Dodoma: Polisi wanayashikilia magari 25 kukiuka amri ya IGP kwa kuyafunga magari yao ving’ora na taa kali

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
1594991985327.png
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma limefanikiwa kuyakamata magari 25 kwa kukiuka amri ya IGP kwa kuyafunga magari yao ving’ora na taa kali pamoja na gari jingine jipya aina ya Probox kukutwa likitumia namba ambazo zipo kwenye gari lingine.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Jijini Dodoma, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Giles Muroto amesema kuwa magari hayo yamekiuka amri ya IGP iliyoagiza kutokufunga ving'ora na taa kali kwa gari za kawaida bila utaratibu huku gari hilo jipya lilikamatwa likiwa na namba ya gari lingine linalopatikana Wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi mkoani humo limekamata zaidi ya mita elfu tatu za nyaya zinazomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, gari linalosadikika halikupatikana kihalali na masanduku mawili yaliyokuwa na bangi ikisafirishwa Jijini Tanga.

Akizungumzia kukamatwa kwa nyaya za umeme, Mhandisi Miradi ya REA awamu ya tatu mkoani Dodoma, Tumaini Chonya amesema kupatikana kwa nyaya hizo ni hujuma zinazofanywa na baadhi ya watu wachache.

PIA SOMA
= > Polisi waagizwa kuwakamata wanaofunga ving’ora na vimulimuli kwenye magari
 
Hv kweli king'ora unaweka kwenye gari yako binafsi cha nini hasa.....
huo ushamba.....
alafu gari za ajabu ajabu ndio wanaweka hizo mambo.....
huwezi kuta Range ama Ford ranger and the like wameweka hizo mambo michezo ya kina probox na akina swift hiyo
 
Sijawahi kuona mtu ana mercedes benz yake, bmw au audi ameweka hivo vitaa vya ajabu ajabu vimulimuli
 
Inatisha na kusikitisha sana kama ndiyo tumefikia hatua hii. Haki na huru aliyopigania baba wa taifa hili viko wapi sasa?
---

Msako magari yanayopiga ving'ora, kuwasha vimulimuli bila kibali

Jeshi la Polisi Jijini Dodoma limepiga marufuku magari ambayo si ya viongozi wa juu wa Serikali na ya Wagonjwa(ambulance) kupiga ving'ora na vimulimuli huku likisema limekamata magari 27 yakiwemo ya Serikali kutokana na kufanya vitendo hivyo
 
Kwa nini mpige ving'ora hovyo hovyo ?Mnaleta noise pollution. Kwa hili nampa bigup kamanda wa polisi.
Kwahiyo yale matarumbeta mnayopiga ktk harusi mkitoka kanisani na wakati wa kwenda na vile vigoma vya urugway kule buguruni ni nini?

Acheni double standard Ebo!
 
Halafu kuna vijana huwa wanazurura hovyo na mabint warembo...waombe vibali maana wanatukera sana sisi wenye ''material wife''
 
Hv kweli king'ora unaweka kwenye gari yako binafsi cha nini hasa.....
huo ushamba.....
alafu gari za ajabu ajabu ndio wanaweka hizo mambo.....
huwezi kuta Range ama Ford ranger and the like wameweka hizo mambo michezo ya kina probox na akina swift hiyo
Wenye vyombo vya usafiri ndio tabia yao sisi wenye magari hatuna huo ujinga
 
Wenye vyombo vya usafiri ndio tabia yao sisi wenye magari hatuna huo ujinga

Tena ungejua magari yaliyolengwa ni ya serikali

VX V8 na Nissan nyingi sio za SM/STK/SU ndo nyingi madereva wake wamefunga vile vimulimuli pale mbele kwenye grill kututishia wakianza mambio yao

Wala sio vigari vidogo kama mnavyosema
 
Tena ungejua magari yaliyolengwa ni ya serikali

VX V8 na Nissan nyingi sio za SM/STK/SU ndo nyingi madereva wake wamefunga vile vimulimuli pale mbele kwenye grill kututishia wakianza mambio yao

Wala sio vigari vidogo kama mnavyosema
Wazee wa 160km/hr hao kwenye vibao vya 50km/hr hao hawakamatwi mkuu
 
Back
Top Bottom