Dodoma: Rais Magufuli aagiza kuchunguzwa kwa Airtel kama ni mali ya TTCL! Wapotoshaji wa Takwimu wachukuliwe hatua kali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,876
Salaam Wana JamiiForums!



Leo Rais Magufuli ni mgeni rasmi katika kuweka jiwe la msingi katika jengo jipya la ofisi ya taifa ya takwimu.

Jengo hili litakuwa makao makuu ya NBS na sherehe hii ya uwekaji jiwe la msingi iko live katika TV 'Pendwa' ya TBC1.

Updates
Rais Magufuli asema takwimu ni muhimu kwa kila nyanja, apongeza Ofisi ya Takwimu kujengwa Dodoma

Rais Magufuli anasema:

"Tulipokuwa tunapata uhuru tuliambiwa kwamba umri wa mwisho wa kuishi ni miaka 41, kwa sasa tunaambiwa ni miaka 60, na mimi bado sijafikisha miaka 60...bado ninasiku za kuishi. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani takwimu ni muhimu"

"Ukuaji wa uchumi wetu unaendelea vizuri. Nusu ya mwaka huu nchi yetu imeongoza katika kanda ya afrika mashariki kwa kukua vizuri. Mfumuko wa bei mpaka mwezi November ulifikia asilimia nne."

"Ninasikia watu wanalalamika kwamba vyuma vimekaza. Ninaomba niwahakikishie kwamba vitakaza kweli kweli. Tutalegeza vyuma kwa wale ambao wako radhi kufanya kazi kwa juhudi. Tunachukua hizi hatua ili kutengeneza maisha mazuri ya watanzania"

"Mnasema vyuma vimebana, vitabana tu kwa wale waliokuwa wamezoea fedha za bure bure, na vitaedelea kubana kweli kweli. Tutabana vichwa, tutabana miguu, tutabana matumbo, tutabana kila kitu."

"Lakini kwa wale wanaochapa kazi, kwa mfano wakazi wa Lindi na Mtwara, walikuwa wanauza korosho saa nyingine kwa bei ya chini mpaka elfu 2 kwa kilo, sasa elfu 4 kwa kilo. Wale vyuma haviwezi vikabana, wale vyuma vimeachia, nasikia wanaamua hata mbuzi kuzinywesha bia, kule vyuma vimefungua."

"Kama serikali inafikia hatua ya kujenga reli yake kwa kutumia fedha za ndani, isingekuwa tumebana vile vyuma, zingekuwa zimeenda kunywewa bia, zingetumika hovyo."

"Ninawaomba Watanzania mpuuze uzushi unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii kwamba uchumi umeshuka. Tumieni takwimu zilizokusanywa na ofisi ya takwimu ya taifa. Achaneni na wanaosema vyuma vimekaza, tumelegeza kwa wananchi wa kawaida."

"Serikali inaendelea kuhakikisha kwamba kasi ya ukuaji wa uchumi inaenda sambaba na ukuaji wa hali ya uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja."

"Tunafanya mazungumzo na nchi ya Israel kuhakikisha kwamba tunanzisha kitengo cha huduma kwa wagojwa mahutui katika hospitali ya Benjamin Mkapa hapa Dodoma"

"Nyumba katika miji imeanza kushuka bei, walikuwa wanapangisha kwa dola tu ukiwa na shilingi hukubaliki, sasa wamebakia na maflat yao."

"Ikitokea mtu ametoa takwimu za uongo shikeni pelekeni mahabusu akajifunze kutoa takwimu wakati tunasubiri anapelekwa Mahakamani hiyo ndio direction yangu. Hatuwezi tukaunda sheria za takwimu bungeni, Spika akapitisha halafu mimi nikasaini na tusitumie."

"Hata wanaosema vyuma vimebana wakati ninyi watu wa takwimu mnasema vimeachia ni takwimu wapeleke wakaeleze vimekaza wapi. Ninyi ndio mnajua wapi vyuma vimepanuka kabisa kwa maslahi ya watanzania."

"Ninaomba kutoa onyo...hasa kwa wale ambao wanakuja na takwimu zao za mifukoni. Mamlaka husika mtumie sheria zilizopo kuwabana wale ambao wanataka kuwapotosha Watanzania kwa takwimu zao za uongo. Ukukosea kutoa takwimu...umeichafua nchi"

"Kifungu cha sheria kinasema atakayepotosha takwimu adhabu ni kifungo cha kuanzia miezi sita hadi miaka mitatu. Au faini ya Millioni moja hadi millioni kumi au vyote kwa pamoja. Tena mimi ningekuwa Jaji hii ya mwisho ndio ningetekeleza"

“Niwaombe vyombo vya habari na wataalam wa mitandao, muwaone wataaalm wanaohusika na takwimu, tusitafute takwimu za kupika"

"Waziri wa fedha, hakikisha unafuatilia suala la Airtel. Kwa taarifa nilizonazo Airtel ni mali ya TTCL Kuna michezo michafu sana inaendela hakikisha unafuatilia suala hili kabla ya mwaka huu kuisha"
 
Hili limedhihirika kila siku katika hotuba zake na nahisi ana ID JF. Muda huu anahutubia katika uzinduzi wa jengo la ofisi za NBS yaani National Beaural for Statistics ambapo ameelezea msemo wa vyuma kukaza kwamba ameona mchoro unaotembea kwenye mitandao ya kijamii ukionyesha vyuma vikizunguka huku oil ikiwa unamiminiwa kulainisha vyuma hivyo.

Rais ametolea mifano mingi inayotembea kwenye mitandao ya kijamii kitendo kinachoonyesha huyu ni mwanamitandao mwenzetu na narudia tena huenda ana ID yake hapa JF.

NAOMBA MODS WA JF WAWASILIANE NAYE ILI WAMSAIDIE RAIS KUWA NA VERIFIED ID HAPA JF ILI TUFURAHIE UWEPO WAKE MUBASHARA......
NAWASILISHA.
 
Hili limedhihirika kila siku katika hotuba zake na nahisi ana ID JF. Muda huu anahutubia katika uzinduzi wa jengo la ofisi za NBS yaani National Beaural for Statistics ambapo ameelezea msemo wa vyuma kukaza kwamba ameona mchoro unaotembea kwenye mitandao ya kijamii ukionyesha vyuma vikizunguka huku oil ikiwa unamiminiwa kulainisha vyuma hivyo.

Rais ametolea mifano mingi inayotembea kwenye mitandao ya kijamii kitendo kinachoonyesha huyu ni mwanamitandao mwenzetu na narudia tena huenda ana ID yake hapa JF.

NAOMBA MODS WA JF WAWASILIANE NAYE ILI WAMSAIDIE RAIS KUWA NA VERIFIED ID HAPA JF ILI TUFURAHIE UWEPO WAKE MUBASHARA......
NAWASILISHA.
Verified? Ili iweje?
 
Rais Magufuli amesema watu wanaotoatakwimu za uongo kuwa uchumi wa nchi umeyumba na kusema vyuma vimekaza wachukuliwe hatua

Amesema wapo wanaosema vyuma vimekaza wakati takwimu zianonyesha vyuma vimelegea wasiogopwe, wakamatwe waonyeshe ni wapi vimekaza

 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom