Dogo Janja: Irene Uwoya ana mvuto, anafaa kuwa mpenzi wangu

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
dogo janja.jpg

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Dogo Janja kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu mahusiano yake, na kutoa sintofahamu kuhusu kutoka kimapenzi na muigizaji wa filamu za kibongo Irene Uwoya.

Akizungumza na East Africa Television, Dogo Janja ambaye mara nyingi hapendi kuzungumzia maisha yake binafsi, ameamua kusema kuwa msanii huyo anafaa.

"Irene ni mwanamke mzuri, anavutia, kila mwanaume anayejua mwanamke mzuri anafaa kuwa naye, ila kwa upande wangu mimi namkubali sana Irene Uwoya, kwani anaigiza vizuri, hivyo namkubali kwa kazi zake pia", alisema Dogo Janja.

Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma za Irene Uwoya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Dogo Janja, ambapo watu wengi wamekuwa na mtazamo tofauti wakisema si sahihi kwani Irene Uwoya ni mkubwa sana kwa Dogo Janja. Jambo ambalo Dogo Janja anaonekana kutoliafiki.
 
Alitakiwa kusema "Mama yangu Irene Uwoya ana mvuto ana faa kuwa mpenzi wangu.."
Kama hili la huyu mtoto ni la kweli basi wakupewa lawama ni Madee na kina Babu Tale...huyu mtoto hawamshauri na kumuongoza vyema....huyu atavuna Ukimwi soon kwa mwendo huu...
Kweli wana ruhusu mtoto kuwa na Mama yake tena wa aina hii?
 
Kabisa hawa vijana sijui hawana wazazi na mashangazi. Halafu baadae wanalalamika serikali haiwapi vijana ajira wakati wameshajiajiri kazi za hovyo kwa hawa kina mama. hahaha
 
Alitakiwa kusema "Mama yangu Irene Uwoya ana mvuto ana faa kuwa mpenzi wangu.."
Kama hili la huyu mtoto ni la kweli basi wakupewa lawama ni Madee na kina Babu Tale...huyu mtoto hawamshauri na kumuongoza vyema....huyu atavuna Ukimwi soon kwa mwendo huu...
Kweli wana ruhusu mtoto kuwa na Mama yake tena wa aina hii?
ila uwoya ni kisu kinoma..au sio?
 
Dogo aachane na haya mambo, atafute Dentist kwanza hawa wakinamama watammaliza kabla hajafika miaka 30
 
Alitakiwa kusema "Mama yangu Irene Uwoya ana mvuto ana faa kuwa mpenzi wangu.."
Kama hili la huyu mtoto ni la kweli basi wakupewa lawama ni Madee na kina Babu Tale...huyu mtoto hawamshauri na kumuongoza vyema....huyu atavuna Ukimwi soon kwa mwendo huu...
Kweli wana ruhusu mtoto kuwa na Mama yake tena wa aina hii?
Kwani kamzaa wa mwenzio mkubwa mwenzako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom