Dokezo: Mtanzania kufungwa maisha London kwa ugaidi

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
Nimeipata sasa hivi wakati nikijiandaa kwenda kupata kabisa kangu pale Gidamez Pub, nje kidogo ya mji wa Lusaka kwamba yupo Mtanzania amepatikana na hatia na atafungwa maisha huko Uingereza. Eti alikuwa na chuo cha kufunza magaidi ndani ya London. Makubwa! Picha yake nitaipata kesho. Leo soma hii habari nimeiattach hapa.
 
Attachments

  • Tanzanian for life sentense in London for terrorism.doc
    21.5 KB · Views: 132
Nimeipata sasa hivi wakati nikijiandaa kwenda kupata kabisa kangu pale Gidamez Pub, nje kidogo ya mji wa Lusaka kwamba yupo Mtanzania amepatikana na hatia na atafungwa maisha huko Uingereza. Eti alikuwa na chuo cha kufunza magaidi ndani ya London. Makubwa! Picha yake nitaipata kesho. Leo soma hii habari nimeiattach hapa.

Hivi hii nayo ni siasa? au ndio hivyo tena JF sio forums bali ni forum?
 
Hivi hii nayo ni siasa? au ndio hivyo tena JF sio forums bali ni forum?

Mwafrika ni siasa maana tayari kuna hate ambayo matokeo ama imezaliwa na siasa.Kutoka Tanzania ukafanya siasa za aina Nchi za watu ni siasa according to me.Now Huyu jamaa si Mtanzania mie nasema ni Mhindi maana hata hapo alipo naamini hakuwa na PP ya Tanzania .
 
Hivi ugaidi (uliopelekea huyo Mtz kufungwa) na uraia (Utanzania wa huyo Mwalimu wa magaidi) sio SIASA?I mean terrorism and citizenship sio part and parcel of politics?Nifafanue kidogo:Wakati Bush na neocons wenzake wanawaita Hizbollah na Hamas kuwa ni magaidi,wafuasi wa makundi hayo wanawachukulia kuwa ni freedom fighters.War on terror,isnt that politics?Nisahihisheni kama nimekosea.
 
Nimeipata sasa hivi wakati nikijiandaa kwenda kupata kabisa kangu pale Gidamez Pub, nje kidogo ya mji wa Lusaka kwamba yupo Mtanzania amepatikana na hatia na atafungwa maisha huko Uingereza. Eti alikuwa na chuo cha kufunza magaidi ndani ya London. Makubwa! Picha yake nitaipata kesho. Leo soma hii habari nimeiattach hapa.

Hata hivo huyu jamaa alikuja UK akiwa bado "todler" hivo unazi wote kuhusu ugaidi kaupatia UK hasa London ambako alihamia akiwa na umri wa miaka 12.

Hivo nafikiri "thread" hii itafutiwe mahala pengine kama Nyepesi (kama inawezekana) please!
 
Moyo ulikwenda mbio, na pumua ikawa ya haraka haraka!

Ingewezekana vipi "Mtanzania" wetu, mzalendo wa hali ya juu ajihusishe na mambo ya namna hiyo?

Jamani, muwe waangalifu mnapohusisha majina ya watu tunaowaheshimu na habari za majanga kama hizi.

'Mtanzania', natumaini tutakusoma mapema hapa JF kutuondoa wasiwasi!
 
Mimi naona hata hiyo heading ibadilishwe kabisa kwa kuwa huyu sio mtanzania bali ni tanzanian-born na hata maadili ya kitanzania hayajui kabisa. Jitu limezaliwa na familia ya kidosi na kukulia Yorkshire?

"I've got a bomb. I'm going to blow you all up."....You rarely meet Tanzanians producing these kind of statements, they dont exist in our dictionaries!

...."Come Mister Taliban, come bomb England, before the daylight come, you wanna see 10 Downing Street done."....Surely Tanzanians songs have better lyrics than these!
 
Kamanda punguza kutuma new THREADS maana babu umezidi na sasa hata pumzi ya kujadili tunakosa,na nyingi unazopost ukweli hazina maana kabisa,seems kazi yako ni kubandua sehemu na kuja kubandika hapa,nimeangalia page ya kwanza tu una zaidi ya thread 11...slow down!
 
Nimeattach hapa picha ya mtu anayedaiwa kuwa Mtanzania ambaye anangoja hukumu ya maisha huko London, Uingereza kwa kupatikana na hatia ya kufunza na kuandaa mashambulizi ya kigaidi.

attachment.php
 
Attachments

  • Picha ya Himid.jpg
    Picha ya Himid.jpg
    26.5 KB · Views: 171
Kamanda unatuchosha na thread zako za kukocopy na zisizokuwa za siasa. Hebu zitafutie mahala pake
 
Back
Top Bottom