Dodoma: Rais Magufuli apiga simu mubashara kwenye Kongamano la CWT na kukanusha kufutwa kwa Ualimu Ngazi ya Cheti

Tengeneza tatizo kila litatue ili upate kiki, hivi kweli kuna mtendaji anaweza toa maamuzi Kama hayo bila ruhusa toka juu
 
Huelewi wewe! Usisahau Ndalichako alivyoua elimu wewe. Hii kitu ilitakiwa kupelekwa katika baraza la mawaziri wewe!!!!
Naam, na Ndalichako ni mvamizi serekalini siyo?. Au unathibitisha kuwa tuna serekalini isiyo ratibiwa??
 
Unaweza sema huyo mama kakosea timing ya tangazo maana alitakiwa asubili uchaguzi upite pia hata Kama ingewagharimu wanafunzi sio mbaya mabadiliko yangewakutia chuoni,hii ingemsaidia kwa sasa na kujirefend hapo baadae kuliko kutoa tangazo sasa ambapo kwa mwanasiasa dizaini ya Magu hangemvumilia
Pili kwa dizaini hii ya wasomi wetu si ajabu wanahitimu phd au masters lakini hawawezi kuajirika huko duniani maana kila kitu ni siasa.TL fumua elimu hii ni upuuzi mtupu haimsaidii mtu kuwa na sifa za kuajirika na kuajiri.
 
HIVI KARIBUNI UTASIKIA ANAKANUSHA SUALA LA VITAMBULISHO VYA WAJASILIAMALI!
Press release ilishatoka zamani imesainiwa na Msigwa kwamba rais kapiga marufuku kuwauzia wamachinga vitambulisho na eti waliouziwa warudishiwe pesa zao kwamba utaratibu ulikiukwa wakati yeye ndio alikuwa anashadidia wauziwe kwa bei tajwa na kila mkoa ulipangiwa kiwango 😆😆😆😆
 
Magufuli ni mshamba ile mbaya anafikili bado tupo enzi za miaka ya 1970 ambapo aliye kuwa na uwezo wa kuangalia tv alikuwa Nyerere peke yake. yaani hiyo anatengeneza tatizo halafu anakuja kulitatuwa ili aonekane kama superhero. akili ya kitoto kwelikweli. amewatuma watu waandike baruwa halafu baadaye aje aitenguwe ili walimu wamshagilie kuwa amewaokowa.
Kikokoto oyeeeeee
 
Huyu hapati kura yangu, ni miaka mitano sasa ninasubili mshahara Mpya, hata ile annual increment imekuwa shida. Kura yangu ni kwa Lissu tu.
kwa tija ipi unayotoa?kutwa unashinda mitandaoni,saa 4 unakunywa chai na vitumbua hadi saa6,saa7 unaenda lunch hadi saa 9,hujibu emails wala barua za kiofisi mpaka mwananchi aje kukuona
 
kwa tija ipi unayotoa?kutwa unashinda mitandaoni,saa 4 unakunywa chai na vitumbua hadi saa6,saa7 unaenda lunch hadi saa 9,hujibu emails wala barua za kiofisi mpaka mwananchi aje kukuona
Kura yangu hata iweje hapati tu
 
sawa ni haki yako lakini usisingizie mshahara.saa hizi ulitakiwa uwe ofisini uwe ofisini,saa 1.30 asubuhi uanze kazi lakini unahangaika humu,nani atakupandisha mshahara
Tumeteseka kwa miaka 5 kura yangu ni kwa Lissu tu, hata stahiki zangu zilizo kisheria imekuwa shida kizipata.
 
Magufuli hana mawasiliano na taasisi za serikali yake?
Taasisi ziko huru, zinapofanya vizuri always no changamoto but wanapoleta taharuki shida inakuwa kubwa ndo hapo anapoweza hitaji kupata briefing kutoka kwa Waziri au KM. Siyo kila kitu Lazmi ajue. Kinapoleta taharuki as now baba ndo anaibuka kuonyesha uwepo wake
 
Back
Top Bottom