Dodoma: Shughuli za Bunge zaahirishwa kufuatia kifo cha Mbunge Irene Ndyamkama

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson amelazimika kuahirisha shughuli za Bunge hadi Jumatano ya April 27 kutokana na kifo cha Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa (CCM), Irene Alex Ndyamkama, kilichotokea jana Aprili 24, 2022


1650875633146.png

=======

Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson ameahirisha kikao cha Bunge leo Jumatatu Aprili 25, 2022 kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Rukwa (CCM), Irene Ndyamkama kilichotokea jana katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha alikokuwa akipatiwa matibabu.

Dk Tulia amesema mwili wa mbunge huyo unatarajia kuagwa na wabunge Jumatano Aprili 27, 2022 katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.

Kanuni za bunge zinaelekeza unapotokea msiba wakati wa vikao vya bunge, shughuli za siku hiyo zitaahirishwa kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wabunge kufanya maombolezo.

Spika amesema taratibu zingine kuhusu ratiba nzima zitatangazwa

Chanzo: Mwananchi

Pia Soma >>> TANZIA - Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamkama afariki dunia
 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa,alikuwa na mimba kubwa nadhani ni complications za uzazi,Mama yake mzazi pia ni Mbunge somebody Lupembe
 
Back
Top Bottom