Dodoma: Waziri Mkuu awataka vijana kuchangamkia fursa za kiuchumi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1633356832379.png

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa rai kwa Vijana kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo kupitia sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Maliasili, Utalii, Ujenzi, Uchukuzi, Mawasiliano, Nishati, Madini, Viwanda na Biashara.

Amesema hayo leo akiwa katika Kongamano la Tano la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Jijini Dodoma na kuongeza, "Haya maeneo niliyotaja yanapatikana kwa urahisi Nchini".

Pia ametoa wito kwa Wadau wa Maendeleo hususan Asasi za Kiraia kuongeza jitihada katika kuwezesha Wananchi Kiuchumi ili kuongezea chachu ya kushiriki shughuli za Uchumi.
 
Tukichangamkia kwenye YouTube na tukiandika heading za kuvutia wanatufyeka.

Kwa kutaja MP kua kafanya nanii ilikuwa kosa
 
fulsa zipo vijana ,tafuta angalau nauli kidogo ikufikishe pwani ,kilimo cha mikoko kinalipa ,ukijitahidi walau uwe na ekali mia~
 
Ili mtupige ety mtupangishe barabarani na yutyubu chaneli zetu
 
Hivi Mzee Ali Hassan Mwinyi alisema nini ile siku pale Diamond Jubilee hadi yule mwamba akamfuata na kumtandika ngumi?!
 
Back
Top Bottom