Dodoma: Rais Samia awatunuku Kamisheni Maofisa wa JWTZ

Naomba nikueleze kitu kimoja ambacho kimebadilika sana kwenye vyuo vingi sana nchini
IFM,TIA,IAA vilikua ni vyuo vya uhasibu zaidi ila sasa hivi wanatoa digrii nyingine nyingi pia tofauti na uhasibu japokua wamejikita zaidi kwenye uhasibu

Hata SUA chenyewe tunachojua ni cha kilimo kina degree nyingine hata hazihusiani na kilimo/ufugaji

Sasa kwa jinsi ninavyodhani mimi(Sina uhakika)
1. Kwanza walichukulia kutafuta partner ambaye yuko karibu kieneo(Geographically) kwahiyo wakajikuta na IAA tu pale Arusha

2. Nadhani pia katika kuandaa modules sana sana watakua na sheria humo, DS ,Utawala,ICT, Hesabu,Lugha nk nk na hawa wakufunzi wanapatikana IAA(kwakua kuna haya masomo pale)

3. Wakufunzi wa TMA wenyewe wanabakia kukazia katika masomo yao ya medani kama Commanding/Leadership, Shooting,navigation, endurance no nk(Hapa nadhani na hawa wakufunzi pia walikula semina za kiraia/Za kule NDC au hata nje nchi) ili kuwa na kiwango cha kutoa hadhi ya BSc

Sidhani kwa vyovyote vile kama inahusiana na Uhasibu hata kidogo(Chuo cha Uhasibu kimabaki jina tu)

Nje ya mada: Hata mkuu wa chuo cha IAA yule Sedo aliyeongea jana pale Chamwino na ndio amesifiwa kwa kukibadilisha sana hiki chuo sio Muhasibu hata kidogo. Nimesoma nae Computer Science miaka mingi iliyopiata(Advance Diploma) na mpaka kaenda nje kufanya PhD ya IT ila ndo mkuu wa chuo cha "Uhasibu"

Kuna jamaa humu alisoma Bsc Military Science Pretoria ngoja nimuombe aje kabla sijamtag atuambie
Sina la kuongeza, 'HESHIMA' mkuu.

Ahsante sana.
 
Back
Top Bottom