Dodoma: Upinzani wampeleka Spika Ndugai Mahakamani

Lissu anatafuta kiki,kuficha maovu yake ya ACACIA mining yaliofeli.
Huko bungeni hajamaliza ngazi za kuomba marejeo anakimbilia mahakamani.
Bahati mbaya mahakama,imefungwa mikono kwa kujadili kinachoamuliwa na bunge,hiyo kesi imeshaanguka kabla hata ya kufunguliwa.
Ni kama Jamaa Pale Magogoni anatafuta kwa issue ya IPTL ambayo ya ACASHIA hajamalizana nayo
 
Wakimfuatisha Lissu nao watakuwa hawaelewi sasa hivi. Bungeni na mahakama wapi na wapi? Mbona wao wakitukana bungeni hawafikishwi mahakamani!! Wamesahau Kinga na madaraka ya Bunge? Au hawajui maana ya Separation of power? Ni upuuzi tu wanaoufanya.
 
Tuwekee basi hapa
Hii hapa: cc Ghosryder

Spika wa bunge la JMT kapewa mamlaka na Katiba ya JMT, na mamlaka hayo kupanuliwa au/na kufafanuliwa zaidi na Kanuni za Kudumu za Bunge (Kanuni). Mamlaka hayo yanalindwa pia na Katiba na Kanuni. Spika wa Bunge la JMT anayo mamlaka katika bunge ambalo yeye ndiye kiongozi wake, ambayo yamegawanyika katika sehemu maalum mbili, Mamlaka ya lazima na mamlaka ya hiyari (mandatory and discretionary powers).
spika wa bunge anatekeleza majukumu yake kwa mamlaka aliyopewa kisheria. Kanuni za kudumu za bunge (2016), kanuni ya 67 (1) na (2) zinampa mamlaka spika kukataza majadiliano na anaweza kumkataza mbunge yeyote kuzungumza. Kanuni hizi zinasomeka hivi:

67.-(1) Spika anaweza kulihutubia Bunge wakati wowote na kwa

ajili hiyo, anaweza kumkatiza Mbunge yeyote anayezungumza.

(2) Endapo Spika atasimama wakati wa mjadala, na kuanza

kuzungumza, Mbunge yeyote ambaye atakuwa anazungumza

wakati huo au ambaye atakuwa amesimama mahali pake akisubiri

kuanza kuzungumza, ataketi mahali pake, na Bunge litabaki kimya

ili Spika aweze kutoa maelekezo au taarifa yake.

Kanuni ya 68 inatoa taratibu mbalimbali na taratibu mbalimbali. Kanuni za 68 (4) na (5) zinasomeka hivi:

4) Spika anaweza, ama papo hapo kutoa uamuzi wake juu

ya jambo la utaratibu lililotajwa au kuahirisha uamuzi ili alifikirie

zaidi jambo hilo na kutoa uamuzi baadaye au kutoa uamuzi na

baadaye kutoa sababu za uamuzi huo, vyovyote atakavyoamua.

(5) Katika kufikia uamuzi wake, Spika anaweza kuitaka Kamati

ya Kudumu ya Kanuni za Bunge au Kamati nyingine yoyote ya Bunge

impe ushauri kuhusu jambo husika.

Mbali na hayo, spika amepewa majukumu na mamlaka ya kudhibiti fujo na kusimamia utaratibu bungeni. Kanuni namba 72 (1), (2) na (4) zinasomeka namna hii:

72.-(1) Spika atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa, utaratibu

bora unafuatwa Bungeni, na uamuzi wa Spika kuhusu jambo lolote

la utaratibu utakuwa ni wa mwisho.

(2) Mbunge atakayekiuka utaratibu uliowekwa na Kanuni

hizi anaweza papo hapo kutakiwa na Spika afuate utaratibu na

vilevile Mbunge mwingine yeyote anaweza kusimama na

kumfahamisha Spika kuhusu ukiukwaji wa utaratibu huo na katika

kufanya hivyo, atalazimika kutaja Kanuni ya Bunge iliyoweka

utaratibu uliokiukwa.

(4) Endapo Mbunge atafanya kosa ambalo alikwishawahi

kuadhibiwa kwa mujibu wa fasili ya (2) na (3) ya Kanuni hii, Spika

atalipeleka suala lake kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka

ya Bunge kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 71 ya Kanuni hizi ili

Kamati hiyo ilishauri Bunge kuhusu hatua za kinidhamu zinazostahili

kuchukuliwa dhidi ya Mbunge huyo.
Kanuni ya 68 (10) inampa spika kuwa na kauli na uamuzi wa mwisho. Kanuni hii inasema:

(10) Uamuzi wa Spika kuhusu suala lolote la utaratibu utakuwa

ni wa mwisho.


Kwa sababu bunge ni chombo chenye mamlaka yake na utaratibu wake, adhabu zimewekwa kisheria kwa yeyote anaekiua utaraitibu na utaratibu wa utekelezaji wake umewekwa. Utaratibu huu upo katika kanuni ya 73. Kanuni za 73 (1) na (2) sinasomeka:

73.-(1) Mbunge au Waziri atakayezungumzia jambo au mambo

ambayo hayaruhusiwi na Kanuni hizi, anaweza kuamriwa na Spika

au Naibu Spika au Mwenyekiti akatishe hotuba yake na kukaa mahali

pake.

(2) Endapo Mbunge au Waziri atatumia maneno au lugha

isiyotakiwa Bungeni, yaani lugha ya matusi, usafihi, uchokozi au

lugha ya maudhi na akitakiwa na Spika ajirekebishe kwa kufuta

maneno au lugha hiyo atakataa kufanya hivyo, Spika anaweza

kumwamuru Mbunge huyo atoke mara moja nje ya Ukumbi wa

Bunge na abaki huko nje kwa muda wote uliosalia wa kikao cha

siku hiyo.

Bunge nalo limepewa mamlaka ya kutoa adhabu kufuatia ukiukwaji wa taratibu au utovu wa nidhamu. Kanuni namba 74 (1), (2) na (3)(b) zinahusika. Hizi zinasomeka kama ifuatavyo:

74.-(1) Spika anaweza kutaja jina la Mbunge kwamba amedharau

Mamlaka ya Spika na kisha kupeleka jina hilo kwenye Kamati ya

Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ikiwa:-

(a) kwa maneno au vitendo, Mbunge huyo

anaonesha dharau kwa mamlaka ya Spika; au

(b) Mbunge huyo atafanya kitendo chochote cha

makusudi cha kudharau Shughuli ya Bunge au

Mbunge yeyote anayeongoza shughuli hiyo.

(2) Ikiwa maneno au vitendo vya Mbunge vilivyoainishwa

katika fasili ya (1) ya Kanuni hii vimetokea wakati Bunge likiwa katika

Kamati ya Bunge Zima, basi Mwenyekiti atasimamisha shughuli za

Kamati na ataagiza Bunge kurudia ili kumpatia Spika fursa ya kutoa

taarifa kwa Bunge kuhusu mwenendo wa Mbunge huyo na

kuwasilisha suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka

ya Bunge.

(3) Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge itajadili

suala hilo na ikithibitika kuwa Mbunge husika ametenda kosa

inaweza kushauri kwamba:-

(a) ikiwa ni kosa lake la kwanza Mbunge huyo

asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi kumi; au

(b) ikiwa ni kosa lake la pili au zaidi Mbunge huyo

asihudhurie vikao vya Bunge visivyozidi ishirini;

Mbali na hayo yote, Bunge limejiwekea miiko yake lenyewe. Bungeni kuna mambo ambayo hayaruhusiwi, miongoni mwa hayo ni yale yaliyomo katika kanuni ya 64 (1)(e), (f) na (g). kanuni hizo ni kama ilivyoainishwa hapa:

64.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda

na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge,

Mbunge:-

(a)

(d)

(e) hatazungumzia mwenendo wa Rais, Spika, Mbunge, Jaji, Hakimu au mtu mwingine yeyote anayeshughulikia utoaji wa haki, isipokuwa tu kama kumetolewa hoja mahususi kuhusu jambo husika;

(f) hatamsema vibaya au kutoa lugha ya matusi kwa Mbunge au mtu mwingine yeyote;

(g) hatatumia lugha ya kuudhi au inayodhalilisha

watu wengine.

Kwa hiyo basi ni dhairi kwamba spika wa bunge hakuenda kinyume na kanuni yoyote ya bunge kwa kumtoa mbunge Mnyika nje ya ukumbi wa bunge na kutoa adhabu palepale pasipo uwepo wa Mnyika mwenyewe. Pia spika alitumia misingi ya kanuni kuwashtaki Halima Mdee na Esther Bulaya kwenye kamati ya maadili ya bunge, na uamuzi uliotoka ni sahihi.

Spika alikuwa anafanya kazi ya mamlaka ya dola, na alikuwa anafanya maamuzi kulingana na utaratibu. kanuni za buge zimetungwa kwa mamlaka ya katiba, kama bunge lenyewe lilivyo na kiti cha spika kilivyo kwa mujibu wa katiba. Ibara ya 100 ya katiba ya JMT inatoa uhuru wa majadiliano wa shughuli bungeni kwa mujibu wa kanuni na taratibu. Pia kifungu hiki kinatoa zuio kwa mahakama au chombo chochote kuhoji yaliyotokea bungini wakati bunge lipo katika kazi yake. Ibara hii inasimeka ifuatavyo:

100. Uhuru wa majadiliano na utaratibu wa shughuli Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 14

(1) Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge, na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama au mahali penginepo nje ya Bunge.

(2) Bila ya kuathiri Katiba hii au masharti ya sheria nyingine yoyote inayohusika, Mbunge yeyote hatashtakiwa au kufunguliwa shauri la madai mahakamani kutokana na jambo lolote alilolisema au kulifanyw ndani ya Bunge au alilolileta Bungeni kwa njia ya maombi, muswada, hoja au vinginevyo.

Kwa vyovyote vile basi Bunge, ikiwa ni pamoja na spika wake, haliko hatarini kupatikana na kosa au kuwa subject to judicial review. Hii ni kwa sababu ya kinga iliyowekewa na katiba. Ikitokwa spika amekuwa so arbitrary hakuna namna ya kufanyia uamuzi wake judicial review au kuhojiwa na mahakama. Kuna mamna wanasheria huwa wanapinga baadhi ya vifungu vya sheria zikiwemo ibara za katiba kwa sababu zinakuwa zinakinzana ka Katiba (unconstitutional). Hata hivyo, hata kwa kutotilia maanani ibara ya 100 ya katiba ambayo mwingine anaweza kusema iko kinyume na katiba kwa kuzuia mamlaka ya mahakama, bado spika hatakuwa subject wa maamuzi au order za mahakama kwa sababu kafuata utaratibu, na kama kuna malalamiko kwamba katumia vibaya madaraka yae labda kwa sababu “Katoa uamuzi wa kukurupuka na uonevu/chuki” bado yuko upande salama.
Hapa chini nimeambatanisha kanuni za kudumu za bunge
 

Attachments

  • Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri.pdf
    305.7 KB · Views: 196
Ndugai yuko sahihi. Kafuata kanuni na kanuni zenyewe zinaruhusu adhabu kama hiyo kutolewa. Bunge linaweza hata kumpiga ban ya kudumu mbunge. vilevile maamuzi ya bunge hayahojiwi wala kujadiliwa na mahakama yoyote ile. Nahisi tundu lisu kawapa huu ushauri. Tundu lissu nilikuwa namuheshimu sana, sasa naanza kumuona ni mwanasheria uchwara.
Ww nani hadi ujifanye mfano bora wa hashima dhidi ya Lissu? Haya, heshima yako haihitajiki na wala haina msaada. Mbwiga fulani tu wa Kolomije, mjiini umeingja kwa Loli la mchanga ukakutana na mabaki ya ccm yanakupatia T-shirt za kijani na kofia za njano, basi unaandika bila kufikiria.

Unamjua TL ww? Unajua ni rais wa wanasheria nchini? Ww ambaye hata jina lako tu umeshindwa kulitaja humu ni nani? Tafadhali.....
 
Always sheria ni usanii na kupoteza muda huku mkiliana timing. Nachukia sana utawala wa kisheria na utawala unaofuata DOMOKRASIA.
Sikushangai kuchukia utawala unaofuata sheria na misingi ya demokrasia sababu we kilaza. Jiangalie alafu ujianalye vizuri uone kama utakuja na conclusion kama you are worth hata kutoa neno watu wakakusikiliza.
 
Ndugai yuko sahihi. Kafuata kanuni na kanuni zenyewe zinaruhusu adhabu kama hiyo kutolewa. Bunge linaweza hata kumpiga ban ya kudumu mbunge. vilevile maamuzi ya bunge hayahojiwi wala kujadiliwa na mahakama yoyote ile. Nahisi tundu lisu kawapa huu ushauri. Tundu lissu nilikuwa namuheshimu sana, sasa naanza kumuona ni mwanasheria uchwara.
Kawaida nyie UVCCM huwa hamumpendi TL
 
Lissu anatafuta kiki,kuficha maovu yake ya ACACIA mining yaliofeli.
Huko bungeni hajamaliza ngazi za kuomba marejeo anakimbilia mahakamani.
Bahati mbaya mahakama,imefungwa mikono kwa kujadili kinachoamuliwa na bunge,hiyo kesi imeshaanguka kabla hata ya kufunguliwa.
Kwahiyo bunge ndiyo lipo juu ya sheria ktk kila jambo? Hata wakiamua kujadiliana mwisho spika akatoa uwamuzi wa kumkata kichwa mbunge mmoja, hakuna wa kuzuia maamuzi yake?
 
Nilijiuliza hili suala la wabunge kumpeleka Mahakamani Mh. Spika nikashindwa kupata jibu. Nashukuru kwa kutuwekea kifungu katika Katiba kuhusu UHURU WA MAJADILIANO NA UTARATIBU WA SHUGHULI mkuu.

Na Uhuru ukikiukwa inakuwaje?Hakuna MTU au Chombo chochote kilichojuu ya Sheria na Katiba ya Nchi.
 
344738bb3384c1bfed906b72ab65ca37.jpg

Upinzani wamefungua shauri Mahakama Kuu Dodoma wakiiomba mahakama itamke kuwa Spika ataliongoza Bunge kwa kufuata kanuni za kudumu tu.

Hii ni baada ya Spika kumzuia John Mnyika kuhudhuria bunge kwa wiki moja ambapo upinzani wamedai hakuna adhabu kama hiyo kwenye kanuni.

Wabunge Watatu Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo Chadema Wamemfungua Mashitaka Mahakama Kuu Ya Dodoma Kupinga Uamuzi Wa Bunge Kuwapa Adhabu Halima Mdee, Estar Bulaya Na John Mnyika

Mdee, Mnyika Na Bulaya Wawashitaki Spika Na Mwanasheria Mkuu

Hakuna kanuni inayosema Spika anao owezo wa kumfungia Mbunge siku saba. Haipo, bali anaingiza kanuni zake mwenyewe kutoka kichwani mwake.

Wito: Wabunge Badilini Kanuni Kuondoa Udikteta wa Spika/N.Spika ...
Vurugu za Jana Bungeni: Chanzo ni Mhe. Job Ndugai!- Ni Dikteta Hatari Kuliko Spika Anne Makinda!.


P.
 
Lissu anatafuta kiki,kuficha maovu yake ya ACACIA mining yaliofeli.
Huko bungeni hajamaliza ngazi za kuomba marejeo anakimbilia mahakamani.
Bahati mbaya mahakama,imefungwa mikono kwa kujadili kinachoamuliwa na bunge,hiyo kesi imeshaanguka kabla hata ya kufunguliwa.
kuwa na akiba ya maneno, siku zijazo uzi huu huu wataufufua hapa na ukanushe
 
wabunge ni wawakilishi wa wananchi. kwangu haiingii akilini mbunge kusimamishwa kuwakilisha wananchi waliomchagua pale bungeni kamwe. kuzuia mbunge asiingie pale bungeni ni sawa na kuwazuia wananchi wa kibamba kwa mfano wasitoe maoni yaon
 
Ndugai yuko sahihi. Kafuata kanuni na kanuni zenyewe zinaruhusu adhabu kama hiyo kutolewa. Bunge linaweza hata kumpiga ban ya kudumu mbunge. vilevile maamuzi ya bunge hayahojiwi wala kujadiliwa na mahakama yoyote ile. Nahisi tundu lisu kawapa huu ushauri. Tundu lissu nilikuwa namuheshimu sana, sasa naanza kumuona ni mwanasheria uchwara.
Weka hizo kanuni na vifungu vyake hapa mezani.
 
Kama serikali inashitakiwa ambayo Bunge na Mahakama zinaitegemea iweje Bunge lenyewe lisishtakiwe!? Mahakama ndio chombo cha mwisho cha kufafanua sheria sio ndugai wala jpm. Kilaza wewe.
Ndugai yuko sahihi. Kafuata kanuni na kanuni zenyewe zinaruhusu adhabu kama hiyo kutolewa. Bunge linaweza hata kumpiga ban ya kudumu mbunge. vilevile maamuzi ya bunge hayahojiwi wala kujadiliwa na mahakama yoyote ile. Nahisi tundu lisu kawapa huu ushauri. Tundu lissu nilikuwa namuheshimu sana, sasa naanza kumuona ni mwanasheria uchwara.
 
Hii nchi ya ajabu Sana, watu wanaongoza mambo kama vile familia ya Baba, mama na watoto wawili, inasikitisha Sana.
 
Ndugai yuko sahihi. Kafuata kanuni na kanuni zenyewe zinaruhusu adhabu kama hiyo kutolewa. Bunge linaweza hata kumpiga ban ya kudumu mbunge. vilevile maamuzi ya bunge hayahojiwi wala kujadiliwa na mahakama yoyote ile. Nahisi tundu lisu kawapa huu ushauri. Tundu lissu nilikuwa namuheshimu sana, sasa naanza kumuona ni mwanasheria uchwara.
Tatizo machadema yanamwona Tundu kuwa mungu wao na ndio kinga yao hata akinya bado kinyesi chake ni mkate
 
Wewe mwendawazimu hakuna Uhuru usio na mipaka. Lete kanuni ya Bunge inayompa mamlaka ndugai kumzuia mbunge mwaka mzima.
Ndio hapo sasa ninapomuona Tundu Lissu anawadanganya mazwazwa ya bawacha,halafu ni mavivu ya kusoma,yenyewe Lissu au Mange akisema tu yanafuata mkumbo
 
Back
Top Bottom