Dodoma: Rais Magufuli apiga simu mubashara kwenye Kongamano la CWT na kukanusha kufutwa kwa Ualimu Ngazi ya Cheti

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,104
Leo tarehe 5 Oktoba, katika Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani lililoandaliwa na CWT, Dodoma, Rais John Pombe Magufuli alipiga simu 'live' na kuongea na washiriki wa kongamano na pia kukanusha kufutwa kwa ualimu wa ngazi ya cheti.

Rais Magufuli amewataka walimu kupuuza taarifa hiyo na kusema kuwa tangazo hilo ni la kipumbavu na kwamba ataendelea kuwa pamoja na walimu wote.

Rais.jpg

PIA SOMA: Siku ya Mwalimu Duniani: Wizara ya Elimu yafuta rasmi mafunzo ya Ualimu wa shule ya msingi na awali ngazi ya Cheti Tanzania
 
Rais Magufuli amewataka walimu na watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa zinazodai kwamba serikali imefuta mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti kwa shule za msingi na awali, na kwamba mafunzo hayo sasa yataanzia ngazi ya Diploma.

Rais Magufuli ameliita tangazo hilo kuwa ni la kipumbavu.

Source: Swahili Times

Maendeleo hayana vyama!
 
Aiseh Elimu yetu IPO mashakani

Hivi inawezekanaje wizara iamue X walio nje ya wizara ambao kimsingi sio wataalamu waamue Y?

Na kwann hawa wataalamu hawawahusishi wadau wote kabla ya kuja na matamko yao ya mwendokasi kama haya

This could no longer be called 'A profession'
Poor us!!
 
Kiki za ajabu sana! Kwani Wizara ya Elimu (iliyofuta ngazi ya cheti) na Rais wako serikali tofauti? Si ni serikali hiyo hiyo moja? Ajabu sana hii! Vinginevyo, kama hiyo habari (ya kufutwa ngazi ya cheti) ni ya uongo itakuwa ilizushwa na "kitengo" kama sehemu ya maandalizi ya kiki ya leo.
 
Ila aliyetoa tangazo hilo ni Dkt. Avemaria ambaye ni Naibu katibu mkuu wa wizara ya Elimu.
 
Hivi hadi katibu mkuu wizara anatoa tamko inamaana alijitolea tuu au lilikuwa kwenye mpango linafahamika na waziri wake pamoja na baraka la baraza la kawazidi? Na kama alijitolea mwenyewe tu je kuna mangapi maamuzi yamefanyika kwa utashi tu wa mtu?

Kuwaambia watu wapuuze nadhani ni kosa kubwa lakiufundi kwenye utendaji mzima hakuna credit yoyote unayopata zaidi yakupoteza point
 
Ukiangalia kwa jicho la tatu sio uamuzi wa kipumbavu kama alivyosema yeye, ingekuza kiwango cha elimu lakini imekuwa wazo la kipumbavu kwake kwa maana yupo kwenye kampeni na atakosa kura ndo maana kapiga simu live.

Ingawa wengi watakosa ajira lakini siyo wazo la kipumbavu angetumia maneno ya busara kidogo.
 
Back
Top Bottom