Uchaguzi 2020 Dodoma: Yaliyojiri mapokezi ya Tundu Lissu na mkutano mkubwa viwanja vya Uhuru Dodoma

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225


WanaJF

Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu leo anatarajiwa kuzindua kampeni katika Kanda ya Kati mkoani Dodoma.

Rais huyo mtarajiwa wa Tanzania ataambatana na mgombea Mwenza Salum Mwalimu, Katibu Mkuu John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu

Tayari Kuna pilikapilika kubwa hapa jijini Dodoma kuhusu ujio wake na maandamano makubwa ya kumpokea na Mkutano wake katika Uwanja wa Uhuru unatarajiwa kuvunja Rekodi kwa wingi wa watu

Lissu ambaye Watanzania wamembatiza jina la 'Charismatic Leader' amekuwa akilakiwa na Maelfu kwa Malaki ya watu popote anakopita ikiashiria kuzoa wingi wa kura katika uchaguzi mkuu wa October 28

Tutaendelea kuwapa taarifa kwa kila kitakachoendelea

Aliyosema Mgombea Urais..

"Dodoma fikirieni 2017 watoto waliofukuzwa Chuo usiku, wanafunzi wa UDOM,wengine hawakuwa na mahali pa kwenda wakiwa kwa maelfu walipelekewa FFU usiku, Rais @MagufuliJP anasimama anasema hawatakiwi kuwa chuoni sababu ni vilaza, alisema hakusema?" Mhe @TunduALissu

"Wenye viwanda, watu wanaotegemewa kutengeneza ajira kwa ajili yetu, wamefilisiwa mali zao, wengine wamepatwa na presha wamekufa, nani wa kuwasemea hawa? " Mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya @ChademaTz Mhe @TunduALissu

---------------------------------------------------

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Lissu amesikia vilio vya Wafanyakazi kote nchini.

Akihutubia maelfu kwa maelfu ya watu kwenye Mkutano wa Kampeni katika Uwanja wa Uhuru jijini Dodoma Lissu amelaani vikali Sheria ya kuondoa Fao la Kujitoa kwa Wafanyakazi Nchini wanaoacha kazi kabla ya umri wa kustaafu.

Katika sheria Kandamizi kwa Wafanyakazi iliyotungwa na Serikali ya CCM na kupitishwa na wingi wa wabunge wa CCM kwa Sasa mtu yeyote anayeacha kazi kabla hahafikisha umri wa kustaafu hatalipwa chochote katika stahili za Mafao yake mpaka atimize miaka 60 hata Kama ameacha kazi akiwa na miaka 30

Lissu amesema hiyo Sheria ni ya kipuuzi na kikandamizaji na akasema Mara tu atakapoapishwa baada ya kuchaguliwa ataifuta Mara moja sheria hiyo na kurejesha Fao la Kujitoa.

Wafanyakazi wengi wamefurahishwa na ahadi hii na kusema itakuwa ni ajabu kwa mtu aliyeajiriwa kuacha kumpigia kura Lissu huku akifahamu wazi kuipigia kura CCM na kutafuta umasikini na kifo chake atakapoacha kazi au kufukuzwa kazi kabla ya umri wa kustaafu.
IMG-20200904-WA0042.jpg
IMG-20200904-WA0044.jpg
IMG-20200904-WA0032.jpg
IMG-20200904-WA0031.jpg
IMG-20200904-WA0037.jpg
IMG-20200904-WA0039.jpg
IMG-20200904-WA0025.jpg
IMG-20200904-WA0055.jpg
IMG-20200904-WA0054.jpg
IMG-20200904-WA0053.jpg
IMG-20200904-WA0034.jpg
IMG-20200904-WA0035.jpg
 
Chadema ndo chama pekee Tanzania chenye Sera ambazo zimelenga kuivusha Tanzania na mtu pekee mwenye uwezo kuongoza Tanzania mpya ni Lissu pekee yake kuna mwingine anajigamba anapambana na ufisadi wakati yeye amejenga uwanja wa ndege wa Kimataifa nyumbani kwake mpaka mbuga ya wanyama amehamishia nyumbani yake ni ulevi wa madaraka #NIYEYE
 
Back
Top Bottom