Dokta Kitila Mkumbo usikimbie hoja mzee wangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dokta Kitila Mkumbo usikimbie hoja mzee wangu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sokomoko, Jun 28, 2011.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Baada ya mdau sulphadoxine kuleta upupu ufuatao.

  Mheshimiwa Dokta Kitilla Mkumbo akamjibu...........

  Nilipomwona Dokta wa ukweli yupo online na alikuwa akifatilia mada nikamuuliza


  Mheshimiwa Mkumbo.

  Japo mimi ni mtanzania lakini sina usahaulifu kama wengi miongoni mwetu tulivyo, nakumbuka wewe ni mmoja wa watu walioinajisi demokrasia ndani ya chama cha "demokraisa" kwa kuwachagua wanawake watakaopita kwenye viti maalumu ndani ya chama chako. Vigezo ulizingatia mwenyewe kwani katiba ya chama haijaainisha vigezo vya watakao teuliwa viti maalumu.

  Tunajua kulifanyika mchakato wa kidemokrasia kupitia baraza la wanawake la chadema BAWACHA lililokuwa likiongozwa na mwana mama aliejitolea kwa hali na mali kukuza chama MS Letcia Musori. Huyu mama alikuwa miongoni mwa wanawake waliochaguliwa na vikao halali vya BAWACHA lakini mchakato ule wa BAWACHWA ulianchwa ukachaguliwa wewe "mwanaume" uwachagulie "wanawake" wawakilishi wao what a joke! Anyway sio mbaya lakini unaposema
  Wakati wewe ulikuwa mmoja wao uliewafanyia short cut baadhi ya waheshimiwa ina maana rahisi sana kuwa wewe hutembei kwenye maneno yako! Hatujui utashi gani kuwa weka juu kina Rose Kamili aliekuwa CCM na Diwani mpaka kabla ya uchaguzi mkuu Mama yangu Mama Naomi Kahihula aliekuwa ananifundisha CBE mpaka kabla ya Uchaguzi hawa wamekuwa wanawake wa juu CDM wamewapita hata wale waliokuwepo tangu mwiaka ya mwanzoni mwa 2000. Siri mnaijua wewe na mwenyekiti wako ila ukweli ni kwamba wewe mwenyewe hukuwajibika kikamilifu kitaaluma na kitaalamu Vipi wanafunzi uliokuwa ukiwahutubia wawajibike na sio kufuata nyayo zako?

  Binafsi sifurahiwi sana na utendaji wako unaonyesha wewe ni mtu wa mizaha na usie na hoja nakumbuka ulitoa jibu kuwa [​IMG] Originally Posted by Kitila Mkumbo [​IMG]
  Tatizo la huyu mama yetu alikariri kwamba yeye lazima ilikuwa awe mbunge wa viti maalumu kwa sababu tu alikuwa mwenyekiti wa BAWACHA kitaifa. Bahati mbaya kwake ni kwamba hatukuwa na kigezo specific cha kumlenga mwenyekiti wa bawacha au kiongozi yeyote mwingine. Katika vigezo tulivyotumia yeye aliangukia kwenye namba 29 kama inavyoonekana katika orodha hapa chini ya first 40 candidates.

  Katika safari hii ya mapambano sio abiria wote watakaofika mwisho wa safari; wapo watakaoshukia njia-huyu ni mojawapo!!

  Hukutupa data ya jinsi ulivyo wa rank hawa wanawake wa juu kwani kwa kuzingatia haki Mama Musori alikuwa Mwenyekiti wa baraza la wanawake Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema na Mweka Hazina wa Umoja wa Madiwani wa Chadema na kukidhi vigezo vilivyowekwa pia Musori alikuwa anajua Kiingezera, Kijerumani na Kiswahili akiwa na Cheti cha Nurse Midwife (Diploma) aliyoipata Ujerumani pia amekuwa akiitumikia CDM kwa muda na kina Rose Kamili wamemkuta!

  Sote tunajua mbunge akimaliza muda anapata kiinua mgongo cha asilimia 40 ya mshahara wake kwa mazingira uliyowateua itakuwa ni vigumu kuamini hakukuwa na rushwa na upendeleo hatujui ulipata/utapata nini kama ahsante ya uteuzi wako uliotukuka. Kwa uchache kina Rose Kamili wataondoka na kitu kama 45 mil baada ya kumaliza term yao ya ubunge ni dhahiri umewatafutia short cut ya nguvu na kwa hili nakupa hongera sana.

  Kumalizia napenda kukufahamisha umewasaidia short cut kina Rose Kamili, Naomi Kaihula, Chiku Abwao ya maisha ungewaacha waweke vipaumbele kwenye kufanya kazi kwa bidii ya kukuza chama, maarifa na kukipenda chama chao. Hakuna short cut ya mafanikio kwenye chama zaidi ya kuwajibika na kuchapa kazi kwa bidii na upendo wa dhati kwa chama na kwa wananchi.

  Dokta napenda uelewe kuwa
  "You can fool some of the people all of the time, and all of the people some of the time, but you cannot fool all of the people all the time." – Abraham Lincoln

  Unafiki wa waandishi wa habari.

  Kuna waandishi wa habari wanasifika kwa vichwa vizuri vizuri vya mada zao kama Maswali Magumu na Ansert Ngurumo, Kuna mmoja anajiita yeye ni mwana wa shambani ilhali anakula bata Marekani amepewa coverage kubwa sana kule TZ Daima hawa hata siku moja huwezi kuwasikia wakiuliza maswali magumu ya kuihusu CDM nasema CDM kikifa tusmtafute mchawi sote tunatunahusika watazamaji na wachezaji kumbukeni CDM nyie ndio tumaini la vijana wengi wanyonge ipo siku watagundua hila na uozo wenu na kuingia mitini.


  Uchu wa cheo waiza,macho wengi hupofuka,
  Mwenyewe hujilemaza,kuvaa kustahika,
  Siachi kujiuliza,vipi atasetirika ?
  Hata upake marashi,kilicho'za kimeoza.

  Wavivu tunawaoza,kwa vyeo kuwajibika,
  Ajizi zinapoanza,jukwaani twalalamika,
  Jamaa twapa vyeo kwanza ,ukubwa kuwapachika,
  Hata upake marashi,kilicho'za kimeoza.

  Vigumu nawaeleza,nchi kuweza jengeka,
  Huku tunafuga funza,madaraka kuja shika,
  Vidole kuviongoza,twende tunapopataka,
  Hata upake marashi,kilicho'za kimeoza

  Kuzoza nilikizoza,si mtu wa kusikika,
  Hodari waliojifanza,waona wameelimika,
  nini utachowafunza,waweze tena kushika,
  Hata upake marashi,kilicho'za kimeoza.

  Yangu sasa namaliza,cheo sitaki kushika,
  Najificha na ajuza,shaibu nimetosheka,
  Anijalie Muweza,hatima kurehemeka,
  Hata upake marashi,kilicho'za kimeoza

   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Katafute uji unywe mtoto huna la maana
   
 3. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ulitaka tusifie tu hata kama anayosema hayaendani na alivyo?
   
 4. A

  Awo JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Dk Mkumbo sio size yako tafuta shughuli nyingine ufanye. Mshauri Mama Musori aende CCM wanakochaguana kwa kukaa kwenye chama kwa muda mrefu. Unatupotezea muda bana!
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hoja inaelea haina mashiko hii ni JF
   
 6. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Samahani wewe ni mmoja wa waliopewa hiyo shot cut nini? maana naona umetaharuki! pole sana ila ukweli dawa hata kama unauma...
   
 7. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Well kuhusu CCM juu ya mambo yao ya ufisadi wanao mfumo wa kidemokrasia wa kuchagua wanawake wa kuwawakilisha wanawake wenzao bungeni juu ya mambo yao ya ufisadi hutasikia ameteuliwa John wala Edward kuwachagua wanawake watakao wawakilisha wanawake kwenye viti maalum bungeni.
   
 8. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
 9. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sio size yangu kwa sababu yeye anakaa uzunguni mie nakaa uswahilini kwa mtogole? no ni saize yangu mie natoka Nduguti na yeye anatoka moja ya tarafa za wilaya ya Iramba mimi na yeye wote tumekulia matogo na sasati. Ila yeye anaweza akawa matawi kwa kuwa ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani kwahiyo ki status ana cheo lakini tukirudi nyumbani sie sote ni wanyiramba bila kujali huyu anatoka gumanga au kinangiri!
   
 10. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu mtumie PM mmalizane huko huko
   
 12. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Natilia shaka lengo lako. Kama ni mwanachama wa CDM tafadhali rejea taraibu za chama. Kama ni wa CCM haikuhusu na nadhani ingekua vyema ukajadiri taratibu za chama chenu hapa tuzilinganishe zinaweza kuwa bora. Ila sisi "wengine" tunaamini Dr. Mkumbo alifanya kazi kitaalamu.
   
 13. c

  carefree JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Sokomarazote huwa natofautiana na wewe ila kwenye hili tuko pamoja mkuu
  15. Joyce Mukya alijiunga na cdm june 2010 hata kusimama jukwaani kujieleza mpaka sasa ni utata wananchji wa arusha hamjui huyu ni mkazi wa tangibovu mbezi jiji dar arusha alikuwa na hawarayake EAComunity akaishi kama miezi mitatu akarudi dar

  Kitila ulichemsha na kama lema anasema kuwa anaamini kwenye haki mbona hili hakuliongelea au kwa kuwa ndiye aliyemkuwadia kwa Mbowe?
   
 14. M

  Marytina JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Don't let them deny it, it's right there in the holy books[​IMG]
   
 15. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi nadhani hoja hapa sio kwamba posho ni ndogo au kubwa. Hoja ni je ni halali wabunge kulipwa posho ya kuingia ofisini kwao ambako ni bungeni na kulipwa posho kwa " kukaa" ofisini kwao? Ni sawa sawa na Meneja na Wakurugenzi wa Kampuni kwenda kwenye Management Meeting na kutaka walipwe posho wakati mikutano kama hiyo iko katika Hadidu za Rejea ( Terms of Service) za ajira yao. Nini kazi ya wabunge kama sio kukaa bungeni na kufanya tulichowatuma na kupokea ujira. Kwa nini Posho?
   
 16. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ili muendelee kuwa vipofu? tunauliza hapa ili na nyie mtuke tongo za macho. Nisalimie Makorora kwa wadekaji.
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Yaani wewe lol! Tafuta yenye Kiti moto labda
   
 18. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Namjua siku nyingi sana Dr Kitila Mkumbo, na nilikuwa namuweka kwenye kundi la watu makini lakini niliposoma kwa makini maelezo ya SOKOMOKO, na nikiangalia ule mchakato wa kuwapata wabunge wa viti maalum kweli Dr Kitila Mkumbo dhambi ya dhulma itakutafuna mpaka mwisho umekwenda kujaza Wachagga na wanawake wa kiongozi na wana ndungu, kina mama makini wote mmewatosa
   
 19. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu mimibaba Hata yeye anasisitiza watu wafanye kazi kitaalam au ndio yale ya fuata mafundisho yangu usifuate matendo yangu? hili la Joyce Mukya alitumia utaalam gani kama alivyotueleza mkuu carefree? Ifike wakati tujue mission and vision ya kila chama ifike mahali tusishabikie vyama tuangalie watu wenye utashi wa kukataa kila ovu kwa vitendo na anae walk on his/her words! ndio maana nina amini kupitia mgombea binafsi ambae anawajibika moja kwa moja kwa wapiga kura wake sio kupitia vyama. Maelekezo ya mchague huyu na yule awe viti maalum ni ubakaji wa demokrasia kwenye chama cha kidemokrasia tena na maendeleo! mbaya zaidi anaefanya hivyo ni mwaume what do you smell hapo? Tunaposisitiza maadili kwa wanafunzi wetu na sie tujiamgalie maadili yetu!
   
 20. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Maumivu ya kichwa huanza poole pole!

  If symptom persist seek medical advise.
   
Loading...