Dodoma: Tundu Lissu afuata gari lake lililoshambuliwa ofisini kwa RPC Muroto. Ashangaa hadi sasa hajahojiwa yeye na Dereva wake

Hehehe Jamaa haogopi tena kifo wala mateso... Huu ujasiri wake ipo siku utaleta matunda positive.. Vile vijana now wana amka na kuacha uoga...Nchi watu tulikuwa waoga sana.. Ila jamaa anachofanya anaweka attitude fulani hvi watu waache uoga
Mtukufu alijaa ushetani kupita kiasi mpaka shetani wengine wamemkimbia mungu kumwambia aache mipango ya shambulio la pili ambalo lilipangwa tena na Bashite na cyprian Musiba ambalo walitaka liwe ni njia za kujipendekeza kwa mtukufu wapate uteuzi, kwa Bahati nzuri sasa wapo wanaccm hawapendi uonevu wanaofanyiwa chadema huwamegea taarifa za vikao vya siri vya kuwaangamiza toka kwa viongozi wote CCM.
 
Arudishiwe gari yake tutamchangia alitengeneze kama bima wasipomlipa.
Bima inapaswa kulipa soon, wakiishapata police report,ila kwakuwa polisi hawajiangahishi na uchunguzi wa tukio.

Bima nao wanaweza wakachelewa kusubiria police report, hii ni assumption yangu.
 
..inachukua miaka mitatu kulichunguza hilo gari?

..hao hawachunguzi chochote, wamrudishie TL gari lake.
Gari hawataweza kumpa kwa sasa, linaweza kuleta kizaa zaa, pindi wakilazimika kuchunguza na likawa liliisha tengenezwa au kuuzwa na kumilikiwa na mtu mwingine.

Hilo litakuwa hapo polisi kwa muda mrefu, nahisi.
 
Kalifuata ila hapo ukute wameshaiba kila kitu hadi engine!!! Ndipo kesi mpya itakapounguruma....
Hawawezi kuba chochote kwasababu inaweza kutokea akashinda, halafu akawataka wachunguze au akaomba msaada wa uchunguzi wa tukio nje ya nchi.

Itakuwaje sasa ikiwa litakuwa limeharibiwa na polisi.

Hizi ni assumptions zangu tu, sisemi itakuwa hivyo.
 
Gari hawataweza kumpa kwa sasa, linaweza kuleta kizaa zaa, pindi wakilazimika kuchunguza na likawa liliisha tengenezwa au kuuzwa na kumilikiwa na mtu mwingine.

Hilo litakuwa hapo polisi kwa muda mrefu, nahisi.

..sidhani kama Polisi wanachunguza.

..ndiyo maana nashauri wampe TL gari lake, badala ya kuendelea kumdanganya, na kuwadanganya waTz.
 
..afande Sirro alisema wapelelezi wake wanamtafuta TL lakini hawajampata.

..sasa leo TL kaenda mpaka kituoni kilichowashinda kumkamata na kumhoji ni nini?
JokaKuu
Hawa jamaa wa CCM pamoja na Jeshi "lao" la Polisi kwa propaganda hawajambo!

Wakati Tundu Lissu yupo nje kwa matibabu, IGP Sirro na wale mashabiki wao wa Buku 7 walikuwa wanatuaminisha kuwa upelelezi wa Jeshi la Polisi hauwezi kuendelea kwa kuwa Tundu Lissu na dereva wake wapo nje ya nchi..............

Huyu IGP Sirro akawa anatuahidi kuwa mara tu Tundu Lissu na dereva wake watakaporejea, basi Jeshi lake litakamilisha upelelezi wao wa tukio lile la kushambuliwa Tundu Lissu kwa risasi..............

Hivi sasa ni mwezi mmoja kamili, tokea Tundu Lissu na dereva wake warejee nchini, mbona Jeshi la Polisi bado linapata "kigugumizi" kumuhoji Lissu??
 
Lissu anajua sana kuwachokonoa hawa poyoyo wa CCM wanaokula laki 4 kwa mwezi
 
Mnapiga porojo halafu matokeo sifuri, chadema wajinga sana nyinyi,mnashindwa kuangalia ni namna gani mtapambana kupata haki ya kugombea ubunge majimbo zaidi ya 20 hayatakuwa na uchaguzi wabunge,mnafosi ushindani na magufuli ambae huyo lisu hata haendani nae.hivi mfumo wa taasisi ya uRais inaendana na huyo jamaa kweli? Mbona mnakuwa wajinga kuwaza mambo ambayo hayawezi kutokea?
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA

Mgombea Urais wa JMT kwa tiketi ya CHADEMA, Mh. Tundu Lissu, leo ametembelea Ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kuchukua gari lake ambalo limehifadhiwa na Jeshi la Polisi Mkoa huo jaribio la mauaji dhidi ya Mh. Lissu la tarehe 7 September 2017.

Mh. Lissu aliambatana na mgombea mwenza wake Mh. Salum Mwalimu na alipokelewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Giles Muroto.

Katika mazungumzo yake na SACP Muroto, Mh. Lissu alisema kwamba ameamua kuja yeye mwenyewe baada ya utaratibu wa kulipata hilo kwa njia zingine kushindikana.

Kwa upande wake, SACP Muroto alimweleza Mh. Lissu kwamba Jeshi la Polisi mkoani hapo linahitaji muda zaidi ili kujiandaa kulikabidhi gari hilo kwake.

Aidha, SACP Muroto alimweleza Mh Lissu kwamba Jeshi la Polisi linamhitaji atoe maelezo kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwake September 2017.

Mh. Lissu alijibu kwamba yeye yuko tayari kutoa maelezo polisi kwa tarehe na muda utakaokuwa muafaka kwa pande zote mbili.

Mh. Lissu alisisitiza mshangao wake kwamba hadi sasa, takriban miaka mitatu tangu kushambuliwa kwake, Jeshi la Polisi halijafanya uchunguzi wowote, ikiwemo kumhoji yeye na dereva wake Adam Bakari Mohamed, licha ya kuahidi kwamba lingefanya tangu Mh. Lissu akiwa hospitalini nchini Kenya.

Imetolewa leo Alhamis, Agosti 27, 2020 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
Huyu Lissu ni mpumbavu kweri kweri. Mahakamani haendi kwenye makesi yake kisa "eti" yupo bize anagombea, wakati huo huo kiguu na njia Polisi tena bila hata kuitwa "eti" kuulizia kwanini haojiwi! Pumbavu!!!!
 
Huna lolote we Mamluki
angalia hii
View attachment 1549652
Kwani mimi nimeandikaje au kusoma kiswahili nako tatizo.
Mimi nimeelezea kwanini polisi hawamkamati Lisu sasa hizi ambazo wewe unazileta na kutaka ku8tofautisha na mimi na niluichosema ni katika vitu ambavyo havihusiani kabisa.
Si kila kitu unakimbilia kupinga na kuona watu ni mamluki,kha.
 
Nashangaa hawajamkamata!! Mbona wanakuwa wema sana kwa Lissu tangu arudi.
hiki ni kipindi cha kampeni hivyo lazima uwe makini na hatua unazochukua dhidi ya kila ufanyalo, ndio maana walifanya maandamano siku ya msiba wa kitaifa wa hayati Mh. Benjamini Mkapa - raisi mstaafu na hawakufanywa chochote, wakaja na kauli za kutatanisha na kutishia usalama wa TZ ila wao wakakaa kimya, saiv kaamua kwenda polisi mwenyewe angali anajua ya kuwa hakuwa tayar kutoa ushirikiano toka mwanzo na kubaki kutoa povu dhidi ya vyombo vya ulinzi na Raisi wa nchi huku akikataa kuja kuendelea na kesi, ila hivi sasa ndio anaenda polisi coz anaona njia zote alizojaribu kufanikisha lengo lake zimegonga mwamba - nao wanamuangalia tyuuu kama mwana sesere.
 
Siasa za Africa mbaya sana, zinaumwa, hawatamuua safari hii! zina gharama kubwa sana, kufa na kupona!
 
Back
Top Bottom