunia​

fedha bandia

Noti hiyo ya dola bandia haikuwa na makosa yoyote na hata maafisa wa kitengo cha ujasusi hawakuweza kubaini iwapo ilikuwa dola bandia ama nakala mbele yao.

Ni baada ya kipindi kirefu cha uchunguzi ndiposa waliweza kuthibitisha kwamba zilikuwa hela bandia.

Lakini noti hizo za dola mia moja zilikuwa hazina dosari yoyote hadi zikapewa jina ''The Super fake Dollars''.

Zilikuwa na rangi kama ile ya noti halisi za dola za Marekani.
Pia zilichapishwa katika karatasi iliokuwa sawa na ile ya pesa halisi ikiwa na robo tatu ya pamba na robo ya kitani{linen}.
Picha ya noti hizo ilikuwa bora zaidi ya zile zilizochapishwa na shirika la kuchapisha fedha Marekani.

Hata zilishindwa kubaini noti hizo bandia

Mashine ya kuhesabu noti katika benki pia zilishindwa kubaini uhalisia wake
Zilikuwa na tofauti kidogo sana, wakati Gazeti la The New York Times liliporipoti kwamba fedha hizo hazikuwa halisi, Marekani lishangazwa kwamba fedha bandia ziliweza kupita benki zake bila kujulikana , kwasababu hakuna aliyeweza kubaini tofauti,
Fedha hizo za Super Dollars zilisambaa kote dunini kati ya miaka 1990 na 2000.
Wakati wa miaka hii , Marekani iliamua kubadilisha noti ya dola 100 mara mbili lakini watengenezaji wa fedha hizo bandia walifanikiwa kubadilisha fedha hizo na kufanana kama zile zinazochapishwa na serikali😄😄
Zilipatikana nchini Denmark, Ufaransa, Austria, Ujerumani, Latvia, Urusi, Czech Republic , Ireland na Urusi.

Wahalifu nchini Urusi walizitumia bila aibu.

Kwa miaka kadhaa zilikuwa mwiba kwa shirika la ujasusi la Marekani FBI.
Hawakujua ni nani aliyekuwa akizichapisha, Ilichukua operesheni kali ya miaka minane ili kuanza kuwakamata wahusika.
Walifanikiwa kuwakamata washukiwa wa kwanza mjini California na New Jersey, baada ya wachunguzi kupata makasha ya fedha hizo kutoka katika meli kutoka kusini mashariki mwa bara Asia.

Wale waliokamatwa walikuwa na uhusiano na wahalifu wa kimataifa, lakini maafisa wa shirika la FBi walikuwa wakishuku kwamba mtandao huo ulikuwa mkubwa.

Fedha hizo hazikutengenezwa na wahalifu wa kawaida ama mtandao wa wahalifu, lakini zilitengenezwa na serikali ya Korea Kaskazini... Serikali ya Marekani ilisema.
Trump akiamkuana na rais Kim Jong un

Trump akisalimiana na rais Kim Jong wa North Korea.

Mara kwa mara fedha hizo zilipatikana katika mikono ya wanadiplomasia wa Korea Kaskazini, pengine kuongeza mapato ya taifa hilo ambalo lilikuwa likikumbwa na matatizo ya njaa na kuanguka kwa mshirika wake mkuu Muungano wa Usovieti.

Hata hivyo Korea Kaskazini inakana kuhusika katika kuchapisha fedha hizo.
''Korea Kaskazini imekana kuhusika katika usambazaji na uchapishaji wa sarafu bandia , lakini Ushahidi unaonesha wazi kwamba ni wao'', alisema Daniel Glazer naibu waziri wa masuala ya Uhalifu wa kifedha akizungumza na New York Times.

''Hakuna masuali yoyote juu ya kuhusishwa kwa Korea Kaskazini'', alisema.
Mamlaka nyengine zilitaja kughushi huko kama shambulizi baya la mfumo wa fedha wa Marekani.

Hatahivyo , kipaumbele cha FBI kilikuwa kusitisha usambazaji wa fedha hizo katika taifa la Marekani.
Jumba la Playboy lilikuwa na jukumu muhimu katika kuangamiza mtandao huo wa uhalifu

Jumba la Playboy

Jumba la Playboy lilikuwa na jukumu muhimu katika kuangamiza mtandao huo wa uhalifu.
Kuwasili kwa dola hizo bandia katika bandari zake kulitokana na kuwasili kimagendo kwa sigara na dawa za kulevya.

FBI ilitumia mbinu ya kuwavutia idadi kubwa ya wahalifu wanaohusishwa na njama hiyo, Harusi bandia na sherehe ya kutalakiana katika jumba la Playboy.

Mpango huo ulifanikiwa na watu 87 walikamatwa, lakini idadi ndogo ya dola hizo bandia zinadaiwa kuendelea kusambaa hadi leo.
Jumba hilo la Playboy lilikuwa na jukumu muhimu la kusambaratisha matandao huo wa uhalifu.
 
Kwanini yeye Marekani pekee ndie awe na haki ya kuchapisha hizo dollars ilihali zinatumika dunia nzima? Ni kwanini isiundwe sarafu ya dunia itakayosimamiwa na shirika la kiduniaa linaloundwa na nchi zote duniani? Mfanockama Euro, ila iwe ya Dunia
 
Soma tena mkuu.

Yani hapo tatizo ni kwamba dola hizo zinapoitwa bandia maana yake zilichapishwa nje ya sheria
 
Soma tena mkuu.

Yani hapo tatizo ni kwamba dola hizo zinapoitwa bandia maana yake zilichapishwa nje ya sheria
Nafahamu, ila nje ya mada, ni haki kwa USA pekee kuwa na mamlaka juu ya Sarafu isiyotumika USA pekee, yaani mfano tuseme Ufaransa pekee awe na haki ya kudurufu Euro ambayo haitumiki Ufaransa pekee?

Kuwa taifa kubwa kuna shida sana.

Yani bajeti yako inakuwa kwenye kujilinda, kulinda mali zako na watu wako.
 
Kwanini yeye Marekani pekee ndie awe na haki ya kuchapisha hizo dollars ilihali zinatumika dunia nzima? Ni kwanini isiundwe sarafu ya dunia itakayosimamiwa na shirika la kiduniaa linaloundwa na nchi zote duniani? Mfanockama Euro, ila iwe ya Dunia
Hakuna central bank ya dunia nzima.

Central bank ndo wanaohusika kutengeneza fedha husika na kuilinda.

Euro zone wana cetral bank. Ndo wanaochapisha Euro.

US Dollar inatengenezwa na Federal Reserve ya US na ndo wanaotakiwa kulinda kwa gharama yeyote ile.
 
Ndio nauliza, ni kwanini isianzishwe? Au huelewi maana ya ‘Kuanzishwa’, jaribu kulegeza ubongo ndugu, usiwe rigid hivyo
 
Nafahamu, ila nje ya mada, ni haki kwa USA pekee kuwa na mamlaka juu ya Sarafu isiyotumika USA pekee, yaani mfano tuseme Ufaransa pekee awe na haki ya kudurufu Euro ambayo haitumiki Ufaransa pekee?

Naona ni mfumo waliouweka duniani kwaajili ya maslahi yao tu
 
Back
Top Bottom