Dodoma: Spika Ndugai ashangaa baadhi ya makofi yanayopigwa na Wabunge

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,696
3,472
Spika wa Bunge Job Ndugai amesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakipiga makofi bungeni lakini haijulikani wamepiga ya nini.

Ndugai alisema hayo jana wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza Khamis akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu (CCM) Husna Sekiboko kwamba polisi wamekuwa wakishindwa kufika kwa wakati maeneo mbalimbali kwa sababu ya kukosa mafuta na matengenezo ya magari.

Awali, akijibu swali Khamis alisema kwa mujibu wa sheria ya bajeti wenye fungu ni mkuu wa polisi nchini (IGP) na Ma-RPC hivyo fungu likitoka kwa IGP linakwenda kwa RPC na kisha kugawiwa kwa wakuu wa polisi wa wilaya husika.

Alisema wanalichukua suala hilo na kwenda kukaa na wadau ili kuona namna wanavyoweza kulifanyia mabadiliko.

Hata hivyo, majibu hayo yaliwafanya baadhi ya wabunge kumpigia makofi naibu waziri huyo, hali iliyomuibua Ndugai ambaye alisema kuna wakati wabunge wanapiga makofi haifahamiki wanapiga ya nini.

Ndugai alihoji kuwa: “Halafu waziri akakae na wadau, wakina nani? Halafu tunashangilia (wabunge) tunakubali hiyo kanzu.”

Chanzo: Mwananchi

======

My take: kwani ndugu Spika alitegemea kitu tofauti toka kwa Wabunge(90%+) wa Chama kimoja?
 
Eti akakae na wadau. Huyo naibu waziri koro wa kiwango cha kwanza. Issue za usalama ni jukumu la kwanza la Serikali hata makusanyo yataongezeka kukiwa na usalama.

Sasa hao wadau anao wataja ni wakina nani? Kama vipi wakabidhi vyombo vya wizara ya mambo ya ndani kwa sekta binafsi maana ndio wadau hao.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Bunge lilikuwa linaongozwa na wapinzani kwa hoja zenye tija kwa watanzania, wabunge wa CCM walikuwa kwa manufaa ya chama.
Hayo makofi ndio yaliyokuwa yanatakiwa, na wabunge wanashangilia waziri anapoenda kukaa na wadau.

Inashangaza eti sasa ndio Mbunge Msukuma anagundua kwamba hali ni ngumu mitaani, kitu kilichoongelewa sana na wabunge wa upinzaji kipindi cha nyuma, na yeye alikuwa ni mmoja kati ya watu waliokuwa wanawazomea wapinzani.
 
Back
Top Bottom