Dodoma: Shirikisho la Walemavu laipongeza NEC

Tofautisha ulemavu na ugonjwa. Ulemavu ni hali ya kupungukiwa kitu fulani katika mwili. Inaweza kuwa ni akili, macho, masikio au kiungo kimojawapo katika mwili. Upungufu huu ni wa kudumu.

Lakini ugonjwa ni hali ya muda fulani tu. Karibu kila mtu, muda fulani amewahi kuwa mgonjwa. Ndugu zetu walemavu, wengine huzaliwa nao, wengine huupata ulemavu baadaye, lakini baada ya kuupata, linakuwa ni tatizo la maisha yake yote.

Wakati watu wote wenye akili timamu, kwa uthibitisho ulio dhahiri wanasema, uchaguzi uligubikwa na kila aina ya uchafu, halafu mlemavu (mwenye upungufu wa akili, asiyesikia, asiyeona, n.k.), anasema kila kitu kilikuwa safi. Kuna nini cha zaidi unachoweza kusema kwa hawa walemavu, zaidi ya:
1) kwa sababu wengine wana ulemavu wa akili, labda hawana uwezo wa kujua kilicho sahihi na kilicho batili
2) Labda kwa sababu wengine hawasikii, hawakuweza kusikia chochote kwa wakati kuhusiana na uchaguzi, wanaongea walicholishwa
3) Labda kwa sababu wengine ni walemavu wa macho, hawakuweza kuona chochote, pamoja na ule uchafu wa kura fake za CCM

Jumuisho: Hawa ni walemavu, wasamehewe, waonewe huruma, tusipoteze muda kuwajadili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeeleweka vyema mkuu.
 
Shirikisho la Vyama vya Walemavu Mkoa wa Dodoma (SHIVYAWATA) limeishukuru Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwawezesha kuwaondolea vikwazo watu wenye ulemavu kwenye upigaji kura katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Shukrani hizo zilitolewa na Katibu wa SHIVYAWATA Mkoa wa Dodoma, Jastus Ngw'antalima wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, kuelezea furaha yao waliyopata kutokana na kushirikishwa kikamilifu katika kuchaguzi Rais, Wabunge na Madiwani ijapokuwa walipata changamoto kidogo.

Katibu huyo alisema, wakati wa upigaji kura, katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, vikwazo vingi vinavyokwamisha watu wenye ulemavu kupiga kura vilitatuliwa na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika upigaji kura huo.

Alisema kutokana na urahisi huo wa kuhakikisha watu hao wenye ulemavu wanashiriki kwa wingi pia imechangia kuwawezesha watu wenye ulemavu kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura na kupiga kura kwa urahisi.

"Sisi kama Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Mkoa wa Dodoma, tuna kila sababu ya kuwapongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuturahisishia upigaji kura kuwa rahisi kwetu tofauti na uchaguzi za huko nyuma," alisema.

Katibu huyo alitaja baadhi ya vikwazo vilivyofaidika navyo kwenye upigaji kura huo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa ongezeko la vituo vya kupigia kura, vifaa vingi vya kupigia kura, kuthaminiwa na kupewa ushauri wa kutosha wakati wa kupiga kura.

Hata hivyo katibu huyo alisema, pamoja na kuondolewa kwa changamoto hizo bado watu hao wenye ulemavu wamekutana na vikwazo vya miundombinu kwenye baadhi ya majengo ya shule na kulazimika kubebwa ili aweze kuvifikia vituo vya kupigia kura vilipokuwa vimewekwa.

Alisema kuwa baadhi ya majengo ya shule ya zamani hayajarekebishwa miundombinu yao, hali ambayo watu wenye ulemavu kukutana na changamoto hizo na kujikuta wakipewa msaada wa kubebwa.

Alitaja majengo hayo ambayo yalikuwa yamewekwa vituo vya kupigia kura ni kuwa ni pamoja na majengo ya shule ya msingi na sekondari na ofisi za serikali ambazo nyingi hazina miundombinu ya watu wenye ulemavu au hazijarekebishwa ili kuwapa nafuu watu wenye ulemavu.

Katibu huyo pia aliwataka watu wenye ulemavu mkoani Dodoma kutojihusisha na chokokocho yoyote ambayo inayoashiria kutaka kuharibu amani ya nchi kwani hakuna pa kukimbilia kama kutatokea vita na watu wenye ulemavu watakuwa waathirika wakubwa ikitokea vita hiyo.

Aidha, aliwataka kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kufanya shughuli zinazowaingizia kipato ili kuiunga mkono serikali katika juhudi zake za kuleta kukuza uchumi ili kuleta maendeleo zaidi kwa watu wote wakiwemo na watu wenye ulemavu.
I AM SORRY TO SAY THAT MNA ULEMAVU WA UBONGO
 
Back
Top Bottom