Dodoma: Tukio la mwanamke kutandikwa makofi hadharani na mtu anayedhaniwa ni Mwanajeshi

dr namugari

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
8,685
14,578
Juzi kulitokea tukio la kushangaza kidogo. Jamaa mmoja mida ya saa kumi na moja jioni aliagiza k.vant kubwa katika moja ya grocery inayopatikana maeneo ya ilazo extension Dodoma.

Mwanamke aliyekuwa mmiliki wa grocery na duka hiyo alimjibu jamaa yule shiti sana hadi kupelekea jamaa yule kunyanyuka na kisha kumzibua makofi mazito na kupelekea mwanamke kuanguka na Kisha kuingia ndani kulia na Kisha kuchukuwa simu kumpigia mume wake kuwa nimepigwa makofi.

Basi jamaa mumewake akawasha gari akaja eneo la tukio kuja kumuona aliye mtandika mkewe makofi. Jamaa alifika na kuoneshwa mtu yule na kisha kumfata.

Jama mume: Wewe vipi mbona unampiga mke wangu makofi?

Jamaa jeshi: Kwani wee unataka nini?

Jamaa mume: Unanijua mimi ni nani?

Jamaa jeshi: Kwani wewe unajua mimi ni nani?

Jamaa mume: Nitakufanya kitu kibaya ujute kuzaliwa.

Jamaa jeshi: Fanya chochote hata sasa, huna cha kunifanya na ole wako usoge hapa nitakumwaga ubongo na chupa hii pumbafu sana! Ndio muwe mnawafundisha wake zenu adabu vinginevyo tutawaumiza sana na hakuna cha kutufanya.

Basi tukaingilia kati jamani acheni hizo siyo poa ni vyema kujua ilikuaje hadi mke kupigwa makofi. Bwana huyu hajalewa hata kidgo labda katukanwa, basi jamaa kanywea.

Jeshi kakausha zake kisha kujiondokea zake huku jamaa akibaki hana la kufanya, ikabidi ilifika muda wakafunga duka wakasepa hadi leo yule mwanamke hajaonekana pale.

Tukio la jana tena Simba na Dodoma jiji.

Muhudumu wa grocery hiyo aliyeachiwa baada ya mama yule kwenda kuuguza makofi aliyotandikwa na jeshi nae akatoa boko.

Ilikuwa Muda wa kudai pesa za mpira wa Simba, basi alivyofika kwa mmasai mmoja jina la Musa akampiga kofi la mzaha hivi na kisha kuchezesha mikono kuwa toa pesa toa pesa. Basi Masai alivyopigwa kofi na akaona amedhalilika akasimama kwa hasira kali mno kwa kupigwa kofi na mwanamke tena hadharani.

Mwanamke akijua kuwa Masai hawezi mfanya lolote, alijikuta yuko chini kwa kofi zito aliyotandikwa na Masai hadi sasa shavu la kulia limevimba vibaya.

Natoa rai
Kuwa wanawake kuweni na heshima na muache kujifanya wababe mkidhani kuwa mume au hawara atakusadia pindi ukiyakanyaga kwa wakoraa. Ona sasa dada yule amedhalilika na mume kashindwa kukupigania na huku alikuja kwa mbwembwe tukajuwa patachimbika kumbe hakuna lolote. Aibu sana , huyo mume unamuonaje hivi sasa?
 
Wajeshi ni watu pisi sana, hadi kupeleka kofi alikuwa amedhalilishwa sana.
...Si wajeshi tu, wanaume ni watu wa Amani hasa wanapokuwa na wanawake pia kiasili kiumbe cha kiume kupiga/kupigana na kiumbe cha kike huwa ni adhimu sana na hii inatokea sana kwa binadamu na kwa 99.9999% inachangiwa na wanawake hiyo 0.0001% ndio Sababu tofauti kama Pombe, Vilevi vinginevyo, n.k
#wadadaAcheniMidomoMirefu
 
kwa nini usiandike tu kuwa mwanajeshi ampiga raia Kofi.......kwani kulikuwa na haja gani uweke Mwanamke.
Hata hivyo siungani na kilichotokea kwa raia husika kwani ni kinyume na utaratibu na maadili yetu
 
kwa nini usiandike tu kuwa mwanajeshi ampiga raia Kofi.......kwani kulikuwa na haja gani uweke Mwanamke.
Hata hivyo siungani na kilichotokea kwa raia husika kwani ni kinyume na utaratibu na maadili yetu
na ndio huu unaitwa uandishi wa kikanjanja, kwani umeambiwa anavyompiga alikuwa kavaa uniform??? Mnashindwa kutofautisha makosa binafsi na makosa yanayohusisha kazi... askari anapofanya kosa fulani akiwa katika sare unaweza kuandika KICHWA CHA HABARI kumtambulisha kwa kazi yake katika tukio hilo sababu huenda likaambatana na picha ila akiwa kavaa kiraia utambulisho wa kazi yake utakuwa ndani ya habari na sio kwenye KICHWA CHA HABARI...Watu wengine mandezi sana huwa wanadhania hao askari wao hawana mwili na damu as if walishushwa tu makambini na wao ni wa vyuma wakati tumezaliwa nao, tumekua nao, tumesoma nao, tumeishi nao na tabia zao ni zile zile akiajiriwa tu inakuwa NONGWA... Wabongo acheni Nongwa mwanamke kaleta ngebe kwa mwanaume popote pale acha akandwe.!
 
Mkuu haijarshe ni mjeshi au raia ni swala la kuheshimiana tuu ata mimi ukinivuruga nakuwashia moto tuu Tatzo jamaa sio kashindw kusimamia haki ya demu wake ni kwamba hajui mwanamke wake amemfanya nn /ugomv upoje ndio jambo lipo hapo


Swala mtu mwenye ajira kupgan au kupga ni zto sana mkuu huwa hatua ya mwishoo kbs maan nirahis kutia doa kibarua
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom