Dodoma: Waziri Mkuu asema Mikoa 18 imeathiriwa na mvua

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali, mbali na kusababisha vifo, imeathiri barabara 73 na madaraja kwenye mikoa 18 nchini.

Pics%20pg%202%20Feb%2008.jpg

Picha: Baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na mvua nchini.

Amesema reli ya Tanga hadi Arusha, na Dar es Salaam hadi Mwanza na Kigoma kwa nyakati tofauti nayo ilifungwa kwa muda kutokana na uharibifu wa mvua.

Akizungumza jana bungeni Jijini Dodoma wakati wa kuahirisha Bunge, Majaliwa alisema mvua hiyo iliyoanza Oktoba mwaka jana ikitarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu, imesababisha vifo kwa watu waishio maeneo ya mabondeni, uharibifu wa nyumba, miundombinu ya usafirishaji ikiwamo ya barabara, reli na madaraja.

"Jumla ya barabara 73 na madaraja katika mikoa 18 ziliathirika. Pia, reli za Tanga hadi Arusha na Dar es Salaam hadi Mwanza na Kigoma kwa nyakati tofauti nazo zililazimika kufungwa kwa muda.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha kuwa huduma za usafiri na usafirishaji kwa njia ya barabara na reli katika maeneo yaliyoathirika zinarejea haraka," alisema.

Waziri Mkuu alisema serikali inafuatilia kwa karibu taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ili kuwafahamisha wananchi mwenendo wa hali ya hewa na kutoa tahadhari kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii.

Katika hotuba yake, Waziri Mkuu aliwataka wananchi kutumia fursa hiyo kuchukua tahadhari kwa kuhama sehemu za mabondeni na kuzingatia taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na TMA.

Majaliwa aliahirisha Bunge hadi Machi 31 mwaka huu litakaporejea tena kwa ajili ya kuendelea na mkutano wa Bunge la Bajeti, ambao utakuwa wa mwisho kwa Bunge la 11.

Chanzo: IPP Media
 
Back
Top Bottom