Dokta Mwakyembe na degree zake 4 hataki kuzoeleka na darasa la 7, akifa atazikwa na nani?

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,262
Nimemtafakari sana Harrison Mwakyembe, kwamba yeye kwakuwa ana degree 4 basi hataki kusemeshwa wala kukosolewa na walioishia tu darasa la 7.

Sasa swali langu: Akifa atazikwa na nani? Kaburi lake watachimba Madaktari wa Falsafa kama yeye pekee? Na kwa hakika Mwakyembe alishapatwa na msiba nyumbani kwake, nani walimzika kipenzi chake?

Lakini pia wapiga kura wa Mwakyembe kule Kyela, watu wanaompa kula yake na kiburi chote hiki alicho nacho wana elimu gani? Wote ni Madaktari wa Makaratasi Kama yeye?

Huyu kweli ndiyo maana alikana thesis yake kuhusu kuunga mkono hoja ya serikali 3, Daktari mwingine wa majalalani.
 
3E12430B-E055-482B-B140-57FAD1FC7513.jpeg
 
Sasa swali langu: Akifa atazikwa na nani? Kaburi lake watachimba Madaktari wa Falsafa kama yeye pekee? Na kwa hakika Mwakyembe alishapatwa na msiba nyumbani kwake, nani walimzika kipenzi chake?
Umegeuza kauli ya mwakyembe kwa manufaa yako
Kauliza mtu wa darasa la saba,utamshauri nini mtu mwenye degree 4 kama yeye?
Chukulia tu mfano wewe na darasa lako la 7,halafu unabishana kuhusu sheria na Phd holder
 
Inatosha jamani Khaa!
Acha wamfundishe.Viongozi wa Sasa wa Tanzania ni wa ajabu sana sana.Umewahi kiona kitabu cha A MAN OF THE PEOPLE? Haswaa yaliyomo mle ndo hapo Tanzania kwa asilimia 95%.Hovyo kabisa
 
Mwaki katuaibisha Sana wanyakyusa dah! Haya mambo ya kujisifia na kujigamba huwa tunasikia kwa wahaya tu
 
Kaonyesha anavyowadharau wapiga kura wake wa kyela, ambao Nina hakika zaidi 90% hapana elimu ya degree
 
.
Umegeuza kauli ya mwakyembe kwa manufaa yako
Kauliza mtu wa darasa la saba,utamshauri nini mtu mwenye degree 4 kama yeye?
Chukulia tu mfano wewe na darasa lako la 7,halafu unabishana kuhusu sheria na Phd holder
Inawezekana sana tu.
 
Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom