Dodoma: Rais Samia azindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza

Baraka Mina

JF-Expert Member
Sep 3, 2020
581
574
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Msalato jijini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anazindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo tarehe 25 Machi 2022.

RAIS SAMIA: HATUWEZI KUAJIRI WATU WAPYA KILA MWAKA
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali yake haina mpango wa kutoa ajira mpya katika Jeshi la Magereza kwa kigezo kuwa wengi waliopo wamepanda vyeo.

“Tulitoa ajira ya watu 700 ambao naambiwa niliwapandisha cheo kwa mapendekezo yenu, nina hakika kuna watu wanazurura tu kwenye korido za ofisi hawana kazi, warudi wakasimamie wafungwa.

“Hatuwezi kuajiri kila mwaka, tuna kiwango kikubwa cha mishahara tunayolipa, haina maana mtu ukipandishwa cheo basi ukae ofisini tu, kama una cheo au hauna rudi kwenye ‘field’ ukasimamie wafungwa, hicho cheo chako utabaki nacho,” - Rais Samia.

Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka Msalato jijini Dodoma ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Samia Suluhu Hassan anazindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza leo tarehe 25 Machi 2022.

Safi,wapi picha za miradi.
 
Back
Top Bottom