Dola bandia kutoka Korea Kaskazini zilivyosambaa duniani na kutumika kwa zaidi ya 20 bila kujulikana.

Ndio nauliza, ni kwanini isianzishwe? Au huelewi maana ya ‘Kuanzishwa’, jaribu kulegeza ubongo ndugu, usiwe rigid hivyo
Itakuja kuanzishwa huko mbele ya safari wakati wa utawala wa Mpinga Kristo. Wakati huo kutakuwa na sarafu moja na dini moja dunia nzima. Ukitaka kujua kwa undani juu ya haya soma Biblia, Kitabu cha Ufunuo wa Yohana.
 
Ndio nauliza, ni kwanini isianzishwe? Au huelewi maana ya ‘Kuanzishwa’, jaribu kulegeza ubongo ndugu, usiwe rigid hivyo
Sio kitu rahisi hivyo.

EU walijaribu na kuna nchi wameanza kujitoa kama UK.

Monetary objectives 3rd world countries ni tofauti na 2nd na 1st world countries.

Spending & investment patterns ni moja ya factors za kutengeneza monetary policies za nchi husika.
 
Uking'amua suala la uchapishaji wa hela, World Bank, IMF, US Dollar, basi unaweza kigundua kuwa, Marekani itaendelea kuwa nchi tajiri miaka na miaka
 
Hakuna central bank ya dunia nzima.

Central bank ndo wanaohusika kutengeneza fedha husika na kuilinda.

Euro zone wana cetral bank. Ndo wanaochapisha Euro.

US Dollar inatengenezwa na Federal Reserve ya US na ndo wanaotakiwa kulinda kwa gharama yeyote ile.
Haya mambo yote ya Centralization yatakuja kuwa history baada ya Cryptocurrencies kumature.
 
Nafahamu, ila nje ya mada, ni haki kwa USA pekee kuwa na mamlaka juu ya Sarafu isiyotumika USA pekee, yaani mfano tuseme Ufaransa pekee awe na haki ya kudurufu Euro ambayo haitumiki Ufaransa pekee?

Sasa mkuu kama kila mtu akiwa na haki ya kuchapisha hizo dolla si kutatokea anguko la kiuchumi?
 
Haya mambo yote ya Centralization yatakuja kuwa history baada ya Cryptocurrencies kumature.
Unazungumzia crypto ambazo kwa mwezi mmoja tu leading crypto inashuka 50% ya thamani yake. Ni mwaka gani duniani USD iliwahi shuka thamani hata kwa 10% kwa mwezi mmoja.

Hakuna vita, corona inadhibitiwa, hakuna mdororo wa uchumi duniani ila crypto kubwa kina BTC, ETH na Doge zimeshuka 60%, 50% ya thamani kwa mwezi. Nchi gani itumie hela zisizo stable kwenye mzungumzo namna hii.

Labda kuna vitu vibadilike lakini si kwa utaratibu huu.
 
Sasa mkuu kama kila mtu akiwa na haki ya kuchapisha hizo dolla si kutatokea anguko la kiuchumi?
Sio kila mtu, iundwe sarafu ya dunia na isimamiwe na jumuia ya kidunia, mfano Euro kwa Ulaya, sasa iwe sarafu ya kidunia inayosimamiwa si na taifa moja, bali mamlaka ya kidunia itakayoundwa
 
Unazungumzia crypto ambazo kwa mwezi mmoja tu leading crypto inashuka 50% ya thamani yake. Ni mwaka gani duniani USD iliwahi shuka thamani hata kwa 10% kwa mwezi mmoja.

Hakuna vita, corona inadhibitiwa, hakuna mdororo wa uchumi duniani ila crypto kubwa kina BTC, ETH na Doge zimeshuka 60%, 50% ya thamani kwa mwezi. Nchi gani itumie hela zisizo stable kwenye mzungumzo namna hii.

Labda kuna vitu vibadilike lakini si kwa utaratibu huu.
Haya mambo yote ya Centralization yatakuja kuwa history baada ya Cryptocurrencies kumature.
 
Hii thread ina maana North Korea wana akili sana kutuzidi sisi waafrika hata baadhi ya wazungu.
Wamevumbua hio dolla feki.
Wameweza kuunda mabomu ya nyuklia
Wanaunda IBM(intercontinetl balistic misile, teknolojia hii inawezesha hata kurusha satelite).
Wanarutubisha nyuklia.
Wanajiundia baadhi ya silaha.
Wanafanya biashar za magendo kwenye black markert.
Mabingwa wa ku hack dunuani.
Wanajiundia window kwa kikorea.
Je kuna haki kuiweka Korea na Tanzania kundi moja la nchi masikini?
 
Mmmh ngumu kumeza siamini Kama marekani inaweza ikafikia kiwango hiko cha uzembe
Kwann usiamin mkuu akili uzidiana ebu soma na hii hawa ni wa Ghana wakachakaza wa marekani

 

Dola bandia zilizotumika kwa miongo miwili na kupumbaza dunia​

fedha bandia

Noti hiyo ya dola bandia haikuwa na makosa yoyote na hata maafisa wa kitengo cha ujasusi hawakuweza kubaini iwapo ilikuwa dola bandia ama nakala mbele yao.

Ni baada ya kipindi kirefu cha uchunguzi ndiposa waliweza kuthibitisha kwamba zilikuwa hela bandia.

Lakini noti hizo za dola mia moja zilikuwa hazina dosari yoyote hadi zikapewa jina ''The Super fake Dollars''.

Zilikuwa na rangi kama ile ya noti halisi za dola za Marekani.
Pia zilichapishwa katika karatasi iliokuwa sawa na ile ya pesa halisi ikiwa na robo tatu ya pamba na robo ya kitani{linen}.
Picha ya noti hizo ilikuwa bora zaidi ya zile zilizochapishwa na shirika la kuchapisha fedha Marekani.

Hata zilishindwa kubaini noti hizo bandia


Mashine ya kuhesabu noti katika benki pia zilishindwa kubaini uhalisia wake
Zilikuwa na tofauti kidogo sana, wakati Gazeti la The New York Times liliporipoti kwamba fedha hizo hazikuwa halisi, Marekani lishangazwa kwamba fedha bandia ziliweza kupita benki zake bila kujulikana , kwasababu hakuna aliyeweza kubaini tofauti,
Fedha hizo za Super Dollars zilisambaa kote dunini kati ya miaka 1990 na 2000.
Wakati wa miaka hii , Marekani iliamua kubadilisha noti ya dola 100 mara mbili lakini watengenezaji wa fedha hizo bandia walifanikiwa kubadilisha fedha hizo na kufanana kama zile zinazochapishwa na serikali😄😄
Zilipatikana nchini Denmark, Ufaransa, Austria, Ujerumani, Latvia, Urusi, Czech Republic , Ireland na Urusi.

Wahalifu nchini Urusi walizitumia bila aibu.

Kwa miaka kadhaa zilikuwa mwiba kwa shirika la ujasusi la Marekani FBI.
Hawakujua ni nani aliyekuwa akizichapisha, Ilichukua operesheni kali ya miaka minane ili kuanza kuwakamata wahusika.
Walifanikiwa kuwakamata washukiwa wa kwanza mjini California na New Jersey, baada ya wachunguzi kupata makasha ya fedha hizo kutoka katika meli kutoka kusini mashariki mwa bara Asia.

Wale waliokamatwa walikuwa na uhusiano na wahalifu wa kimataifa, lakini maafisa wa shirika la FBi walikuwa wakishuku kwamba mtandao huo ulikuwa mkubwa.

Fedha hizo hazikutengenezwa na wahalifu wa kawaida ama mtandao wa wahalifu, lakini zilitengenezwa na serikali ya Korea Kaskazini... Serikali ya Marekani ilisema.
Trump akiamkuana na rais Kim Jong un

Trump akisalimiana na rais Kim Jong wa North Korea.

Mara kwa mara fedha hizo zilipatikana katika mikono ya wanadiplomasia wa Korea Kaskazini, pengine kuongeza mapato ya taifa hilo ambalo lilikuwa likikumbwa na matatizo ya njaa na kuanguka kwa mshirika wake mkuu Muungano wa Usovieti.

Hata hivyo Korea Kaskazini inakana kuhusika katika kuchapisha fedha hizo.
''Korea Kaskazini imekana kuhusika katika usambazaji na uchapishaji wa sarafu bandia , lakini Ushahidi unaonesha wazi kwamba ni wao'', alisema Daniel Glazer naibu waziri wa masuala ya Uhalifu wa kifedha akizungumza na New York Times.

''Hakuna masuali yoyote juu ya kuhusishwa kwa Korea Kaskazini'', alisema.
Mamlaka nyengine zilitaja kughushi huko kama shambulizi baya la mfumo wa fedha wa Marekani.

Hatahivyo , kipaumbele cha FBI kilikuwa kusitisha usambazaji wa fedha hizo katika taifa la Marekani.
Jumba la Playboy lilikuwa na jukumu muhimu katika kuangamiza mtandao huo wa uhalifu

Jumba la Playboy

Jumba la Playboy lilikuwa na jukumu muhimu katika kuangamiza mtandao huo wa uhalifu.
Kuwasili kwa dola hizo bandia katika bandari zake kulitokana na kuwasili kimagendo kwa sigara na dawa za kulevya.

FBI ilitumia mbinu ya kuwavutia idadi kubwa ya wahalifu wanaohusishwa na njama hiyo, Harusi bandia na sherehe ya kutalakiana katika jumba la Playboy.

Mpango huo ulifanikiwa na watu 87 walikamatwa, lakini idadi ndogo ya dola hizo bandia zinadaiwa kuendelea kusambaa hadi leo.
Jumba hilo la Playboy lilikuwa na jukumu muhimu la kusambaratisha matandao huo wa uhalifu.
Kwahiyo wamefanikiwa kuzitokomeza??
 
Back
Top Bottom