Dodoma: Rais Magufuli akivunja sheria za barabarani wakati akitokea ofisi za CCM alipoenda kuchukua fomu ya urais

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Hatimaye kampeni zimeanza, tumeanza kujishusha kwa wananchi. Haya maving'ora kwa sasa yatatupunguzia kura.

Rais Magufuli leo anaonekana Dodoma akiwa na gari binafsi huku akitanua bila wasiwasi wowote.
 
Rais Magufuli muda wote yupo Tanzania na Wananchi anawatumikia

Labda yule jamaa anayehutubia Facebook ndio anatakiwa aje ajishushe
Huyu
FB_IMG_15923955080558615.jpg
 
Kitu ambacho hujajua wewe mleta mada ni kuwa raisi alikwenda kwenye shughuli yake binafsi. Na kitu kingine hakutaka kuweka attention ya watu ndio maana wengi mmejua kuwa kachukua fomu baada ya taarifa kutolewa na vyombo rasmi vya CCM.

Halafu kusema kuwa kavunja sheria za barabarani si sawa, barabara inaweza kutumika kivyovyote inategemea na mahitaji ya wakati huo. Halafu hizo gari zimembeba mkuu wa nchi, kiprotokali mkuu wa nchi hawezi kukaa kwenye foleni, si kwa sababu ya heshima bali kwa sababu ya usalama wake.
 
Kitu ambacho hujajua wewe mleta mada ni kuwa raisi alikwenda kwenye shughuli yake binafsi. Na kitu kingine hakutaka kuweka attention ya watu ndio maana wengi mmejua kuwa kachukua fomu baada ya taarifa kutolewa na vyombo rasmi vya CCM. Halafu kusema kuwa kavunja sheria za barabarani si sawa, barabara inaweza kutumika kivyovyote inategemea na mahitaji ya wakati huo. Halafu hizo gari zimembeba mkuu wa nchi, kiprotokali mkuu wa nchi hawezi kukaa kwenye foleni, si kwa sababu ya heshima bali kwa sababu ya usalama wake.
Thread closed
 
CHADEMA hamnaga akili. Hicho ki wimbo cha kwenye Clip kinaipromote CCM, Ila umekurupuka speed kuanzisha thread isiyo na kichwa wala miguu. Ndo maana wakati mwingine Tanzania Daima inaandikaga habari za CCM front page bila kujua inaipigia debe CCM.
 
Hii sasa inabidi Mwanasheria Mkuu Serikali abebe jukumu baada ya sheria ya kinga ya viongozi kutoshitakiwa kupitishwa. Zamani angeweza kushitakiwa kama John Pombe Joseph Magufuli

Jaji Samatta: Rais Mstaafu anaweza kushitakiwa
By
Mtanzania Digital
-
March 17, 2019

maxresdefault-2-1024x515.jpg

Awaasa wenye siasa za malengo, tamaa Ikulu

NA AZIZA MASOUD-DAR ES SALAAM

JAJI Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inaonyesha kuwa Rais Mstaafu anaweza kufunguliwa mashtaka mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kutokana na kile kinachoitwa ‘kinga ya urais’ kuwa na mipaka yake.

Jaji Samatta ambaye amepata kuwa Jaji Mkuu kwa takribani miaka saba kabla hajastaafu mwaka 2007 alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwasilisha mada ya ‘Uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika vyombo vya dola pamoja na utekelezaji wa sheria na utoaji wa haki’ katika kipengele cha wajibu wa Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) na Takukuru kwa wanafunzi wa Shule ya Sheria nchini.

Akiwasilisha mada hiyo katika mkutano wa uwajibikaji ulioandaliwa na taasisi isioyo ya serikali ya Wajibu, Jaji Samatta ambaye amekuwa akisifika kwa misimamo na kusimamia haki alirejea Ibara 46(3) ya Katiba akisema kinga aliyopewa Rais katika ibara hiyo haihusu vitendo Rais alivyovifanya akiwa Rais lakini inahusu vitendo alivyofanya kama Rais.

“Ni ukweli kuwa chini ya Katiba ya nchi hii Rais Mstaafu anaweza kufunguliwa mashtaka Mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).Ni muhimu sana ukweli huu ukaeleweka.

“Ni sahihi kabisa kusema kuwa chini ya Ibara 46(3) ya sheria mama hiyo rais aliyeacha madaraka ana kinga dhidi ya mashtaka, hata hivyo kinga hiyo ina mipaka. Inahusu tu “jambo …..alilofanya……kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba…..”kinga hii haihusu vitendo alivyofanya Rais akiwa Rais,lakini inahusu vitendo alivyofanya kama Rais,”alisema Samatta.

Alisema kuna tofauti kubwa na iliyo wazi kati ya maneno ya ‘akiwa’ na ‘kama’,kwa mujibu wa kifungu hicho cha Katiba aliyekuwa rais hana kinga dhidi ya mashtaka kuhusu jambo lolote ambalo hakufanya kama Rais.

“Kuhusu jambo la aina hiyo Mkurugenzi wa mashtaka ana mamlaka ya kumfungulia mashtaka na mahakama zina mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi hiyo kama ilivyo kwa kesi za jinai zinazoweza kufunguliwa dhidi ya watu wengine nchini.

“Kwa mfano kama alipokuwa madarakani Rais aliamua siku moja kuendesha gari yeye mwenyewe na akamgonga mtu na kusababisha kifo chake kutoakana na uzembe mkubwa kinga chini ya Ibara 46(3) ya Katiba haitamwokoa kutokana kwenye mashtaka ya kitendo hicho,vitendo vya ufisadi navyo vitakosa kinga hiyo,”.

Katika hilo hilo, Jaji Samatta alikwenda mbali na hata kuwaasa wale aliowaita wenye siasa za malengo au tamaa ya kuwa mpangaji Ikulu akiwataka watambue fika kwa faida ya nchi,ukweli huo.

Alisema watawala pia wanapaswa kuzingatia kuwa safari yao ya kuelekea huko na wakati wote watakapoongoza nchi kwenye jumba hilo kwamba ukweli ni kuwa Rais aliye madarakani hana mamlaka ya kutoa msamaha kwa mhalifu yeyote kabla hajapatikana na hatia mbele ya mahakama isipokuwa tu kama ibara ya 45(1) ya Katiba itabadilishwa kumpa mamlaka hayo.

Alisema hakuna shaka yeyote kuwa ofisi ya DPP ni moja ya ofisi kuu muhimu ndani ya dola hivyo jinsi Katiba inavyoelekeza ndivyo inavyopaswa kuwa katika nchi yenye kufuata utawala wa sheria.

“Ofisi ya DPP ikiyumba na utawala huo utatereka vibaya, hilo likitokea hakuna mwananchi ambaye hataathirika kwa namna moja au nyingine, moja ya malengo ya sheria ni kumpa DPP uhuru katika kutumia mamkala yake na kuhakikisha hakuna woga, uonevu au upendeleo katika kuamua mshukiwa ashtakiwe au mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya mtu huyo yafutwe au laa,”alisema Jaji Samatta.

Alisema utenganisho huo wa mamlaka hayo pia unalenga kuzuia siasa kuingilia au kutumika katika masuala hayo nyeti na kitaalamu.

Alisisitiza kuwa ofisi ya DPP haipo kwa lengo la kuhakikisha kuwa mshukiwa lazima ashitakiwe au mshitakiwa lazima aonekane na hatia.

Alisema DPP na maafisa walio chini yake ni watumishi wa nchi ambao wajibu wao ni kulinda maslahi ya umma yakiwemo yale yanayohitaji mtu asiye onyeshwa na ushahidi kuhusika na utendaji wa kosa la jinai hashtakiwi na mshitakiwa ambaye ushahidi dhidi yake hauthibitishi kwamba alitenda kosa hatiwi hatiani.

Alisema kutumia njia za uonevu na udanganyifu hakuwezi kuyafanya mapambano dhidi ya uhalifu likiwemo kosa la rushwa yafanikiwe kinyume chake hatua hizo zitafanya mapambano dhidi ya uhalifu kutofanikiwa na chuki dhidi ya watawala kujengeka.

“Mwananchi aliyeshitakiwa na kosa la rushwa na inaonekana na mahakama kuwa haijathibitishwa kutenda kosa hilo ana haki ya kuachiliwa ,kama mshitakiwa aliyeshitakiwa na kosa lingine lolote na ushahidi dhidi yake unaposhindwa kulazimisha atiwe hatiani.

“Wakati mwingine siku hizi ninaposikiliza taarifa ya habari kupitia vituo vya televisheni napata picha kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wanateka mamlaka ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, bila shaka yoyote hatua hizo ni kinyume cha Katiba na zinaweza kusababisha viongozi wakahukumiwa kama watafunguliwa kesi za madai mahakamani na kuwalipa wanaonewa,”alisema Jaji Samatta.

Alisema hatua hizo za watawala zinaweza kusababisha kuharibika kwa kesi ambazo vinginevyo zingeweza kuthibitisha hatia za washtakiwa, uovu huo unaweza kutokea hata kwenye kesi za rushwa na mapambano dhidi ya uovu huo lazima yafanyike kisheria na si vinginevyo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa taasisi ya Wajibu ambaye ni Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Ludovick Utouh alisema a alisema lengo la taasisi hiyo ni kuongeza ushirikishwa wa wananchi katika suala zima la uwajibikaji.

Alisema aliamua kumualika Jaji Samatta kwakuwa ni mmoja kati ya viongozi waadilifu ambao wanaongea na kutenda vitu ambavyo wanaviamini na kwamba ni miongoni mwa watu wanaochukia rushwa kutoka moyoni.

Alisema mkutano wa jana ambao ni wa tatu baada ya kufanyika mikutano mingine mwishoni mwa mwaka jana katika Chuo Kikuu Dodoma pamoja na Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo Morogoro ni muendelezo wa kutoa elimu kuhusu uwajibikaji kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Mwisho

Source : Jaji Samatta: Rais Mstaafu anaweza kushitakiwa | Mtanzania
 
Kitu ambacho hujajua wewe mleta mada ni kuwa raisi alikwenda kwenye shughuli yake binafsi. Na kitu kingine hakutaka kuweka attention ya watu ndio maana wengi mmejua kuwa kachukua fomu baada ya taarifa kutolewa na vyombo rasmi vya CCM. Halafu kusema kuwa kavunja sheria za barabarani si sawa, barabara inaweza kutumika kivyovyote inategemea na mahitaji ya wakati huo. Halafu hizo gari zimembeba mkuu wa nchi, kiprotokali mkuu wa nchi hawezi kukaa kwenye foleni, si kwa sababu ya heshima bali kwa sababu ya usalama wake.
Mkuu umeandika vizuri sana. Nimelike lakini nimeona haitoshi mpk niandike kwa maneno
 
Huyu mtu wausalama kaniacha hoi, anakimbia sambamba na hiyo V8, halafu huyo trafik haamini macho take kuwa JPM anasukuma mkoko mwenyewe, good work JPM
 
Ingekuwa Lowassa au Ridhiwani na babaake wangechukua msafara wa Bajaji za Dodoma nzima.

Kwa hilo namsifu.
 
Back
Top Bottom