DODOMA: Rais Magufuli azindua jengo la PSPF na tawi la benki ya NMB. Akataa kufuta hati za viwanja jirani na jengo hilo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
DODOMA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amezindua Jengo la PSPF la ghorofa 11 na tawi la benki ya NMB(NMB Kambarage)



Makongoro Nyerere:
Mheshimiwa Rais chapa kazi wanaokurudisha nyuma wapo na tumeshawazoa toka zamani. Wapo watu alinifuata wakasema "Ee bwana Makongoro, huyu huyu mheshiwa yupoje huyu? Toka ameanza kazi mbona hakuchagui?" Ili nichukie

Lakini kwa kuwa mimi ni mchezaji, kwani aliyesema mimi sio mchezaji nani? Nipo nafasi yangu inaitwa benchi la mchezaji wa akiba. Na wachezaji huwa tunafahamiana, wapiga ngoma wanafahamiana, wanasiasa wanafahamiana.

Huyu nilishapata taarifa zake kwamba anasema Makongoro usimpe kazi bwana halafu anakuja kuniambia huyu amtu namna gani. Ni hawa wanajaribu kila mbinu tukuchukie Rais wetu kwa sababu hii, moja unafanya kazoi nzuri. Chapa kazi

Hii inanipa mimi nafasi nzuri sana kwamba kazi utatoa ngapi, ni kweli kwamba Rais ni muajiri moja kwa mujibu wa katiba ambaye anaweza kuajiri watu wengi. Lakini ukiangalia idadi yetu atatoa ajira ngapi? Ila tunataka wale waliochaguliwa watuwakilishe vizuri

Sisi ndio tulikuchagua wewe na kukupa kazi, Mheshimiwa Rais Chapa kazi!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli Magufuli;
Nashukuru kwa viongozi wote walionialika kufungu jengo hili la PSPF na tawi la Nmb la Kambarage. Pamoja na Wazee wa Dodoma nashukuru pia kumuona muwakilishi wa Mama, Makongoro Nyerere ambaye anasema anacheza kwenye benchi lakini anastahili kucheza kikosi cha kwanza kabisa

Natoa pongezi kwa PSPF kwa kujenga jengo hili hapa

Nimefurahi kusikia kuwa jengo hili limesanifiwa na kusimamiwa na watanzania na zaidi ya watanzania 250 walipata ajira hapa wakati wa ujenzi

Nimefurahi kusikia karibu asilimia 100 ya jengo hili tayari limeshapangishwa, tofauti na majengo yanayojengwa na watu wengine kwa sababu hawapo strategic. Nilienda kufungua majengo fulani na kwa wakati ule asilimia 28 ilikuwa imepangishwa

Serikali ina hisa asilimia 32 kwenye benki hii, huwa najisikia furaha kila nikiona benki hii inaendelea kufanikiwa. Napenda pia kuipongeza kwa kuwa namba moja kwa kufikisha huduma sehemu kubwa ya nchi hii. Asilimia 60 ya huduma hizo zipo maeneo ya vijijini

Napenda sana niungane nanyi kwa kumshukuru Mama yetu, Mama Nyerere kuridhia benki hii kuitwa Kambarage, nategemea wafanyakazi wa benki hii wataoa huduma itakayo endana na jina hili. Sitegemei kuwa na mambo ya rushwa au kucheleweshwa chelewashwa kwa wateja

Kwa tawi la NMB benki yapo mengi ambayo mmeyafanya ambayo yameelezwa, Naibu Waziri pia ameeleza kuhusu gawio ambalo ametoa kwenye Serikali na ametoa takwimu za Bilioni 16.5 mlizotoa mwaka jana. Mimi nimeenda mbali nikaona nicheki kuanzia mwaka 2012. Mwaka 2012/13 walitoa bilioni 10.805, mwaka 2013/14 walitoa bilioni 14.301, kwa mwaka 2014/15 walitoa bilioni 16.525, tena mwaka 2015/16 walitoa hizo hizo bilioni 16.525, na mwaka 2016/17 wakatoa bilioni 16.525. Hapa ndio nina maswali, ndipo ninapojiuliza. Ninamatumaini mwaka 2018 haitakuwa bilioni 16.525.

Haiwezekani kama benki inapata faida, wafanya kazi wanaongezeka gawio liwe constant kwa miaka mitatu kwa sisi wa 32%. Hawezekani hesabu zikawa zinagota pale pale, pale kuna mchezo mchafu unachezwa. Najua meseji sent and delivered. Watu wetu wanaotuwakilisha mkae mfanye mahesabu vizuri. Hili limeniuma

Leo mmetoa mchango wa milioni 50 hapa nawashukuru sana, na nitafuatilia kwa Mbunge na Mkuu wa mkoa nijue zinaenda kutumika wapi ilizisije zikapotea tu zikaonekana zilitumiaka. Nakama zitajenga mradi wowote mkubwa mradi ule ni bora ukaitwwa NMB Mradi

Niliwahi kukaa hapa Dodoma wakati nikiwa Makutipora sijawahi kusikia neno michuzi ila leo nimeskia na kila mtu amelipata, meseji imefika. Naibu spika amesikia na Waziri amesikia ni matumaini yangu mtaenda kulijadili Bungeni

Mwenyekiti wa PSPF yeye hataki kukaa jirani na mtut yeye anataka anapojenga yeye awe yeye tu. Kule kuna kiwanja cha ubalozi na kiwanja cha wizara kipo huko. yeye yupo hapa, parking tumeambiwa magari mia ngapi nayaweza kupaki lakini anataka lazima wazuiliwe wale wakati hata michoro ya majengo yao hajaijua inawezekana wanataka kujenga ghorofa 20.

Swala la kufuta viwanja kwa kuwa lipo karibu na viwanja vingine mimi sitalifanya lakini tunakaa nao kwa kuwa sisi ni watanzania. ukitaka kumtoa jirani mwenzako, mnunue ili kusudi mjenge hayo mnayotaka kujenga

Lakini kufuta viwanja ambavyo havina makosa mimi siwezi ikiwa wao waliomba kwa mujibu wa sheria

Katika jukumu lolote la kazi hata kwenye famili lazima watakaopatikana kupinga pinga kidogo lakini kikubwa na kunyoosha msitari ili kulenda maendeleo kwa watanzania. Wapo wengine watatumika na mabepari. Serikali ipo imara na tunaenda imara na tutafika tukiwa imara

Mzee Pinda tunakushukuru sana, wewe ni mtu mwenye moyo wa pekee, nilikuwa nakuona kama Padri hivi, nikakutoa nikakupeleka kwenye Uchungaji nikakutoa nikakupeleka kwenye Ushekh nikaona niyajumlishe yote. Wewe ndio wewe

Mzee Pinda you are too special, watanzania wanakuheshimu sana na watakukumbuka kwa ukarimu wako. Na ndio maana unaonekana kijana kabisa ni kwa sababunmoyo wako umetulia hujipi presha unafanya kile unaamini. Na mimi ikifika siku yangu ya kustaafu nitakuj akuchukua ujuzi kwako

Kwa viongozi wengine nawashukuru sana. NMb nawashukuru ila gawio liongezeke. PSPF nawapongeza sana kuunganishwa kwa hizi hifadhi za jamii wala kusiwape wasiwasi tunafanya mambo kwa faida ya wote wala msiwe na wasiwasi na position zenu
 
Rais Magufuli muda huu anazindua jengo la PSPF na tawi la benki ya NMB Kambarage Mjini Dodoma. Ujenzi wa jengo hilo mpaka kukamilika imegharimu Tsh. Bilioni 30.5

Dbd4Cv8WsAAhPWI.jpg

Dbd4FXDW4AAHx27.jpg


UPDATE
 
Makongoro Nyerere:
Mheshimiwa Rais chapa kazi wanaokurudisha nyuma wapo na tumeshawazoa toka zamani. Wapo watu alinifuata wakasema "Ee bwana Makongoro, huyu huyu mheshiwa yupoje huyu? Toka ameanza kazi mbona hakuchagui?" Ili nichukie

Lakini kwa kuwa mimi ni mchezaji, kwani aliyesema mimi sio mchezaji nani? Nipo nafasi yangu inaitwa mchezaji wa akiba
Makongoro, bora angeuchuna tu ......... huyu wa safari hii ukijifagilia ndiyo kabisa anakutosa.

Hata huko Butiama watamuona tena 2020 ..!!
 
Mungu amjalie Afya Njema Rais wetu kipenzi cha Watanzania. Mungu azidi kuwasambaratisha Wavaa Nguo za Khaki zenye mifuko mingi na Vishikizo Vikubwa. Amen!
 
Back
Top Bottom