Dogo janja aacha shule,afukuzwa na Madeee na kurudishwa kwao Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dogo janja aacha shule,afukuzwa na Madeee na kurudishwa kwao Arusha

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Yo Yo, Jun 14, 2012.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  .
  Rapper mdogo kutoka A town Dogo Janja aliekua akisoma na kuishi Dar es salaam amerudishwa kwa wazazi wake Arusha jana kutokana na kufanya mambo mbalimbali ambayo uongozi wa Tiptop Connection haujapendezwa nayo.
  Tip Top ambao walikua wanasimamia kazi za muziki za Janja wamempandisha basi na kumrudisha kwao jana baada ya kuona msanii huyo hazingatii shule kama inavyotakiwa, amekua mtoro wa mara kwa mara katika shule aliyokua akisoma ya Makongo na hasikii anaporekebishwa, hiyo ndio sababu kubwa ya kumrudisha ili kukwepa lawama za baadae ambazo zingetokana na Dogo Janja kutosimamiwa vizuri kwenye swala la Elimu kwa sababu Tiptop ndio waliokabidhiwa kumsimamia.
  Stori kamili ya hii ishu utaipata baadae baada ya kuzungumza na Meneja wake ambae ni Madee.
  [​IMG]
  Alichokiandika Dogo Janja kwenye Facebook jana.

  thanks.....http://millardayo.com/
   
 2. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Wakati mwingi Dogo Janja alikua akiongea na simu kuwaaga watu huku akiwa na furaha ya kuondoka Dar es salaam alikoishi kwa tabu, anafurahi kurudi nyumbani Arusha.

  [​IMG].

  [​IMG]Dogo Janja akiagana na kaka yake mwenye T shirt ya bluu yenye mistari.

  [​IMG].

  [​IMG].

  [​IMG].

  [​IMG].

  [​IMG]Bye bye.

  [​IMG].

  Jana kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM Msanii Madee wa Tip Top Connection ambae ndio alikabidhiwa na wazazi kumlea na kumsimamia Dogo Janja aliamplfy kuhusu sababu za kumrudisha Dogo Janja mikononi mwa wazazi wake baada ya kudai kumshindwa.
  Madee kasema "Dogo Janja aliekua form II Makongo High School kakataa kusoma kwa hiyo mimi siwezi kukaa nae wakati hataki kusoma, nilikua safarini Iringa na Mbeya ambapo baada ya kurudi mwalimu wake wa darasa alinipigia simu na kunipa pole kwa sababu Dogo Janja anaumwa, nikashtuka ikabidi nimpigie nikawa simpati kwenye simu.. nikaenda nyumbani kwa Tunda Man alipokuepo na alipojua nimekuja akajificha alikua anataka kunikimbia nikampiga sana vibao, kweli nilimpiga ambapo kesho yake baada ya kuamka nikamuuliza unataka kusoma au kuzurura mtaani? akajibu kwamba anataka kwenda kusoma Arusha ikabidi nimpigie baba yake palepale ambapo mzee wake alniomba nisimrudishe Arusha niendelee kukaa nae"
  Madee ameendelea kusema kwamba "nilimwacha nyumbani baada ya kuchukua simu yake ambapo nilikuta vitu vingi sana vya kishenzi shenzi kaviandika na ninavyo mpaka leo kwa ajili ya ushahidi, vimeniumiza hasa kwa mtu kama mimi ambae najua nimemtoa wapi, kaandika kuhusu uchafu mbaya na kingine kinanihusu mimi ambacho hapaswi kusema kwa mtu kama yeye, baada ya hapo msimamo wake ulikua vilevile kwamba anataka kurudi kwenda kusoma Arusha, jioni tukakaa kikao juzi na kaka yake na watu wengine na mimi nikampa baraka zote"
  Kwenye sentensi nyingine Madee amesema "kwa wiki iliyopita na wiki hii Dogo Janja alitoroka kwenda shule kwa siku tatu na hii ni mara ya pili ambapo mara ya kwanza nilimpeleka shule na kumchapa mbele ya wanafunzi wenzake, yani nilivyompeleka shule wanafunzi wenzake mpaka walikua wanamshangaa, alisingizia vitu vingi vya uongo alikua ananidanganya mimi nyumbani na siku hiyo ndio nilimkuta Ubungo Plaza alikua anaogelea na rafiki yake, walimu wake waliniambia hawajamuona shule kwa muda wa wiki moja"
   
 3. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ngoja tusikie upande wa pili wa story kabla ya kucomment.
   
 4. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Hapa ni conflict of interest..
  Story ingenoga kama na dogo nae angefunguka.. Kifupi hawaja balance story..
   
 5. M

  Mbundenali Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 9, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Walugulu tunasema mlongayeka kahuma. Yaani katika kesi mtu akiongea peke yake lazima ashinde. Kwa hiyo ngoja tumsikie dogo naye
   
 6. A

  Annabel New Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  go back to school we mtoto....
   
 7. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  ndio nani hawa?
   
 8. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Calculated movie ili kumpandisha chart
   
 9. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  ndio kwanza namuona huyu mtoto, kaimba mwimbo gani kwani?
   
 10. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Dogo Janja: Show ya
  milioni, Madee alinipa laki
  moja
  Siku moja baada ya Dogo
  Janja kudaiwa kufukuzwa
  Tip Top Connection, ukweli
  halisi kuhusiana na uamuzi
  huo umewekwa wazi na
  yeye mwenyewe.
  Sababu zilizotajwa na Tip
  Top Connection ni kwamba
  Dogo Janja alilewa sifa na
  kuwa mtoro shuleni.
  Kwa mujibu wa interview
  (ya pili kufanyiwa baada ya
  kipindi cha Amplifaya cha
  jana) tuliyofanya naye kwa
  simu saa moja asubuhi leo
  (June 14) akiwa stand
  kurejea nyumbani, uonevu
  na dhuluma ndivyo
  vilivyomchosha kuishi Dar
  es Salaam.
  Anasema tangu aje Dar es
  Salaam hajawahi
  kusaidiwa chochote na
  Madee zaidi ya mambo ya
  muziki pekee huku kula,
  malazi na ada ya shule
  vikifanywa na rafiki yake
  Madee aitwaye Abdallah
  Doka ambaye (Dogo Janja)
  alikuwa akiishi kwake.
  Anasema kutokana na
  ngoma zake kujipatia
  umaarufu alikuwa akipata
  show nyingi nchini na zote
  alikuwa halipwi chini ya
  milioni moja.
  Kilichokuwa kinamsikitisha
  anasema ni kulipwa hela
  kidogo isiyozidi laki mbili
  na hivyo kumfanya aishi
  kwa tabu licha ya kuingiza
  hela nyingi za show.
  “Nilikuwa navumilia tu bro
  kwasababu kila
  nilipolalamika kuhusu
  mambo ya hela Madee
  alikuwa mkali sana,”
  ameongea uchungu.
  Dogo anasema ilikuwa
  inafikia wakati akifanya
  show za ukumbuni
  hulipwa elfu hamsini au
  chini ya hapo na wakati
  mwingine alikuwa halipwi
  kabisa.
  Tamaa ilizidi kumwingia
  Madee kiasi cha
  kumnyang’anya kadi yake
  ya benki na kuanza
  kuchukua hela bila kujua
  password aliipata wapi.
  “Kuna wakati nilikuwa
  nataka kumtumia mama
  laki moja, Madee
  akanikataza eti kwakuwa
  watadhani nina hela sana,”
  anasema.
  Mpaka tunaongea naye
  asubuhi hii, anasema kadi
  yake imebakiwa na shilingi
  25,000 tu.
  Ameendelea kudai kuwa
  juzi Madee alimpigia simu
  na kumwambia kuwa kaka
  yake wa Kibaha ameandaa
  show ya CCM na atamlipa
  shilingi laki moja.
  “Hivi kweli bro mimi ni
  mtu wa kufanya show ya
  laki moja?”. Hata hivyo
  aliamua kukubali ili
  kuepusha lawama.
  Baada ya show kumalizika
  anasema yeye na back up
  artist wake walirudishwa
  saa saba usiku wakati
  asubuhi yake alitakiwa
  kwenda shuleni kuchukua
  namba ya mtihani na
  kuandaa dawati la kukalia.
  Dogo Janja anaeleza kuwa
  inamuuma sana kwakuwa
  muziki haujampa chochote
  licha ya Madee ambaye
  huwa hapati hata show
  kumtumia kimaslahi na
  hadi leo hii anamalizia
  kujenga nyumba yake.
  “Ni kama vile Madee
  alinipanda ili anivune.”
  Ameendelea kusema kuwa
  hiyo juzi sasa hadi kufikia
  Tip Top watangaze
  kumfukuza alikuwa kwa
  Tundaman akipiga story na
  Madee akamuita kisha
  kuanza kumpiga.
  Alichukua simu yake
  akaondoka nayo. “Jamaa
  alianza kujitumia meseji
  kutoka kwenye simu
  yangu kwenda kwake za
  matusi ama kuwa nataka
  kumroga. Jana
  nimemuonesha Milard hizo
  meseji na amesikitika
  sana.”
  Anasema simu yake
  alipewa jana.
  Kitendo cha kumwambia
  Madee kuwa amechoka na
  anataka kurudi nyumbani
  ndicho kimemfanya
  amfanyie yote hayo hadi
  kumwambia kuwa
  watahakikisha
  wanambania asifanye
  vizuri tena kwenye muziki.
  Pia amedai kuwa Madee
  aliwapigia simu wazazi
  wake ili wamkataze Dogo
  Janja asifanye interview na
  vyombo vya habari.
  “Wanajua nikiongea
  wataabika sana.” http://
  leotainment.blogspot.com/2012/06/
  dogo-janja-show-ya-
  milioni-madee.html?m=1
   
 11. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Huyu mtoto namfananisha na Justin Bieber, nadhani wanalingana kiumri, sasa hivi Bieber ni Milionea kama sio Bilionea kwa sababu ya muziki tu, hapo ndipo unapojiuliza Hivi sisi Waafrika nani katuroga??!!!... eeeeshh
   
 12. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  urithi wao kutoka chama cha machangu ni ufisadi! ss hata huyo mtoto unamdhulumu ili iweje?? nways ili maandiko yatimie kuwa samaki mkubwa, humla mdogo, amen!
   
 13. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Du! kazi ipo sasa sijui nani mkweli
   
 14. A

  Angel Aore New Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njia ya mwongo ni fupi, km Madee alikuwa anamdhulumu dogo mambo yatakuwa hadharani, muda c mrefu. Dogo karibu nyumbani.
   
 15. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 378
  Trophy Points: 180
  Kweli mziki bongo haulipi,dogo alivyojuu kiasi icho ana 25000 tu kwenye account yake?whats going on Tip top?kumbe huku kwenye makundi nako kuna wahindi(wanyonyaji)?kabla ya wasanii kuanza kupambana na wanyonyaji wanaowaita wahindi,wajiangalie kwanza wenyewe km wanatendeana haki?keisha alikimbia tip top,saiv dogo janja kaondoka...kuna haja ya tip top kuji-evaluate upya na kujisafisha mbele ya jamii.
   
 16. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Kuhukumu dhambi lakini kwa niwajuavyo Tip Top na hasa Madee inasikitisha hasa kwa mtoto kama huyu.Dogo Janja rudi shule focus sana na elimu lakini usikitupe kipaji chako.andika mashairi,ingia mkataba na Maproducer kutengeneza ngoma zako mkatane kwenye mapato lakini this tyme ingia mkataba rasmi na uwe mkataba wa muda mfupi mfupi ili ukishindwa huongezi mkataba.pole sana dogo kua uyaone!
   
 17. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Alijiita dongo janja, amekutana na kubwa janja. Ila, kama kweli, madee, si mpango. Dogo bado mdogo.
   
 18. Mizizi

  Mizizi JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,266
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tutadis matukio yote ya Tip Top ili kuonyesha kukataa kwetu kwa dhulma kwa wasanii watoto!!
   
 19. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,528
  Likes Received: 10,441
  Trophy Points: 280
  dogo janja shoo zote zile anarudi na akaunti inayosoma 25000 duh.!
   
 20. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Amevuna alichopanda!
   
Loading...