Dodoma: Serikali kuzindua Makao Makuu ya kitaifa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,794
2,000
Kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika, Serikali inatarajia kuzindua Makao ya Taifa ya Malezi na Makuzi ya Watoto yaliyojengwa katika Kata ya Kikombo, jijini Dodoma.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Dkt Dorothy Gwajima amesema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Isdor Mpango atazindua makao hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yatakayofanyika tarehe 16 mwezi huu.

Dkt. Gwajima amesema lengo la kujengwa kwa makao hayo ni kutatua changamoto za makao ya Taifa ya awali yaliyokuwa Kurasini Dar es Salaam za ufinyu wa maeneo ya shughuli mbalimbali ikiwemo michezo, bustani, ujasiriamali na ufugaji kutofanyika sawasawa hivyo kufanya hali ya lishe na uchumi kuwa duni.

"Ujenzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Taifa wa Kimkakati wa kuwatambua, kutengamanisha na kuwaunganisha na familia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, pia ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais kuwa watoto wanaotunzwa kwenye makao waandaliwe mapema kadri inavyowezekana kuwaunganisha na familia ili kuwawekea msingi wa malezi" alisema Dkt. Gwajima.

Ameongeza pia watoto wanatakiwa kukaa kwenye makao kwa muda tu na wakiisha kuimarika warejeshwe kwenye makazi ya kawaida iwe ya kambo au kuasili ili waishi kawaida katika familia.

Dkt. Gwajima amesema, uzinduzi huo utaambatana na uzinduzi wa vituo vya Jamii vya malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya watoto pamoja na Baraza la Taifa la Watoto hapo tarehe 14 mwezi huu.

Aidha, Dkt. Gwajima ametoa rai kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanatimiza jukumu la malezi ya watoto wao na kuwa, hatua ya kulelewa katika makao iwe ni ya mwisho baada ya hatua zote kushindikana.

Mradi wa Ujenzi wa Makao ya Watoto Kikombo, umetekelezwa kwa Ushirikiano kati ya Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Shirika la ABBOT Fund Tanzania na Makao hayo yana uwezo wa kuhudumia watoto 250 kwa wakati mmoja na hadi sasa watoto wanaohudumiwa katika Makao hayo ni 28.
 

Mafuluto

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
1,865
2,000
Nafikiri ni muda sahihi sasa wa serikali kuwa serious ktk issue hii.

Mpango mkakati upo, lakini ukweli sehemu nyingi suala hili nimekuwa linafanywa ki usanii na NGOs nyingi imekuwa ni mradi wa kujipatia pesa watu wachache kwa jina la kusaidia watoto waishio ktk mazingira magumu.

Ipo mifano hai ya watoto hao kuteswa, pigwa wakiwa ktk shelters, pesa za wafadhili kufujwa..na watumishi ktk ofisi za serikali hasa ustawi wa jamii wanajua lkn wanapuuzia na wengine kutulizwa na viposho!

Wengine, wanawatumia watoto hawa ktk sanaa na kuwapeleka nje ya nchi kuwatumikisha, then viongozi hao kwa kushirikiana na wageni wanakula pesa za vijana hao.

Badala ya kuwafundisha maadili vijana wengi wanafundishwa namna ya kutumia ngono ili kujikomboa, yaani kuoa wageni kama ambavyo viongozi wao wamefanya, tena kwa kuwatosa wake zao wazawa na kukimbilia kuoa wageni.

Fuatilieni hasa mkoa wa DSM maana sio siri!
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,502
2,000
Inashindikana vipi kuwa na nyumba ya kulelea watoto kila mkoa. Watoto yatima na wanaotoroka nyumbani kukimbia ndoa za utotoni pia wanaoshi katika mazingira magumu.

Afisa ustawi wa jamii anakua mlezi na msimamo zo wa budget ya mwaka. Vituo vinaweza kujiongeza kuomba ufadhili kutoka kwenye makampuni.
 

COMOTANG

JF-Expert Member
Jan 6, 2021
1,564
2,000
Kwa mradi huu Mama Gwajima Ninatamani kuja kufanya kazi Hapo KUHAKIKISHA tuna wabadili Saikolojia na tabia watoto hao NILITAMANI SANA HILI LICHUKULIWE SERIOUS NA SERIKALI.HONGERA MAMA GWAJIMA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom