Dola: 1 = 1,750 TZS, Wizara ya Fedha mtutasaidiaje?

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Wana JF.
Kila siku kukicha shilingi yetu inazidi kuporomoka kwa kasi ya ajabu.

Leo Dola moja ya Marekani imefika Sh1750 ya Tanzania, mwenye majukumu ya Uchumi wetu ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu.

Hivi serikali inafanya juhudi za makusudi kuokoa hii hali au ndio tunaelekea kama Zimbambwe, kwenda sokoni na kapo la hela.
Wadau hii hali inakuaje
 
Wapuuzi watakwita wewe ni mchochezi kwa hii thread, ila kwa ufupi nchi imemshinda kabisa kikwete!!!!!!!!!
 
Nakumbuka sana Pouni(1Pound was =20Tsh) na PIa Dala(1USD was = 5TSh) lakini sasa ni balaaaaaaaaaa,Jeikei upo?
 
Wapo mapumzikoni wanaendelea kuchambua kwa nini tanzania ni maskini na watakuja na mkakati na mipango ya kututoa kwenye umaskini
 
Sio kwetu tu!Hata jirani hapo Kenya rate imebadilika kwa high speed!Usd 1=Kshs100
 
Sio kwetu tu!Hata jirani hapo Kenya rate imebadilika kwa high speed!Usd 1=Kshs100
Utetezi dhaifu sana huu na ni non-scientific!!
Kwani Kenya ndiyo standard unit yako ya kujipimia?
Kama shilingi inaporomoka simply ni kwamba hakuna exporting.
Na for sure hakuna exporting maana hakuna umeme nchi hii, utapeleka kitu gani kwa watu bila kukiprocess viwandani?
Shilingi haiwezi kupanda kwa kushika bastola majukwaani!
 
Haaaaa umenikumbusha ile mtoto karudi nyumbani akampa mama matokeo ya mtihani:

Mama:Mbona umefeli mtihani wako huu??

Mtoto:sio mimi mama niliefeli hata monitor nae kaferi haaaaaaa

Sio kwetu tu!Hata jirani hapo Kenya rate imebadilika kwa high speed!Usd 1=Kshs100
 
Mkulo alishasema bungeni kuwa tatizo la kuporomoka kwa shilingi lipo nje ya uwezo wa serikali.
 
Hizi zote ni athari za uhaba wa umeme, viwanda vimepunguza uzalishaji kama si kusimama kabisa, tunazidi kuagiza vitu toka nje kwasababu sisi hatuzalishi vya kutosha achilia mbali kupeleka huko nje. Serikali yenyewe ni legelege, inatoa ngonjera tu kuhusu umeme.
 
Wana JF.
Kila siku kukicha shilingi yetu inazidi kuporomoka kwa kasi ya ajabu.

Leo Dola moja ya Marekani imefika Sh1750 ya Tanzania, mwenye majukumu ya Uchumi wetu ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu.

Hivi serikali inafanya juhudi za makusudi kuokoa hii hali au ndio tunaelekea kama Zimbambwe, kwenda sokoni na kapo la hela.
Wadau hii hali inakuaje

Na bado!
Haya ndio matokeo yake, hakuna uzalishaji unaoendelea na export zetu zimeshuka sana badala yake tumekuwa soko la wengine. Hivi nguvukazi inyopotea bure kule Igunga wangekuwa mikoani wanahamasisha Kilimo Kwanza labda tungepata matumaini fulani.
 
Mwaka 1983 Dola 1 ilikua sawa na sh 12!leo dola 1 sawa na sh 1750 na huku tuna export gold,tanzanite,diamond,coal.
 
Kweli maumivu bado yanakuja. Ripoti ya BoT inaonyesha kuwa hata balance of payment deficit imefika asilimia 8, hapo bado hatujaona effects za kutumia dola nyingi kwa ajili ya emmergence power projects. Ni lazima zitapandisha deficit ya balance of payments na kupunguza kiwango cha dola kwenye mzunguko, kwa hakika dola itazidi kupaa na tutaumia sana kama Mkulo akiendelea kuamini kuwa haya ni matatizo yaliyo nje ya uwezo wa serikali.
 
Wana JF.
Kila siku kukicha shilingi yetu inazidi kuporomoka kwa kasi ya ajabu.

Leo Dola moja ya Marekani imefika Sh1750 ya Tanzania, mwenye majukumu ya Uchumi wetu ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu.

Hivi serikali inafanya juhudi za makusudi kuokoa hii hali au ndio tunaelekea kama Zimbambwe, kwenda sokoni na kapo la hela.
Wadau hii hali inakuaje
aisee imefika 1750 tu? mi napenda ifike 2000 tusipate taabu ya chenji, tehetehe....
 
Hili suala inabidi Magamba wawajibike ni hatari kwa uchumi wetu.
Ukiwa na dola 1000 unapata Sh1.675.000
 
Back
Top Bottom