Dodoma: Wanafunzi 47 wapewa ujauzito kuanzia Desemba 2019 hadi Januari mwaka huu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Wanafunzi wa kike 47 katika shule mbalimbali za sekondari katika wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wameachishwa masomo kwa kupata ujauzito kwa kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka jana.

Kauli hiyo ilitolewa na Ofisa Elimu Sekondari Wilaya ya Mpwapwa, Nelson Milanzi wakati akizungumza na gazeti hili ofisi kwake mwishoni mwa wiki.

Milanzi alisema suala la mimba shuleni linawaumiza vichwa viongozi na wazazi kwani linakwamisha watoto wa kike katika kufikia ndoto za maisha yao.

“Tunapozungumzia suala la mimba shuleni ili kulikomesha, tunahitaji ushirikiano wa hali ya juu kuanzia jamii, vyombo vya kutoa uamuzi hadi viongozi wenye dhamana mbalimbali katika serikali.

“Kushuka kwa maadili katika jamii ndicho chanzo kikuu cha wanafunzi kupata mimba katika umri mdogo ambako kunasababishwa na watu wakubwa wanaoshirikiana nao, wakati mwingine wazazi na jamii inaona wanaingia nyumba ya wageni lakini hawachukui hatua wala kutoa taarifa,”alisema.

Uchunguzi uliyofanywa na gazeti hili baada ya kuzungumza na baadhi ya wanafunzi waliopata ujauzito (majina yamehifadhiwa) walisema, kuna baadhi ya viongozi wa dini, vijana wa bodaboda na watumishi wa serikali wamekuwa wakiwarubuni kwa kuwaaahidi vitu vingi zikiwemo zawadi kama simu na nguo.

“Wengi wanaopata mimba huamua kuzitoa ili kupoteza ushahidi, mimi siwezi kata kata kutoa mimba, siwezi kuua kwa kumtunzia siri mtu bora nipambane na hali yangu,” alisema msichana mmoja.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri alikaririwa akisema hana uvumilivu kwa mtu yeyote anayejihusisha kimapenzi na mwanafunzi na kwa mujibu wa sheria kifungu na 130 (1) e na 131(1) (2) ya kanuni ya adhabu namba 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 inamtia hatiani mtu yeyote anayefanya mapenzi na mtu mwenye umri chini ya miaka 18 kwa kupewa kifungo cha miaka 30 jela.

“Ukiona mtu anampa mwanafunzi mimba, utambue kuwa huyo mtu alifanya ngono zembe ambayo inamsababisha kujiingiza katika hatari ya kuambukizwa Ukimwi na magonjwa ya zinaa,”amesema.

Shekimweri alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wote kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kuhusu gesti bubu ambazo zimekuwa maficho ya wanafunzi kupatia mimba. Pia aliitaka jamii kutoa taarifa za mtu yeyote anayejihusisha kimapenzi na mwanafunzi ili kuchukua hatua za kisheria stahiki.

CHANZO: HabariLeo
 
... hiyo ni wilaya moja tu - Mpwapwa tena ndani ya mwaka mmoja! Mwaka 2012 kabla ya uwepo wa Mkoa wa Songwe, nchi ilikuwa na wilaya 169. Well, pengine Mpwapwa inaweza kuwa worst case kwa suala la mimba kwa wanafunzi; so let's assume kwa kipindi hicho wastani ilikuwa 30. Kwa wilaya hizo 169 kulikuwa na mimba 169 x 30 = 5,070 kwa mwaka. Duh! Huu ni umati mkubwa sana kukosa elimu! Tunazalisha wajinga wengi sana kwa mtindo huu!
 
kuna shida pahala nje na ugoigoi wa malezi.

hivi uwepo wa wageni wengi kwenye baadhi ya maeneo ya shule/makazi ya wanafunzi haliwezi kuwa tatizo pia? nasemea upanukaji wa miji, majiji, vituo vya usafirishaji, vituo vya starehe na teknolojia (kutajwa simu kama kishawishi liangaliwe)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
na hawa ni sampuli iliyojulikana. achilia waliofanikiwa kuharibu mimba, waliokimbia shule kama utoro wa kawaida, idadi yao yaweza kuzidi hizi takwimu rasmi.

vita hii si ya mmoja wa serikali pekee.
... hiyo ni wilaya moja tu - Mpwapwa tena ndani ya mwaka mmoja! Mwaka 2012 kabla ya uwepo wa Mkoa wa Songwe, nchi ilikuwa na wilaya 169. Well, pengine Mpwapwa inaweza kuwa worst case kwa suala la mimba kwa wanafunzi; so let's assume kwa kipindi hicho wastani ilikuwa 30. Kwa wilaya hizo 169 kulikuwa na mimba 169 x 30 = 5,070 kwa mwaka. Duh! Huu ni umati mkubwa sana kukosa elimu! Tunazalisha wajinga wengi sana kwa mtindo huu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maadili na malezi ni shida sana, na hii yakuruhusiwa kusoma na watoto mmm, binti anazalishwa na boss mwenye nazo anakuja shule huku mkwanja mzito Mwl unakula mhongo wa kuchemsha shuleni, binti anatunzwa na mzazi mwenzie, heshima hakuna kabisa, labda aweke sheria madhubuti

Nionavyo tatizo haianzii kule juu inaanzia kwenye jamii. Tunaendekeza umwari. Rais aliwakanya takukuru kukomalia rushwa ya ngono vyuoni ni kupoteza muda. Jana nimeona hoo utafiti ya rushwa ya ngono Magufuli stand. Taifa linalohusudu ngino linadai linapigana na tatizo hili. Turudi kwenye jamii vigodiro
 
Ndiyo hayo malezi yanaanzia huku chini kabisa, huwezi mkanya mtoto mwenye umri mkubwa bila kuanza akiwa mdogo kabisa, sie tumelelewa mama akikukata jicho tu unaelewa tu hapa siruhusiwi kabisa, siku hizi kitoto kinakuaibisha mzazi na mgeni

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom