Dodoma: Rais Magufuli achangia M10 kwenye harambee ya ujenzi wa Kanisa

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
7,892
14,347
Rais Magufuli amewashukuru Viongozi wa Dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba Mungu ili aliepushe Taifa na corona, ametoa shukrani hizo leo alipokaribishwa kuwasalimu Waumini wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata,Chamwino, Dodoma.

“Mungu amejibu maombi ya Watanzania ambao wamesali, wamefanya toba na kufunga, na matokeo yake maambukizi ya corona yamepungua na wananchi wanaendelea na maisha yao huku wakichapa kazi, tofauti na ilivyodhaniwa kuwa corona ingesababisha madhara makubwa”-JPM

Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuwa makini dhidi ya mbinu zozote zinazoweza kufanywa kuwaambukiza corona ama magonjwa mengine, huku wakimshukuru na kumtumaini Mwenyezi Mungu aliyemuwez wa yote.

Akiwa Kanisani hapo, JPM ameendesha harambee ya kuchangia upanuzi wa Kanisa hilo na kufanikiwa kuchangisha zaidi ya Tsh. Mil 17 ikiwemo Tsh. Mil 10 aliyochangia yeye mwenyewe na mifuko 76 ya saruji, ametaka upanuzi wa kanisa uanze kesho.

JPM for 2020-2025
 
Barakoa mbona imekaa kama titi moja la Mtu mmoja hivi limekatwa upande mmoja, weka huku kama...-Magu.
 
Rais Magufuli amewashukuru Viongozi wa Dini na Watanzania wote kwa kuitikia wito wa kumuomba Mungu ili aliepushe Taifa na corona, ametoa shukrani hizo leo alipokaribishwa kuwasalimu Waumini wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata,Chamwino, Dodoma.

“Mungu amejibu maombi ya Watanzania ambao wamesali, wamefanya toba na kufunga, na matokeo yake maambukizi ya corona yamepungua na wananchi wanaendelea na maisha yao huku wakichapa kazi, tofauti na ilivyodhaniwa kuwa corona ingesababisha madhara makubwa”-JPM

Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kuwa makini dhidi ya mbinu zozote zinazoweza kufanywa kuwaambukiza corona ama magonjwa mengine, huku wakimshukuru na kumtumaini Mwenyezi Mungu aliyemuwez wa yote.

Akiwa Kanisani hapo, JPM ameendesha harambee ya kuchangia upanuzi wa Kanisa hilo na kufanikiwa kuchangisha zaidi ya Tsh. Mil 17 ikiwemo Tsh. Mil 10 aliyochangia yeye mwenyewe na mifuko 76 ya saruji, ametaka upanuzi wa kanisa uanze kesho.

JPM for 2020-2025

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwambie tuna video zake akiwa na yule disii hivyo akae kwa utulivu
 
Anafanya biashara gani mpaka atoe milioni 10 kirahisi-rahisi namna hiyo? angekuwa hata ameandika kitabu kama kina Marehemu Mengi au Mzee Obama tungesema anapata pesa kupitia mauzo ya vitabu. hizo pesa za kugawa barabarani anatoa wapi kama siyo anazipata kwa rushwa?
 
Back
Top Bottom