DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

Mimi ni mtanzania mzalendo sina chama ninampenda mtanzania yeyote yule bila kujali ni chama gani, dini gani, kabila gani, rangi gani, sehemu gani aliyotoka n.k.
Kwa suala hili la ndugu yetu kipenzi chetu Tundu Lisu kupigwa risasi wengi wetu wameshapeleka mawazo upande mmoja fulani hivi...... lakini kumbuku Rais wetu mpendwa ni mtu mwenye nia ya maendeleo mimi kama mzalendo mwingine yeyote nampongeza rais mpendwa kwa sababu kazi anayoifanya ya kula pande mbili ndani ya chama chake na upande wa pili pia, kila mzalendo tanzania mwenye uchungu na nchi hii lazima asifu kazi za rais mpendwa wa watanzania ndg Magufuli. Lakini kumbukeni rais ni kama binadamu mwingine awaye yote na amepania kufanya kazi ile kwa nguvu zote, kwa hiyo kwa ninavyomwelewa anataka afanye kazi bila kelele nyingi, au kama ukiona kosa sehemu basi kama mtu maarufu unaweza kumuarifu kuwa kuna kosa mahali badala ya kuongelea hadharani ili alifuatilie, najua kwa yale mambo anayoyafanya ya kuzuia siasa si kikatiba lakini vilevile sis wananchi hatutaki siasa majukwaani bali tunataka tuone matendo na bila shaka nitamuunga Rais Mkono kwa hili la kutaka kufanya kazi zaidi kuliko siasa za majukwaani.

Pili, kwa mwazo yangu kuna coicedence hapa, jinsi rais anafanya kazi ya kupamban na wanyonyaji wa uchumi wetu, wana mipango mingi sana ya kuharibu ile mipango ya rais wetu, mfano haya makinikia ya almasi kuna mabepari walikuwa wanavuna kama wako kwao vile sasa hii nguvu ya rais wanataka kuhamisha na kufuta la makinikia ili tuanzishe habari nyingine za misiba na tusahau mambo ya wizi mkubwa kwenye madini yetu, maana wanajua wakimuua mtu popular ana critical kama Mwanasharia mzalendo Tundu lisu ambaye kwa sasa habari ya mjini ni Lisu, baada ya zile Buldozer wetu na Rais wetu Magu.

Sasa basi tuwe na uvumilivu yawezeka ni watu tu wana nia ya kuhamisha hili suala la makinikia na kuanza habari za msiba ili tusahau. tushirikiane na serikali yetu tumpate huyo adui anayetaka kuifanya hii ndege yete "TANZANIA" isitakeoff yaani isianze kupaa.

Ndugu zangu niwaeleze kitu kimoja mliomo humu hakuna wazungu, au mtu kutoka nje ya tanzania anayetaka watanzania tuendelee kwa hiyo lazima tuwe wamoja katika hili, tushirikiane na serikali mpaka hao watu wapatikane.

maana kubwa ya kuandika hili ni kuwa kwa sababu tu ndug yetu tundu lisu amesumbuana na serikali basi wengine wanaweza kutumia hi nafasi kufanya uhalifu wao na wananchi wakaamini yule aliyekuwa anamsumbua ndiye aliye muua tuwe macho sana.

Nawapenda watanzania wote hayo ni mawazo yangu, tujenge nchi tuwe wazalendo badala ya kuwa washabiki

aksanteni

Tutoe muda useme, lakini inatia uchungu sana.
 
Tangu nipate habar hz kila nilichojaribu kufanya nimeshindwa. Moyo unaniuma sina namna ya kuelezea. Niseme tu Mungu amponye na ashughurike na wates wetu. Kumpoteza Lissu ni hasara kwa taifa isiyoelezeka. Sijui kama viongoz wanafaham mchango wa Lissu. Niishie hapa
 
Wakuu,

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ajeruhiwa kwa risasi.

Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya!




56d494001b8e52eca1b71490ff9635e4.jpg


9f94cea0e0708e5fafb57915caf1dd27.jpg

abc21fedd617180297c6247f403b7362.jpg


Updates to follow

=======

UPDATES:

=======

UPDATE: Ndege imeshawasili Dodoma ili kumchukua Tundu Lissu kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi

DODOMA: RPC amesema watu waliomshambulia Tundu Lissu walikuwa wakitumia gari aina ya Nissan la rangi nyeupe

Freeman Mbowe: Ndugu Lissu kwa sasa yuko katika chumba cha upasuaji anajaribu kuokoa maisha yake, nitazungumza baadaye.
View attachment 583459
UPDATES: Miongoni mwa waliofika hospitali kumuona Lissu ni Spika Job Ndugai, Waziri Ummy Mwalimu na katibu mkuu wa bunge, Dkt. Thomas Kashilila

TAARIFA YA AWALI KUHUSU SHAMBULIO LA KUPIGWA RISASI MHE. TUNDU LISSU

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kupigwa risasi Mwanasheria Mkuu wa Chama ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Antipus Lissu baada ya kikao cha Bunge mchana wa leo.

Shambulio hilo limetokea majira ya mchana nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma.

CHADEMA tunalaani vikali kitendo hicho, na tunafuatilia kwa karibu hali yake.

Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Uenezi, Mawasiliano na Mahusiano ya Nje.

CHADEMA MAKAO MAKUU

DAR ES SALAAM.

=====

Preliminary Press Statement on the incidence of Hon. Tundu Lissu being shot

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) has received with great shock the report on the shooting of the Attorney General of the Party who is also the Chief Whip of the Official Opposition in Parliament and MP of Singida East, Hon. Tundu Antipus Lissu just after a Parliamentary session today.

The attack took place at his Dodoma residence at midday and was seriously wounded and had been rushed to the Dodoma Regional Hospital.

CHADEMA strongly condemns this act, and we are following up closely on his condition.

We will continue to update as we get more information.

Issued by the Directorate of Ideology, Publicity, Communications and Foreign Relations.

=======

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.

Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari.

"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na kuanza kurusha risasi upande wa Lissu." amesema.

Selasini amesema, “Risasi zilimpata mguuni, mkononi na tumboni lakini daktari anasema anaendelea vizuri."

Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari huku wengine wakilia.

MORE UPDATES

Katibu wa Bunge amethibitisha kufika kwa ndege Dodoma kumchukua Tundu Lissu kumpeleka hospitali ya Muhimbili ili kuokoa maisha yake

View attachment 583477

Rais Magufuli ametoa pole na kutaka Vyombo vya Dola kuchukua hatua:

3b0c289593c46e591d17070adda48d11.jpg


CCM imetoa pole

31c0c74743877f774b093e84c0906232.jpg


Waziri wa zamani, Mark Mwandosya naye ametoa pole

12d9f3126c463d0b2305ab6ada291270.jpg


Hivi hiyo barua ya CCM ya tarehe 7 August 2017 walikuwa wameiandaa wakati wanapanga hili tukio au ni bahati mbaya tu?
 
Kwahiyo alipopatiwa first aid hospitali ya rufaa Dodoma walishindwa kummalizia hapo na hawakujua kama angejeruhiwa first step angepelekwa hapo?

Son of a teacher and you still don't get it, kama nia ni kuua wangejipanga vipi kwenda kummalizia hospitali ya rufaa Dodoma???
 
Lissu nae si alijui hilo why hakumwambia tupotilize?!!!

Hicho ndicho tunataka dereva atuambie kwa kuwa kwa sasa Lissu hawezi kutueleza ilivyokuwa. Je dereva alimtaarifu Lissu kuhusu gari lililokuwa linawafuata? Au alikuja kumwambia usishuke baada ya kufika eneo la tukio wakati wauaji walishakuwa tayari kushambulia?
 
Arud bungeni kwa rivas au kwa kufanyaje kwa mfano?Lissu alishasema kuwa anafatiliwa nadhan video ipo HUMU.DEREVA amejitahid alivyoweza

May Allah bless Me and You

Lissu amezungumza kumbe baada ya kushambuliwa? Maelezo ya dereva yanasema alishtukia kuna gari linawafuatilia kabla ya kuingia nyumbani. Kwa nini hakukimbiza hilo VX kuelekea kwenye usalama? Au unataka kusema mtaa anaokaa Lissu hautoki mpaka urudi reverse?
 
Lissu amezungumza kumbe baada ya kushambuliwa? Maelezo ya dereva yanasema alishtukia kuna gari linawafuatilia kabla ya kuingia nyumbani. Kwa nini hakukimbiza hilo VX kuelekea kwenye usalama? Au unataka kusema mtaa anaokaa Lissu hautoki mpaka urudi reverse?
Agost 18,2017 Lissu alisema kuwa anafatiliwa na alitaja aina ya gari na Namba zake.
Huo uzi upo hapa JF na video ipo.
Kwa hiyo hata kama leo ameona anafatiliwa basi alichukulia kawaida.
Then kama waligundua wanafatiliwa wao sidhan kama walihisi wanaowafatilia wana Silaha.
Na hatujui mazingira yalikuwaje?Ya kuwafanya waongeze mafuta?Warudi nyuma?Au wakanyage mafuta kuendelea kwenda kwingine?
Hope dereva wake atakuja kuweka bayana.
Kuhusu Lissu kuongea baada ya shambulizi SIO KWELI

May Allah bless Me and You
 
Nafikiri ipo haja ya wapinzani kuachana na siasa wafanye mambo mengine. Tuliambiwa vyama vingi ni hitaji la katiba lakini kumbe kuna huyu mwenzetu hataki kusikia habari ya upinzani. Tuiache CCM ifanye itakavyo. kama upinzani ni uadui wa namna hii, hakuna sababu ya kuwepo vyama vya upinzani. kama ni kuuana kwa namna hii, basi tuachane na siasa za vyama vingi, ibaki CCM tu kama wana CCM na viongozi wao wanavyotaka. JK kashauri juzi tu kwamba upinzani si uadui, lakini hawaelewi kabisa.

Freedom has a price. Hayo wanayoyafanya CCM na viongozi wao kama yasingekuwa yanamuathiri kila mtanzania kungekuwa na busara kwenye hayo uliyoyasema. It is better to die on you feet than to live on your knees.
 
Kwanza, sisi ni binadamu ambao hapa duniani hatutakuwepo milele na hivyo tunapita. Hapa tu safarini. Tutendeane na kusemeana yaliyo mema. Sote tu safarini.
Hatuna haja ya kusakana na kushambuliana kwa mijadala tu.

Pili,amani na utulivu tulionao kama nchi ni zao la utawala wa sheria na kusikilizana;tukosoane kwa staha na kuvumiliane wakati wa kutofautiana kwetu. Kukosoana ni afya ya kinchi kiutawala na kisiasa.

Tatu, wakosaji washughulikiwe kwa mujibu wa katiba,sheria na taratibu tulizojiwekea kama taifa. Hatuna haja ya kushughulikiana kwa namna nyinginezo.

Nne, tumtangulize Mungu katika kuilinda amani yetu kwakuwa ndicho kinachotuunganisha kama taifa na ndicho kinachotufautisha na nchi nyingine.

Tano, tuviamini vyombo vyetu vya ulinzi na usalama katika kuchunguza na kushughulikia wahusika wote wa matukio ya kijinai. Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama viko imara na vyenye weledi wa kutosha.

Sita, kila mmoja wetu ana umuhimu wake na nafasi yake katika taifa hili. Kila mmoja wetu ana wanaompenda na kumkubali na wale wasiompenda na wasiomkubali. Mchanganyiko huo ndiyo nchi yenyewe.
Watakuwa wameingilia account yako.

"PAMBANA NA HALI YAKO"
 
Moja yaManatumizi Mabaya ya sentensi za kiswahili
”Watu wasiojulikana ”
Utalisikia Neno Hilo hata pale video ya mhusika na jina lake vikiwekwa hadharani.
Nafunika vinywa vya viongozi wote Tanzania kwa Damu ya Yesu
 
Back
Top Bottom