Dodoma: Rais Magufuli anazindua ujenzi wa barabara ya Mtumba, Makao Makuu ya TARURA na Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto

Kasema hataki kuongezewa muda atafuata katiba ya nchi ili awachie wenzake, sasa sijui wale vigaguro wanaongea nin kama mashosho.
 
Kuwapa Maofisa Tarafa pikipiki ni jambo zuri sana lakini kwa siku za mbele ni vyema hawa Maofisa nao wapatie usafiri wa magari japo ya bei nafuu na yenye uwezo wa kumuda mazingira ya vijijini.
Vijijini vijiji vingi Tanzania Kuna barabara? Hayo magari ya kuhimili vijijini ya Bei nafuu Ni yepi hayo?
 
Naomba ushuri na maoni kwangu nashangaa siku ya bajeti naona matangazo ya rais akifanya uzinduzi wa barabara na majengo lakini katika mkoa huo huo kuna usomwaji wa bajeti ya taifa. Haipewi kipaunbele kabisa.

Ivi kati ya ivyo viwili kipi kina maslai kwa raifa?
 
Naomba ushuri na maoni kwangu nashangaa siku ya bajeti naona matangazo ya rais akifanya uzinduzi wa barabara na majengo lakini katika mkoa huo huo kuna usomwaji wa bajeti ya taifa. Haipewi kipaunbele kabisa.

Ivi kati ya ivyo viwili kipi kina maslai kwa raifa?
Hapo ndio ujue kuna bajeti ya kibwege sana
 
Bajeti inasomwa saa kumi na itakuwa live.

Huo uzinduzi ni saa ngapi na unarushwa saa ngapi?
 
Kuwapa Maofisa Tarafa pikipiki ni jambo zuri sana lakini kwa siku za mbele ni vyema hawa Maofisa nao wapatie usafiri wa magari japo ya bei nafuu na yenye uwezo wa kumuda mazingira ya vijijini.
Pikipiki inapita chocho zote,,mbadala wake labda wapewe V8
 
Ujenzi bila archtectural drawings sio ujenzi..

Rais Magufuli yupo sherehe za kuzindua ujenzi wa 51.2 km za barabara ya mji wa kiserikali wa Mtumba, mkoani Dodoma

Barabara hiyo itakuwa na km 11.2 za njia nne, zenye upana wa mita 7 kila upande

Katika sherehe hizo pia kutakuwa na uzinduzi wa Jengo la ofisi za TARURA mji wa Mtumba, katika sherehe hiyo Maafisa tarafa watakabidhiwa pikipiki 480
===

Katika tukio la kwanza la uzinduzi wa Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami inayotarajiwa kuwa na Urefu wa KM 51.2 Rais Magufuli alianza na kupewa ufafanuzi kwa kuoneshwa ramani wa namna barabara hiyo itakavyokuwa. Adha, Baada ya kuoneshwa ramani Rais aliweka jiwe la msingi na kisha kupiga picha na viongozi na mbalimbali.

Baada ya tukio hilo, Rais aliondoka na kuelekea katika uzinduzi mwingine wa jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya wakala wa barabara za mijini na vijijini Katika tukio hilo, Viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo walipata nafasi ya kufungua tukio hili kwa maombi ambapo viongozi hao walianza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu pamoja na kumuombea Rais Magufuli.

Suleiman Jaffo
Kuweka fedha hapa zaidi ya bilioni 89.1 ni jambo la kipekee

Barabara hizi zitakuwa za kipekee. Eneo hili ndani ya miezi 18, kilomita 51, ni barabara zenye uwezo wa kubeba malori na mitambo mbalimbali zitakuwa tayari

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI
Rais amewataka wahudhuriaji kusimama na kumkumbuka Rais Nkurunzinza na wanane waliofariki hapo hapo kwa kugongwa na Lori

Leo nimefarijika kualikwa kuja kuweka jiwe la msingi kwenye barabara hizi ambazo zitagharimu bilioni 89.132, ambazo nimeambiwa zitapambwa na mambo mbalimbali na kuacha maeneo ambayo treni na magari ya mwendokasi yatapita

Bara bara hizi zitapambwa na mambo mbalimbali ikiwamo pamoja na kuacha maeneo ambayo treni na mabasi ya mwendo kasi yatapita. Lakini pia nimeambiwa patawekwa taa zaidi ya mia saba na kitu na patapandwa matunda ya aina mbalimbali.

"Nina uhakika watoto wangu na watani wangu Wagogo watakuwa wanaokota matunda tu barabarani badala ya kuokota mabuyu."

"Wapo watu ambao hawakuamini katika maisha yao kwamba itawezekana Dodoma kuwa ndio makao Makuu ya nchi kwa sababu saa nyingine kuamini ni kugumu sana".

"Nakumbuka niliposema tutahamia Dodoma ndani ya miaka mitano wapo waliosema kwamba ni ndoto za mchana. Mimi huwa sioti mchana naota usiku tu"

"Mpaka sasa hivi Watumishi zaidi ya 13,361 wameshahamia hapa. Ni pamoja na Watumishi wangu wa Ikulu wote pamoja na mimi, Makamu wa Rais, Mawazairi, Makatibu Wakuu wote wako hapa. Kwahiyo, suala la kusema tunajaribu halipo tena. Dodoma ndio makao Makuu ya Nchi. Na kwa hili nalipongesa sana Bunge kwa kupitisha Sheria kuwa Makao Makuu ya Nchi ni Dodoma"

"Kwahiyo, hata nikiondoka mimi Rais atakayekuja hatahamisha Makao Makuu Dodoma, atakaa hapa Dodoma. Kwahiyo, ni amri Dodoma ndio makao Makuu."

Mafanikio ya Bararabara haya ni asilimia 100 fedha ya serikali'

"Ujenzi wa nyumba hizi nzurunzuri za Mawaziri mbalimbali pamoja na nyumba za Mabalozi zimeufanya Mji wa Dodoma kuwa kweli Mji wa kisasa."

"Dodoma imependeza, hata wanawake wa Dodoma walikuwa weusi wamekuwa weupe. Watani zangu Wagogo wamebadilika kwa sababu ya kuwa na makao makuu hapa".

Kwa sasa kuna mradi mkubwa wa kilomita 100 wa barabara utakaogharimu mabilioni zaidi ya 600. Utazunguka Dodoma hii. Tumetangaza tenda na fedha zipo zimetolewa na African Development Bank

Tumepata Bilioni 500 kujenga uwanja wa ndege mkubwa kama wa Dar es Salaam

"Nitoe Tahadhari: Mumejenga jengo la makao makuu. Sasa sio kila mahali mujenge majengo ya Tarura. Hizi fedha zilianzishwa kwa mujibu wa sharia, na fedha hizi lazima zitumike kujenga barabara."

"Mukianzisha miradi ya kujenga tu nyumba inawezekana kusudi la kuanzishwa likabadilika. Kwenye wilaya huko mutumie majengo ya serikali."

MSAMAHA WA DENI LA IMF
Leo ninavyozungumza tumepata fedha za msamaha. Bodi ya Wakurugenzi ya IMF imeidhinisha leo msamaha wa USD 14.3 milioni za madeni tuliyokuwa nayo. Na kwasababu tulipambana vizuri na ugonjwa wa Corona. Msamaha huu umekuja wakati muafaka.

Nimepanga leo nitamwandikia barua mkurugenzi mkuu wa IMF kumshukuru kwa niaba ya Watanzania na kumweleza kuwa fedha hizi tutazitumia katika kuendelea kupambana na corona lakini pia katika kushughulikia maeneo mengine ambayo ili kusaidia Corona isije tena.

Ukishatengeneza barabara nzuri, watu wakapita haraka, hata yule mdudu wa Corona hawezi kumsogelea yule anayekimbia haraka.

Ukishatengeneza hospitali nzuri au uwanja wa ndege mzuri, Corona itapotea. Hata ukilipa mishahara au ukasaidia, itasaidia Corona isitupate haraka.

KUGAWA PIKIPIKI KWA MAAFISA TARAFA
Ndugu zangu nimekuja hapa pia kugawa pikipiki. Katika kikao chetu na Watendaji wa tarafa, kikubwa walichokuwa wanahangaika nachomaafisa tarafa 570 ni usafiri. Hawa ni viongozi muhimu. Waliniambia kwenye mkutano ule kuwa hawana pikipiki, kitu ambacho ni nyenzo muhimu katika utendaji wa kazi zao.

Tulitoa bilioni moja zikatumike kununua pikipiki katika mikoa yote ya Tanzania. Nimeshuhudia kwenye Tv pikipiki zikigawiwa kwenye maeneo mbalimbali ya mikoa yetu na wilaya zetu.

Leo nimekuja kushuhudia mwenyewe kwamba katika pikipiki zilizopangwa kununuliwa 300 na kitu, zimenunuliwa 448. Nawashukuru wote waliohusika katika mchakato wa kupata hizi pikipiki. Kwa pikipiki zilizokuwepo pamoja na hizi mpya, hakyuna Katibu Tarafa au Ofisa Tarafa ambaye atakosa. Wote 570 watakuwa wamepata pikipiki.

Niwaombe maofisa tarafa wazisimamie vizuri. Zisiende kuharibiwa au kutumika kama daladala. Zikafanye kazi za serikali.

Maofisa wangu wa Tarafa musizitumie pikipiki hizi mukiwa mumelewa, zisitumike kubeba mishkaki. Zikatumike katika kazi za maendeleo ya tarafa husika.

Nikuombe waziri na wote munaohusika, kila atakayekabidhiwa akabidhiwe kwa maandishi – asaini, ili kusudi akiiharibu au ikipotea ailipe. Hakuna vya bure Tanzania. Hizi ni fedha za walipa kodi wa Tanzania. Watanzania masikini wamechanaga bilioni 1 kurahisisha utendaji wa maofisa tarafa.

Hata kama ni ofisa tarafa mwanamama, usiiache hiyo pikipiki – utakuwa unapakiwa hata na mume wako au mshkaji wako unapoenda kufanya kazi. Ili mradi ukafike kushughulikia matatizo ya wananchi katika tarafa ile. Natumai zitatunzwa ili baadaye watendaji wengi wa serikali wapate usafiri wa kuwarahisishia kazi zao.

UCHUMI
Napenda kuwahidi kuwa Tanzania tupo mbele, tunaenda vizuri. Ni miongoni mwa nchi 5 Afrika ambzo uchumi wake unakwenda vizuri.

Watanzania wote popote mulipo, tembeeni kifua mbele kwasababu taifa linakwenda vizuri.

KUNG'ATUKA KWA MUJIBU WA KATIBA
Nami kama kiongozi muniombee, nisiwe na kiburi, nisiwe na jeuri. Nikawe mtumishi wa kweli kwa Watanzania wote bila kuwabagua kwa rangi zao, kwa dini zao, kwa makabila yao. Nikatimize wajibu wangu katika kipindi ambacho kimepangwa kwenye Katiba, ili kusudi baada ya hapo tuwaachie wengine watakaokuja watimize wajibu wao.

Nataka kuwahakikishia Watanzania ninawapenda lakini pia nataka niwahakikishie kazi hii ni ngumu sana. Ina mateso sana. Inahitaji sala. Inahitaji dua. Inahitaji nguvu za Mwenyezi Mungu. Kwenye hilo ndugu zangu, naomba muendelee kuniombea na mimi naendelea kuwaombea.

KUHUSU CORONA
Tunamshukuru Mungu kwa kutuepusha na igonjwa huu wa Corona. Mambo yanakwenda vizuri. Tusidharau dawa za kienyeji. Tusidharau hata kidogo; uchawi tu ndiyo mbaya lakini miti yote iliumbwa na Mungu kwa ajili ya kutusaidia sisi.

Nimetoa maelekezo kwa Wiizara ya Afya kile kitengo cha madawa ya asili kiendelezwe kwa nguvu zote na bajeti yake iongezwe. Watu wanapotengeneza madawa yao tusiwadharau. Kuna tendency watu wakitengeneza madawa yao munawaambia wamepitwa na wakati, wewe ndiyo umepitwa na wakati.

Tulipumbazwa tusiamini kilicho chetu na tuamini kilicho chao. Niwaombe Watanzania tubadilike.

Tuwasapoti wanaofanya kazi halali kutumia dawa za asili. Hata ukienda kwenye nchi zilizoendelea kuna dawa za kisasa na za asili.

Kujifukiza kumesaidia sana. Corona bado haijaisha sana lakini imepungua sana. Tuendelee kuchukuwa tahadhari.

Wale waliotegemea kuwa tutakufa sana na kwamba barabarani kutakuwa na maiti wameshindwa na wakalegee kikwelikweli. Mungu wetu anatupenda na tukaendelee kumtegemea Mungu wetu.

Yatazungumzwa mengi na watu wao wanaowatumia. Ninyi msikate tamaa, endeleeni kuchapa kazi.

UZINDUZI JENGO LA JESHI LA ZIMAMOTO DODOMA
Tukio hili lilifunguliwa na maombi kutoka kwa viongozi wa dini kwa kufanya maombi ambao wametumia nafasi hiyo kuliombea taifa, kumuombea Rais na kumpongeza katika mambo mbalimbali.

Baada ya Maombi Rais Magufuli alizungumza masuala mbalimbali:

"Hata aliyekuwa Kamishna wenu, simrudishi Fire lakini nitamtafutia kazi. Ameshaniomba msamaha mara nyingi. Niwaombe sana ndugu zangu wa Jeshi hili, yaliyopita si ndwele tuyasahau na tusiyarudie."

"Simwanza wewe ulikuwa unaondoka, nimekusamehe na wengine sitaki kuwataja majina hapa. Nafanya haya kwa unyeyekevu mkubwa na kumuogopa Mungu. Sisi wote ni wadhambi. Unapomuona mtu anaonesha dalili za ku-repent, msamaha lazima utoke."

"Majeshi yetu ni 'Super'. Na ndio maana niwaombe Makamanda wa Jeshi la Zimamoto najua mmepitia kwenye changamoto nyingi - Hususan katika ule mradi wa ajabu mlioufanya na Kamishna Jenerali aliyekuwepo nikamtoa. Nashukuru mmefanya marekebisho ya kutosha."

"Nafahamu palikuwa na mapendekezo ya Makamishna kama wanne hivi kuwateremsha cheo na wengine hata kuwafukuza. Nimeangalia kwanza mnavyopendeza, mlivyo na huruma na upendo mkubwa wa kuchapa kazi na nyuso zenu zinanionesha kuwa mmetubu. Nimewasamehe leo."


 
Back
Top Bottom