Huyu ni shemeji yangu(mdogo wa mke wangu),alihitimu kidato cha sita na akajiunga na jeshi la kujenga taifa kwa mujibu wa sheria akahitimu mafunzo mwaka jana.
Mwanzonimwa wiki hii alipigia simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mkuu wake wa kikosi alipofanyia mafunzo na akamjulisha kuwa kuna nafasi za kazi za kujiunga na JWTZ lakini zipo katika kambi nyingine(Hapa sitazitaja hizo kambi) na akampa namba ya simu ya mtu aliyeko huko kwenye kambi yenye hizo nafasi.
Baada ya kumpigia,huyo mtu alimwambia kuwa ni kweli na yeye ni miongoni mwa waliobahataika kupata hiyo nafasi na anatakiwa kufika kambini hapo haraka ili kuchukua vifaa vya mafunzo na kuelekea katika mafunzo ambayo tena yatakuwa yanafanyikia kambi nyingine(Kumbuka mpaka hapo zimeshafika kambi tatu ukianzia na pale simu ya mwanzo ilipotoka).
Mashaka yakaanza pale alipomwabia kuwa anatakiwa kwenda na shilingi 350,000/=kwa ajili ya gharama ya vifaa vya mafunzo.
Je,kwa wajuzi wa haya mambo,hapo kuna kazi kweli au ndo jama na wao wantekeleza kauli mbiu ya HAPA KAZI TU?